Navigate / search

Utafiti:Ukifanya mambo haya 2 Kila Siku,Utafanikiwa Kwa Haraka

Cristiano-Ronaldo

Miaka mingi huko nyuma taasisi moja ya Marekani inayoitwa Gallop iliwafanyia Usahili watu 1500 wake kwa waume waliofanikiwa ili kugundua siri ya mafanikio yao.

Kati ya maswali waliyowauliza mojawapo lilikuwa kueleza mtu mwenye akili nyingi ni mtu wa namna gani(Highly intelligent person) ? Majibu yaliyotarajiwa kutoka na tafiti zilizopita ingekuwa ni mtu aliyefaulu vizuri sana katika masomo yake ya shuleni ama mtu mwenye IQ kubwa.lakini utafiti huu ulileta uvumbuzi mpya kwani wengi wao walieleza mtu mwenye akili nyingi kwa tafsiri mbili :

1)Mtu ambaye kila siku anafanya mambo yanayochangia kumsaidia kufikia malengo yake.

Wengi wao walieleza kuwa,mafanikio yao hayakutokana na uwezo wao wa darasani ama kiwango Chao cha IQ bali uwezo wao mkubwa wa kuhakikisha kila kitu wanachofanya kinakuwa na mchango katika ndoto yao kubwa.

Swali la kujiuliza, Je kati ya mambo uliyoyapanga kufanya leo ni mangapi yanachangia katika ndoto yako kubwa?

2)Mtu ambaye anaepuka kutumia muda wake katika mambo yasiyochangia katika malengo yake.

Kuna mambo Mengi yanayotuvuta kila siku.Mengine ni kwa ajili ya kujiburudisha tu,Mengine ni kwa ajili ya kufurahisha na mengine hata yanaharibu akili yetu.

Katika utafiti huu watu waliofanikiwa walieleza kuwa kila siku huepuka kupoteza muda wao kwa mambo yasiyo na mchango katika malengo yao makubwa.

Chunguza ratiba yako ya leo na angalia mambo ambayo hayachangii katika malengo yako makubwa na jiepushe nayo.Usipoteze muda n nguvu zako katika mambo hayo.

Utafiti huu ndio ulifanya watu wengi kuelewa kwa nini si kila mtu anayefanya vizuri darasani hufanya vizuri Kwenye maisha ya kawaida pia.Na ni kama vile wengi waliofanya vizuri Sana darasani huwa wanaishia kuishi maisha ya wastani tofauti na wengi ambao walionekana kuwa wa kawaida darasani wanaishia kuishi mafanikio ya juu maishani(ingawa hii sio kwa kila mtu).

Utafiti huu ulionyesha kuwa Kanuni za kukufanya ufaninikiwe katika masomo yako ya darasani ni tofauti na zile za kufanikiwa katika masomo yako ya kawaida.

Je,Ratiba yako ya leo inachangia kiasi gani katika kukupeleka Kwenye mafanikio yako?Kama hakuna Kitu kinachochangia, tambua kuwa unajiandaa kufeli katika maisha yako.

Bila kujali kama unadegree ngapi ama Una akili kiasi gani za darasani, kama ratiba yako ya kila siku haichangii katika ndoto yako kubwa basi kufeli katika maisha litakuwa jambo la kawaida kwako. kitakachokufanikisha sio elimu uliyonayo tu bali RATIBA uliyonayo kila siku.

Tembelea Ukurasa wangu wa facebook kujifunza Zaidi.

See You At The Top

Leave a comment

name*

email* (not published)

website