Navigate / search

Vitu viwili Vinavyowafanya Watu Wafanikiwe Kwa Haraka

social-media-business-success-stories

H.L Hunt alijulikana kama mfanyabiashara amkubwa sana marekani na aliyefanikiwa katika maisha yake.Kuna wakati alishawahi kutajwa kama tajiri mkubwa wa wakati huo.Bwana Hunt alikuwa anamiliki makampuni Zaidi ya mia mbili aliyokuwa anayaendesha.

Siku moja akiwa anahojiwa na kipindi cha redio akaulizwa swali la muhimu sana:”Bwana Hunt,hebu tueleze siri ya mfanikio yako”.Akasema mafanikio yake yamejengwa katika siri mbili tu maishani mwake.Hizo ndizo ninazotaka tuziangalie leo:

Moja ni uwezo wako wa kujua kwa ufasaha unataka kufanikiwa katika jambo gani(Clarity of Purpose).Alisema kuwa hakuna mtu anayefanikiwa bila kujua kwa ufasaha anataka kufanikiwa katika jambo lipi maishani.Watu wengi hawafanikiwi kwa sababu kila wakati huwa hawajui wanatafuta nini,wanataka kuwa nani na wanataka kufanikiwa katika jambo gani.Kwa kukosa kuelewa kwa ufasaha wanachokitaka maishani mwao,basi hujikuta kila wakati wanabadilisha mambo wanayoyafanya;leo utakuta wanafanya hiki,kesho watafanya kingine ili mradi tu wana kitu cha kufanya.Ili ufanikiwe lazime ubobee kwenye kitu ulichoamua kukifanya.

Kuna watu wengi hata leo ukiwauliza,hivi lengo lako mahsusi kwenye maisha yako ni lipi?Hawatakupa jibu.Lakini kila siku utawaona wako bize.Kwa sababu ya kutokujua lengo mahsusi la maisha yao,basi hujikuta kila wakati wanaanza hatua mpya katika maisha yao.Maisha umepewa uishi mara moja tu,huna fursa ya kujaribujaribu,muda unakuacha..Amua mara moja unataka kufanya nini maishani na anza kuwekeza katika hilo kwa kujifunza,kujiunganisha na watu walioko kwenye hiyo field n.k.Bila “clarity of purpose” hakuna mafanikio maishani.

Pili alisema ni utayari wako wa kulipa gharama inayotakiwa ili kupata unachotaka.Kinachotofautisha mtu anayemiliki Toyota Grande na yule anayeendesha Range Rover ni uwezo na utayari wao wa kulipa gharama za kumiliki.Kwenye maisha ndivyo,hivyo hivyo-Tofauti ya utayari na uwezo wa kulipa gharama ili kutimiza lengo ulilonalo maishani ndio kigezo kikubwa kinachotofautisha mafanikio ya watu katika fani mbalimbali.Siku moja nilimsikia Mayweather akihojiwa na mtangazaji.Yule mtangazaji akamwambia kuwa ana bahati sana ya kushinda mapambano yake,Maywaether akamwambia “sio bahati ni kwa sababu nalipa gharama kubwa kuliko wengine,wakati wengine wamelala,mimi nafanya mazoezi”

Ili kufikia ndoto yako lazima ulipe gharama mbalimbali.Inawezekana ni gharama ya kuwa na muda wa kujisomea kitabu kila siku,inawezekana ni gharama ya kujinyima kununua vitu vya gharama kubwa ili uwekeze,inawezekana ni gharama ya kujinyima kuangalia vipinzi vya television unavyovipenda ili muda huo ufanye mambo mengine,inawezekana ni gharama ya kutumia pesa yako kuhudhuria semina/mafunzo ya kujenga uwezo wako n.k

Kiufupi ni kuwa hakuna mafanikio bila kwanza kujua unataka nini kwa ufasaha na pili kama uko tayari kulipa gharama inayotakiwa.Leo kabla siku haijaendelea sana,jiulize-Hivi nikiambiwa niandike kwa paragraph moja nataka kufanikiwa katika lipi katika maisha yangu nitaweza?Jaribu kuandika sasa.Pili,orodhesha kila jambo ambalo unatakiwa kulifanya kama njia ya kulipa gharama ya kile ambacho unakusudia kukifanikisha maishani mwako.
Endelelea kutembelea www.JoelNanauka.Com ili kujifunza Zaidi.

Ndoto Yako Inawezekana,

See You At The Top

Leave a comment

name*

email* (not published)

website