Navigate / search

Unachagua Kuishi Kwenye COMFORT ZONE Ama SUCCESS ZONE?

Watu wengi sana wameondoka duniani wakiwa watu wa KAWAIDA sio kwa sababu hawakuwa na uwezo wa kufanya mambo MAKUBWA sana katika maisha yao bali ni kwa sababu walishindwa kuchukua hatua muhimu ili kuufanya ukuu wao UDHIHIRIKIE katika maisha yao.

Moja ya hatua mojawapo muhimu ya kuchukua ni kile alichosema mwanafalsafa mmoja kuwa “Meli inapokuwa imepaki Bandarini iko salama,lakini meli haikuumbwa ili ipaki bandarini”.

Huu ndio ukweli wa maisha-Ukweli wako haujafichwa katika wewe kupenda kukaa sehemu salama bali umefichwa katika wewe kufanya kitu ambacho umepewa uwezo wa kipekee kukifanya.

Hautaweza kupata matokeo makubwa zaidi ya uliyonayo sasa kama hautakuwa Tayari kutoka nje ya mipaka ya kile ambacho unakifanya kwa sasa.Kupenda kukaa kwenye kufanya jambo hilohilo kila wakati bila kutaka kubadilika,inaitwa kupenda kukaa Kwenye ” Comfort Zone”.

Watu wengi wameshindwa kupiga hatua kwa uoga wa kuondoka kutoka katika “Comfort zone za kwao”.Kuna Watu kitu pekee kinachowafanya wasichukue hatua muhimu Kwenye maisha yao ni kwa sababu kila wakati wanajiuliza swali-” Nisipofanikiwa itakuwaje?”

Leo nataka ujue kuwa kwa kila hatua sahihi unayoogopa kuchukua kwenye maisha yako unakosa fursa kubwa ya kubadilisha maisha yako.Hivyo swali lako linatakiwa kuwa-“Hivi  nisipochukua hii hatua nitakuwa nimekosa fursa gani”

Usikubali kuishi maisha yako ya WASTANI kwa kung’ang’ania kuishi kwenye “Comfort Yako” wakati unayo fursa ya kuchukua hatua na kuanza kuishi Kwenye “Success Zone”.

Pata Ujasiri,chukua hatua na badilisha Maisha yako.

See You At The Top

@JoelNanauka

#TIMIZAMALENGOYAKO

Leave a comment

name*

email* (not published)

website