Navigate / search

Uko Tayari Kuwa Kama Luteni Rowan ???

Mwaka 1899 mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Elbert Hubbard aliandika kipande kidogo cha Makala katika gazeti lililokuwa linajulikana kama Palestina kuhusu vita ya marekani na jeshi la Hispania nchini Cuba.Siku moja wakiwa wanakunywa chai na familia yake walianza kujadili habari ya vita hiyo na kila mtu alikuwa anamwaga sifa kwa Generali wa jeshi la cuba aliyekuwa anaitwa Calixto Garcia ambaye aliongoza vikosi vya waasi wa cuba kupata uhuru kutoka kwa wahispania.Katika majadiliano mtoto wa Hubbard aliwaambia wengine kuwa anayetakiwa kupewa sifa sio jenerali Garcia ila ni lutein Rowan wa jeshi la marekani aliyepeleka ujumbe kwa jenerali Garcia.

Ili uweze kuelewa vizuri ni kuwa mwaka 1895 kisiwa cha Cuba kilikuwa kinahangaika kupata uhuru wake kutoka kwenye utawala wa mabavu wa kihispania ambao ulikuwa unawatesa watu na kuwakandamiza.Kwa sababu ya ukaribu wa kijiogrofia na uwekezaji wa marekani nchini Cuba kila wakati ilikuwa inaendelea kuangalia kwa jicho la karibu kile kinachoendelea.Hata hivyo ilipofika mwaka 1897 hali ya Cuba ilizidi kudhorota na kulikuwa kuna maandamano yameanza katika mji wa Havana yakiongozwa na wazalendo wakipinga utawala wa jeshi la Hispania.Kutokana na hali kuendelea kuwa mbaya,Rais wa marekani wa wakati huo McKinley aliamua kutuma meli ya kivita na ikakaa karibu na bandari ya Havana ikiwa ni ishara tu kwamba wako tayari kuwatetea wacuba.Ilipofika February 15,1898 mlipuko mkubwa ulisikika bandarini ikiwa meli ya marekani imelippuliwa na jeshi la Hispania hapo ndipo marekani ilipoamua kuingia vitani na jeshi la Hispania lililokuwa linatawala Cuba.

Kabla Rais McKinley hajatangaza vita alifanya kikao na kanali Arthur Wagner aliyekuwa mkuu wa taasisi ya usalama jeshini na akamuuliza-“Nitampata wapi mtu ambaye atapelea ujumbe kwa Garcia kiongozi w akikundi cha waaasi wa Cuba ili tuone namna ya kufanya nao kazi pamoja tuungane ili tupigane vita kwa pamoja kinyume na wahispania?”ALiuliza hivi kwani alijua kuwa sio kitu rahisi kwa sababu jenerari Garcia alikuwa yuko katikati ya milima na mapori huko Cuba na hakukuwa na mawasiliano ya simu,barua pepe wala hakuna mtu alikuwa anajua yuko eneo gani haswaa na pia kuna hakuwa anaonekana mara kwa mara hata sura yake haikuwa rahisi kuitambua.Hata hivyo Kanla Wagner akamwabia Rais kuwa “Nina kijana ofisa mdogo anaitwa Luteni Summers Rowan,huyu anaweza kupeleka huu ujumbe”

Saa moja baadaye Kanali Wagner alimuita luteni Rowan akamwambia-“Hii ni barua kutoka kwa Rais wan chi,ipeleke mahali alipo jenerari Garcia huko misitu ya Cuba,panga safari yako mwenyewe hauendi na mtu yoyote yule hili ni jukumu lako”.Kisha akamshika mkono na akamuaga kwa kumsisitiza,”Hakikisha umemfikishia ujumbe huu jenerari Garcia”.Cha kushangaza ni kuwa Rowan hakumuuliza kanali Wagner swali hata moja akachukua barua na akanza kujipanga.Baada ya muda barua ilimfikia Garcia na majibu aliyarudisha kwa kanali Wagner na hatimaye Rais McKinley bila kuumuuliza alliyemtuma swali kuwa-Huyo mtu yuko wapi haswaa,sura yake inafananaje,anapenda kuvaa nguo za namna gani n.k

Il kufanikiwa katika dunia ya leo unahitaji kuwa na moyo na tabia kama ya Rowan.Ni lazima ufike sehemu katika maisha yako uamue kuchukua hatua hatarishi amabazo unaweza kwa mwanzoni ukawa hauna majibu nayo ya kujitosheleza ila ndani ya moyo wako uanona kabisa hili ndilo jambo sahihi.Ili ufikie malengo yako makubwa sana,ni lazima uamue kuwa uko tayari kuhatarisha maisha yako ili ufikie kilele cha mafanikio yako.Hebu fikiri safari ya Rowani ilikuwaje-Kupita katika misitu na kuingia nchi ya watu kwenda kuonana na waasi wan chi hiyo-Si jambo rahisi,linahitaji ujasiri wa hali ya juu sana.Wako watu wengi leo wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ni waoga mno.Ukiwapa fursa wanaogopa kupoteza,wanaogopa kupata hasara na swali lao la kwanza linakuwa hivi itakuwaje nikifeli na wala hawajiulizi hivi nitapoteza faida gani nisipotumia hii fursa.

Baada ya kupewa maagizo na kuambiwa kuwa jukumu lililokuwa mbele yake lilikuwa la kwake peke yake na hakuna mtu mwingine;Rowan hakuwa na namna nyingine ya kufanya isipokuwa kujipanga namna anavyoweza kufanikiwa katika maisha yake.Ukwlei ni kuwa mkuu wake alijua kuwa kama angetoa jukumu lile kwa mtu zaidi ya mmoja ingewezekana lisifanikiwe kabisa kwani wangeanza kujadiliana jinsi ilivyo ngumu,wangeanza wangeanza kupeana ushauri na kama ingetokea mmoja njiaani pengine amekufa basi waliobaki uoga ungewazidi.

Kasi ya mafanikio yako inaongezeka pale ambapo unajua fika kuwa hakuna mtu mwingine wa kumtegea kuhusu mafanikio yako.Hii inamaanisha kuwa kama ukifanya uzembe unajua fika kuwa hakuna mtu mwingine wa kumtegemea ili akusaidie.Watu wengi wamekwama katika kufanikisha malengo yao kwa sababu kila wakati wameweka tumaini lao juu ya mtu fulani kuwa atawasaidia kwa namna moja ama nyingine.Kama wewe ni mtu ambaye kila wakati unajihesabia haki ya kutaka kusaidia na wengine basi ujue unakwamisha mafanikio yako.Leo amua kuwa utakuwa kama Rowan,utachukua wajibu wako na utaanza safari ya kuelekea katika kutimiza malengo yako bila uoga na bila kutegemea watu wengine.

Dunia ya leo inawatafuta akina Rowan katika Nyanja mbalimbali za kilimo,biashara n.k.Watu ambao wako tayari kufanya mambo yasiyo ya kawaida ambayo kiloa mtu akiyasikia anashangaa.Watu ambao wakiweka malengo yao,hata kama yanahatarisha kiasi gani hawako tayari kuishia njiani hadi wamekanilisha na kufanikiwa.Leo chunguza maisha yako na angalia malengo uliyojiwekea,Je uko Tayari kuwa kama Rowan?Uko taayari kusafiri safari ya mafanikio ukiwa peke yako wakati kila mtu amekuacha?Uko tayari kupitia katika hatari za maisha zinazotishia lakini bado utaenedelea kufuatilia unachotaka.Mafanikio si jambo RAHISI ila LINAWEZEKANA.Ili nawe uwe mmoja wa watu wanaofanikiwa ni lazima uwe tayari kufanya mambo kwa namna ya tofauti kabisa kuanzia leo.AMUA KUWA NI LUTENI ROWAN WA MALENGO YAKO,INAWEZEKANA.

Siku zote usikubali mambo haya mawili yakukwamishe.

Kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO kimeelezea mbinu 60 ambazo watu waliofanikiwa wanazitumia kufikia kilele cha mafanikio yao.Unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba 0655 720197 na tutakuelekeza kwa wakala wetu katika mkoa uliopo ama kama uko Dar Es Salaam na unahitaji kuletewa hadi pale ulipo uanweza kuwasiliana nasi kupitia 0712 224282

Endelea kutembelea www.JoelNanauka.com/www.Mentorship.co.tz ili kujifunza zaidi.

See You At The Top.

©JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website