Navigate / search

Unasubiri NINI Ili Uanze Kuishi Ndoto Yako?

mENTORSHIP

Mmoja utamkuta anasema bado mambo yangu hayajakaa vizuri nitaanza biashara yangu mwakani,ikifika mwakani anasema tena sasa hivi najipanga nitafanya mwezi wa sita.Mwingine anakuambia nilipanga kufanya kazi miaka 2 tu kisha nijiajiri lakini naona bado ngoja nijipange,matokeo yake amestaafu juzi.Mwingine anasema mimi lengo langu ni kufanya kazi hadi niwe na cheo cha juu kabisa lakini wakati huo nitakuwa namiliki biashara zangu na nitakuwa nafanya kilimo cha kisasa,ni mwaka wa kumi sasa hajaanza kufanya biashara yoyote ile na hata hajanunua bado hata robo heka nje ya mji,anataka kulima kwenye lami?

Hawa ndio wale watu ambao wakiona wengine wanaendelea kufanikiwa katika kile ambacho wao wameshindwa kufanikiwa kabisa huwa wanakuja na visingizio vya kila aina kuelezea kwa nini wao hawajafanikiwa na wengine wamefanikiwa.Watu wengi sana wameshindwa kufikia kilele cha mafanikio yao kwa sababu tu ya kurubuniwa na lile wazo la kusubiria hadi mazingira yawe sawa kabisa.Hata wewe leo inawezekana unazo ndoto nyingi sana ambazo ungetamani sana kuzitimiza lakini kwa kuwa tu unasubiri hadi kila kitu kiwe sawa,ni miaka mingi sasa unaendelea kulisemasema wazo lako lakini haujaanza hata kulifanyia kazi.
Jambo la kwanza na la muhimu unalotakiwa kulifahamu ni kuwa,hakuna siku yoyote katika maisha yako ambako mazingira yatakuwa yametimia kwa asilimia 100 na hakutakuwa na changamoto yoyote ile.Inawezekana kuna aina fulani ya mazingira yaje ili uanze kuiishi ndoto yako lakini ukweli ni kuwa mazingira ambayo ni kamilifu kwa kila kitu huwa hayapo katika maisha.

Hakuna siku shida zitaisha kabisa ili uweze kuanza kuweka akiba,kila siku itaionekana kama vile matumizi yanazidi,hakuna siku muda utakuwa mwingi na utapata muda wa ziada wa kusoma vitabu,kila siku utajikuta mambo yanazidi kuwa mengi.Hivyo kama kuna wazo lolote ambalo unataka kulitekeleza katika maisha yako ni lazima uamua kuanza kuchukua hatua bila kusubiri kila kitu kiwe sawasawa kabisa.Mfanyabiashara mkubwa sana nchini Marekani bwana Alan Cohen aliwahi kusema hautakiwi kusubiri mazingira yawe kamilifu kabla haujaanza,anza na kadiri unavyoendelea utajikuta mazingira yanajiweka vizuri.

Jambo la pili la muhimu sana katika maisha yako no lazima kujua kuwa kuna fursa ambazo huwa haziji amra kwa mara katika maisha yako,na zingine huwa zinakuja mara moja tu na huwa hazirudi tena.Kuna watu wengi sana ambao wamekosa fursa muhimu sana katika maisha yao kwa sababu waliamua kusubiria kila kitu kiwe sawa.Nimeshakutana na watu wengi sana ambao huwa wanajilaumu kwa sababu ya fursa ambayo waliipoteza na ingeweza kubadilisha maisha yao kabisa na wakati wako tayari kuitumia fursa hiyo basi wamejikuta hawana uwezo tena wa kuiutumia.

Hebu jiulize,hakuna fursa katika maisha yako ambayo uliwahi kuipoteza kwa kutaka kusubiria hadi kila kitu kiwe sawa na leo unaijutia?

Hata hivyo jambo la tatu na la muhimu sana ni kuwa kila unapoamua kuchukua hatua fulani katika maisha yako huwa kuna muda wa kujifunza kufanya kitu.Hii ndio maana watu wengi ambao wamefanikiwa katika kutimiza ndoto zao ni wale ambao walikuwa tayari kuanzia chini kabisa bila kujali aina ya mazingira.Ukifuatilia stori ya mfanyabiashara mkubwa sana wa kichina,Jack Ma,utagundua kuwa alianza biashara yake ndani ya eneo la bweni.Inawezekana leo usiwe na mtaji unaoutaka,inawezekana leo uanweza usiwe na ofisi unayoitaka,inawezekana leo hauna sapoti unayoitaka-Haya yote ni mazingira yasiyo kamilifu lakini ili ufanikiwe ni lazima uwe tayari kuanza kwa kidogo ulichonacho huku ukiendelea kujifunza bila kukata tamaa kabisa.

Usiwe aina ile ya watu ambao eti kwa sababu wana ndoto kubwa basi hawako tayari kabisa kuanza na kufnaya kitu kidogo katika maisha yao.

Watu ambao wamekuwa na tabia yakusubiri hadi kila kitu kiwe sawa kabla hawajaanza kufanya jambo lolote katika maisha yao wamekuwa ni watu ambao wanachelewa sana kufanikiwa na ni watu ambao wanapitwa na fursa kila zinapojitokeza.Hawa ni aina ya watu ambao huwa ni waoga wa kujihatarisha,hawako tayari kufanya kitu ambacho hakina uhakika wa asilimia mia moja,wako tayari wawe na akiba kubwa kwenye akaunti benki lakini wasiwekeze hata robi ya waliyonayo,ukiwauliza utasikia naogopa kupoteza fedha zangu ngoja kwanza uchumi ukae vizuri.

Tabia ya kusubiria hadi mazingira yote yawe sawasawa imewafelisha watu wengi sana na imesababisha wengi wakwame katika kufikia malengo ya maisha yao.Kama unataka adui huyu wa mafanikio asikukwamishe kuanza kuiishi ndoot yako basi anza mara moja leo kufanyia kazi wazo lako.Hebu jiulize,kama mtoto angesema sitaanza kutembea hadi niwe na balansi ya kutosha na nisianguke hata mara moja ingekuwaje?Kama ulishawahi kuendesha baiskeli utagundua kuwa njia bora kabisa ya kukufanya uwe derive mzuri ni kukuballi kuanza kuendesha hata kama unajua kkuwa utaanguka mara kadhaa kabla haujaweza vizuri.

Kumbuka kuwa ndoto Yako Inawezekana,

Endelea kutembelea www.JoelNanauka.Com na www.Mentorship.co.tz ili kujifunza zaidi.

See You At The Top.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website