Navigate / search

Usiishie Njiani:Jinsi Ya Kukamilisha Kila Unachoanzisha

Jamaica's Usain Bolt crosses the finish line to win gold in the men's 100-meter final during the athletics in the Olympic Stadium at the 2012 Summer Olympics, London, Sunday, Aug. 5, 2012. (AP Photo/Christophe Ena)
Jamaica’s Usain Bolt crosses the finish line to win gold in the men’s 100-meter final during the athletics in the Olympic Stadium at the 2012 Summer Olympics, London, Sunday, Aug. 5, 2012. (AP Photo/Christophe Ena)

Watu wengi kwenye maisha wana matatizo ya kushindwa kumaliza walichoanza,na hii hupelekea nguvu,fedha muda na rasilimali zao nyingi kupotea kila wakati.Hata katika kiwango cha Taifa,ukipita nchi nyingi hasa za afrika utakuta miradi mingi imeishia njiani,majengo mengi yameachwa bila kumalizia n.k

Kuna watu kwao imekuwa ni kama kifungo wanachoshindwa kujitoa,wakianzisha mahusiano basi yataishia njiani,wakianzisha biashara basi ikifika miezi michache wanaiacha na wanajaribu kuanza upya,wakianza kusoma kitabu huwa hawawezi kukimaliza hadi mwisho,hata wakifanya mtihani wanajikuita hawawezi kumaliza maswali yote,wakitoa ahadi ya mchango wa harusi hadi siku ya harusi unakuta wametoa nusu tu ..Kiufupi ni kuwa kwa kila walifanyalo huishia njiani,halikamiliki kwa asilimia 100.

Hali hii ikitokea mara kwa mara hujenga Imani kuwa hakuna unachoweza kufanya lakini pia hukufanya kuona kuwa ni kitu cha kawaida kwenye maisha yako.Ukiwa mtu wa kuanza bila kumaliza unakuwa hauna tofauti na timu ya mpira yenye golikipa mzuri,mabeki wazuri,viungo wazuri lakini hawana wafungaji wazuri..Watamiliki mpira vizuri lakini hawatapata ushindi kamwe.
Unapokuwa mtu wa kuachia mambo njiani yafuatayo hutokea:

1)Unakuwa umepoteza muda,nguvu na fedha zako kwenye jambo hilo.

2)Akili yako inajenga mtazamo kuwa hautaweza kufanikiwa tena katika jambo lolote.

3)Watu wengi wanaanza kutokukuchukulia serious maishani kwani wanajua hata wakikusaidia utaishia njiani.

Ningependa kukumbusha kuwa.. “Commitment is doing the thing you said you were going to do long after the mood you said it in has left you”.Kujitoa kufanya jambo ni ile hali ya kufanya ulichoahidi hata wakati ule ambapo zile hisia ulizokuwa nazo wakati unaahidi zimeondoka.Kumbuka kuwa hakuna mwanariadha anayepata medali kwa sababu alianza vizuri mbio,bali anayepata medali ni yule aliyemaliza vizuri mbio.

Mambo machache ya kukusaidia ili usiwe mtu wa kuishia njiani:
1)Kabla haujaanza kufanya chochote/au haujatoa ahadi ya kufanya jambo pata muda wa kutafakari na kujipima kama unao uwezo na nia ya kukamilisha unachokisema.Usikubali kulazimishwa kutoa ahadi ama kusema ndio ukiwa bado haujapata muda wa kutafakari.

2)Usiwe mwepesi wa kuanza kufanya jambo/kuahidi ukiwa kwenye hali ya furaha sana kwenye maisha yako,jipe muda.Usijisikie vibaya,ni kitu cha kawaida kuomba upate muda wa kutafakari kabla haujaamua.
3)Kabla haujaanza kufanya jambo Fulani jiulize “why”,sababu inayokusukuma-Je ni kwa sababu mtu Fulani alifanya akafanikiwa,au kwa sababu unataka kuprove kuwa unaweza,ama unataka kumuonyesha aliyekuacha kuwa umeshapata mwingine n.k

Hizi ni baadhi ya sababu zitakazo kufanya uishie njiani kwani hazina nguvu ya kukupeleka mbali.Kitu cha muhimu kukusukuma kufanya jambo ni kwa sababu ni kitu sahihi kwako kwa wakati huo na una moyo wa kukifanya bila kujali vikwazo.

Leo.Jikague maishani mwako.Ni mara ngapi umeanzisha jambo ukashindwa kumaliza?Je hilo ulilolianza hivi karibuni uko tayari kulikamilisha?Je,kuna jambo unataka kulianza lakini haujajitathmini kama una nia,sababu na uwezo wa kulikamilisha?

Kwenye Maisha mafanikio hayaji kwa sababu umeanzisha mambo mambo mengi bali huja kwa sababu umeweza kukamilisha mengi katika yale uliyoyaanzisha.

JITATHMINI KISHA FANYA MAAMUZI; JIFUNZE KUKAMILISHA UNAYOYAANZISHA.

Endelea kutembelea ukurasa wangu wa facebook(Joel Nanauka) kujifunza Zaidi
Ndoto Yako Inawezekana,See You At The Top.

Comments

Diana Kazinza
Reply

Ahsante sana kaka Joel kwa somo zuri.
I’ve learned a lot and am blessed too and delivered too.
This is a life lesson for me.

I also have a question.
What’s the exit strategy if you have started a journey without considering the the three advices above?

Leave a comment

name*

email* (not published)

website