Navigate / search

Watu Wanaowaza Kwa Mtindo Huu Huongoza Kwa Kutofanikiwa

Kuna aina ya mawazo ambayo ukiwa nayo katika maisha yako huwa tayari yanakuwa kizuizi tosha kabisa cha wewe kuweza kuendelea mbele na kutoka katika changamoto ambayo inakukabili .Kumbuka maneno ambayo Albert Einstein alisema hauwezi kutatua matatizo yanayokukabili kwa sasa kwa kutumia kiwango kilekile cha ufahamu ambacho ulikuwa nacho wakati uanpata tatizo ulilonalo sasa.
Kuna aina moja ya kufikiri ambayo imewakwakmisha watu wengi sana na imewafanya washindwe kabisa kupiga hatua kutoka hapo walipo.Kuna watu wengi sana kwa sasa wakabiliwa na matatizo mbalimbali ambayo ukweli ni kuwa yamefikia kiwango cha kuwaonyesha kama vile hawataweza kutoka katika changamoto waliyonayo.
Inawezekana unaposoma kuna changamoto fulani inakukabili katika maisha yako-inawezekana ni changamoto ya kiafya,inawezekana ni changamoto ya kazini kwao,inawezekana ni changamoto ya kimahusiano na katika familia yako,inawezekana ni changamoto ya kifedha n.k Ila kitu kingine ni kuwa inawezekana kuwa changamoto hii imedumu muda mrefu sana na imefika sehemu ni kama vile unataka kukubali kuwa hakuna namna ambayo unaweza kuishinda kwani kila dalili na mzingira yanaonyesha hivyo.
Watu wengi wakifika katika mazingira haya kuna namna huwa wanaanza kufikiri ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa sana katika mafanikio yao na kuhakikisha kuwa wanatoka pale walipo.Huwa wanafikia sehemu na wanakubali katika akili yao kuwa hakuna namna wanaweza kutoka hapo walipo,wanafika sehemu na wanashawishika kuwa hakuna namna wataweza kuinuka tena.
Unachotakiwa kujua ni kuwa,mara tu utakapoanza kuamini namna hii kuna mambo mawili makubwa yatatokea:
Moja ni kuwa akili yako itaacha kufanya kazi kutafuta majibu ya changamoto ambayo inakukabili.Hii inamaanisha hata kama itataokea fursa ya wewe kuweza kupata suluhisho la changamoto inayokukabili,hautaweza kuiona kwani akili yako inakuwa imefungwa.Kumbuka kuwa macho yako hayaoni kila kitu bali kile tu ambacho huwa akili yako inakitafuta.Hii ndio maana unawesza kwenda mahali na ukamuona mtu fulani lakini baadaye ukianzwa kuulizwa alivaaje,uanweza kujikuta kuwa umesahau kabisa.Hii ni kwa sababu akili yako haikuelekezwa huko.Usikubali kuamini kuwa haiwezekani hata kama kwa sasa hakuna dalili yoyote yawewe kuweza kupata suluhisho unalolitafuta katika maisha yako.
Mbili ni kuwa unapofikia hatua ya kuona kama vile hakuna namna unaweza kufanikiwa tena ama kupata majibu ya changamoto unayoitafuta,basi kuanzia hapo mazingira,watu na fursa ambazo zilikuwa zijitokeze ili kukusaidia huwa zinapotea na kuwa mbali na wewe.Kitaalamu hii tunaita “Reppelling Effect”.Hii inamaansiha,mawazo yako ya kukata tama yanapoanza basi kila kitu ambacho kingeweza kutokea ili upate msaada huwa kinaanza kwenda mbali zaidi na wewe.
Hii ndio maana mtu akianza kukata tama ni kama vile mambo yanaanza kwenda mrama zaidi.Ni kama jambo moja baada ya lingine huwa linaanza kuharibika.Njia bora ya kutoka hapo ulipo sio wewe kufikia hatua ya kukata tamaa na kusema kuwa haiwezekani bali ni wewe kuendelea kutumaini.Kama utaamua kuamini kuwa utapata majibu bila kujali hali yako ya sasa,sina shaka kuwa utafanikiwa muda si mrefu kutokea sasa na utapata majibu ya changamoto zako.Kumbuka kuwa njia rahisi ya kuhalalisha kufeli kwako ni kuamini kuwa haiwezekani.
Ningependa kukumbusha kuwa changamoto yako inayokukabili leo ina majibu usikate tama.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website