Navigate / search

Waliofanikiwa Hufanya Mambo Haya 3 Kila siku

index

Tom Corley alifanya utafiti wa tabia za kila siku za matajiri 233 na pia akachunguza tabia za kila siku za watu maskini wapatao 128. Alichogundua ni kuwa kulikuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya tabia za maskini na matajiri katika namna walivyoipanga ratiba yao ya kila siku.Katika kipindi cha utafiti wake aligundua kuna karibu mambo 300 ambayo hutofautisha wanaofanikiwa na wale ambao hawafanikiwi maishani.Mara nyingi ni rahisi sana kufikiri kuwa tofauti ya waliofanikiwa na wasiofanikiwa hutokana na mambo makubwa sana yanayotutofautisha.

Mara nyingi huwa tunafikiri ni tofauti ya vipaji,ama mara nyingine huwa tunafikiri ni tofauti ya elimu ama ni tofauti ya familia tulizozaliwa.Lakini utafiti uliofanywa na wataalamu mbalimbali umeonyesha kuwa kinacholeta tofauti kati ya watu wanaofanikiwa na wale ambao hawafanikiwi hutokana na tabia zao za kila siku mara wanapoamka hadi pale wanapoenda kulala.Kwa maneno mengine,ukiweza kubadilisha tabia zako na mambo unayofanya kila siku tangu unapoamka hadi pale unapoenda kulala kuna fursa kwako kuweza kubadilisha kwa kiwango kikubwa sana kiwango cha mafanikio yako maishani.

Leo ningependa tuziangalie tabia tatu ambazo kama utaweza kuziishi kila siku unaweza ukajikuta umeongeza kiwango cha mafanikio yako si chini ya 50% katika kila eneo linalogusa maisha yako.

1)Kuwa na malengo yaliyoandikwa kila siku

Jambo la kwanza ambalo kila aliyefanikiwa huwa nalo ni kuwa na malengo ya kila siku.Mara nyingi inashauriwa kuyaandaa malengo yako usiku kabla asubuhi haijafika,lakini kama ukijikuta asubuhi imeshafika na hukuundaa usiku wake basi kiwe ni kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kufanya.

Hakikisha unaorodhesha malengo/majukumu yako yote unayotakiwa kuyafanya kwa siku hiyo.UKiweza kufanya hivi itakusaidia kuanza kutengeneza mwelekeo thabiti(focus) wa kuzingatia mambo muhimu uliyojiwekewa na hautaruhusu siku yako kuingiliwa na mambo ambayo hayapo kwenye ratiba yako ya siku hiyo.Utaalamu unaonyesha kuwa kwa kila dakika moja unayoitumia kujiandaa unaokoa dakika 10 katika utekelezaji.Leo,anza siku yako kwa kuwa na malengo mahsusi.

2)Weka Vipaumbele vyako vizuri.

Mara tu baada ya kukamilisha orodha yako ya mambo uliyokusudia kuyafanya katika siku yako;weka vipaumbele.Katika orodha yako angalia ni jambo gani lina umuhimu mkubwa sana kuliko mengine kisha hilo liweke liwe namba moja,pili angalia katika yaliyobakia na ujiulize swali kama hilohilo hadi utakapotimiza yote.Katika orodha ya malengo yako inatakiwa kuwa yamepangwa katika umuhimu wake kuanzia la kwanza hadi la mwisho.

Ukitaka kujua umuhimu wa jambo jiulize faida ya kulifanya ama madhara ya kutolifanya;hii itakuonyesha uzito wa jambo hilo na umuhimu wake kwako.

3)Anza na jambo la muhimu Zaidi.

Katika kitabu chake cha Eat that Frog,Brian Tracy anasema kuwa ubongo wa mwanadamu umeumbwa kupenda kufanya mambo marahisi yasiyo na tija na kuyaacha mambo magumu yenye tija.Watu waliofanikiwa wanaanza na mambo ambayo ni muhimu bila kujali ni magumu kiasi gani.mara baada ya kufanikiwa kumaliza mambo magumu katika siku yako;unajijengea ujasiri na hali ya kuhisi kuwa umefanikiwa sana-Hisia hizi hugeuzwa na kuwa ni nguvu ya ziada ya kukukusaidia katika kukamilisha majukumu yako yaliyobakia kwa siku hiyo.Siku itakapofikia ukingoni,pitia orodha yako uliyokuwa umejiwekea na angalia umefanikiwa kwa kiwango gani.

Kumbuka,tofauti ya mafanikio yetu katika maeneo mbalimbali huletwa na utofauti wa tabia zetu za kila siku kuliko kitu kingine chochote kile.

Usikubali kuanza siku yako leo bila kutekeleza mambo haya uliyojifunza leo.Kumbuka kuwa ndoto yako inawezekana.

Endelea kutembelea www.JoelNanauka.Com ili kujifunza Zaidi.

See You At The Top.

Comments

jacqueline mwasha
Reply

waoooooo asanteee sanaaa????????????????????

Leave a comment

name*

email* (not published)

website