Navigate / search

Ukiwa na TABIA Hii Basi Utaanza kuwa MMOJA wa Watu Waliofanikiwa

nanauka

Gazeti Marufu la Forbes mwaka 2014 lilifanya mahojiano na mabilionea 50 duniani kutoka katika nchi mbalimbali kuhusu bidii yao na masaa ambayo huwa wanayatumia kila siku kufanya kazi.Kati ya kitu kilichoshangaza ni kuwa kati ya hao waliohojiwa asilimia hamsini wanafanya kazi zaidi ya masaa 60 kwa juma(Muda wa kawaida ni masaa 40 kwa juma;yaani maasaa 8 kwa siku tano za juma ukiondoa muda wa saa moja ya mapumziko).Baadhi walionyesha kufanya kazi kwa masaa mengi sana,kama vile mfanyabishara mkubwa sana,Mr.Barron ambaye alisema huwa anafanya kazi takribani kwa masaa 70 hadi 80 kwa wiki.

Hii si mara ya kwanza kwa utafiti wa namna hii kufanyika na kuleta majibu kama haya.Kiufupi hakuna mtu yeyote mwenye mafanikio ambaye utakutana naye na atakuwa mvivu.Mafanikio huja kwa utayari wako wa kufanya kazi kwa bidi bila kuchoka.Kuna watu wengi wenye vipaji na hatima kubwa lakini huwa ni wavivu wa kufuatilia ndoto zao.Wakipata hasara mara moja tu basi wanakata tamaa,wakikataliwa mara kadhaa basi wanaacha,wakiambiwa hawawezi kusaidiwa jambo fulani basi wanaachana na ndoto zao.HAPANA;Ili ufanikiwe ni lazima uwe mtu ambaye unaifuatilia ndoto yako kwa bidii na usikubali kitu chochote kikukwamishe.

Moja ya kanuni muhimu sana katika maisha yako ni ile inayoitwa 40+.Kanuni hii inasema kuwa mtu anayefanya kazi kwa masaa 40 tu kwa wiki basi huyo atafanikiwa kusukuma siku tu ili asife njaa.Lakini kama mtu anayetaka kufanikiwa kwa kiwango cha juu basi ni lazima afanye kazi zaidi ya masaa hayo tena kwa bidii katika kuifanikisha ndoto yake.

Siku moja wakati Aliko Dangote(Tajiri nambari moja Afrika) ameenda katika chuo kikuu cha LAGOS kwenda kuzungumza na wanafunzi aliulizwa kuhusu ratiba yake ya kila siku.Hii ilitokana hasa na fikra kuwa kwa sababu ni tajiri sana basi angekuwa anatumia muda wake kujipumzisha na kulala zaidi.Aliwashangaza sana watu wengi pale aliposema huwa anatumia masaa 5 tu kwa siku kulala(Maana yake anafanya kazi takribani masaa 19 kwa siku).Huyu ni tajiri namba moja Afrika,lakini bidii yake ya kazi ni ya ajabu sana.

Hii si mara ya kwanza nasikia habari za watu waliofanikiwa kuwa watu wa bidii katika kazi zao.Siku moja nilimsikia Dr.David Oyedepo alipokuja Dar es Salaam akasema huwa anafanya kazi kwa masaa 18 kila siku kwa miaka zaidi ya ishirini kwa sasa.Huyu ni mtu amejenga vyuo vikuu vitatu na ana ndege zake binafsi takribani tatu,na ni mwafrika kama na hakurithi utajiri.Inaonekana wazi kuwa kama kweli mtu anataka kufanikiwa ni lazima awe na bidii katika kile anachokifanya.

Bila kujali ndoto yako ni kufanya nini maishani mwako,bila bidii basi hautaweza kuifanikisha hata kidogo.Yeyote anayesema mafanikio ni jambo rahisi ni muongo-Ingekuwa hivyo hakuna mtu ambaye angekuwa hajafanikiwa.Ndoto yako na mipango yako lazima uiwekee bidi isiyo ya kawaida katika kuitekeleza.Kama unauza nyanya,fanya kwa bidi,kama umejiajiri usiende ofisini muda wowote unaojisikia,uwe na nidhamu kama vile umeajiriwa,uwe na bidii isiyo ya kawaida-Kinachotutofautisha sio kile tunachofanya ama fursa tunazokutana nazo bali ni bidii yetu katika kufanyia kazi ndoto zetu.
Watu wawili wanaweza kuwa na fursa sawa,mtaji unaofanana,na hata elimu inayofanana ila bidii yao itawatofautisha sana katika kuelekea mafanikio yako.

John D. Rockefeller tajiri mkubwa aliyewahi kutokea marekani alipoulizwa kuhusu mafanikio yake alisema-“Nilikuwa nafanya kazi kama mbwa kila siku ili kutimiza ndoto yangu,sikutaka kubakia katika umaskini ambao ulikuwa unaizunguka familia yangu”
Kuna mambo mawili ya kukusaidia kuhusiana na juhudi ya kuelekea katika maisha yako:

Moja,Kubali kuumia kwa muda ili baadaye uishi maisha ya kifalme.Muhamadi Ali alisema-“Nilichukia kila dakika ya mazoezi,lakini nilijiambia moyoni ,ni bora niteseke kwa sasa ili baadaye niishi kama mfalme”.Kwenye kuelekea katika ndoto zetu ni lazima tutapita katika nyakati kama hizi ambazo tutatakiwa kuruhusu kuumia kwa muda ili tutimize lengo kubwa.Inawezekana itabidi ujibane matumizi,au ufanye kazi ya kiwango kidogo kulinganisha na elimu yako,ama ufanye biashara inayoonekana inakudhalilisha,ama kutonunua vitu vya gharama kwa muda.Kwa namna yoyote ile kubali kuumia leo ili utengeneze fursa za kesho,usikubali kuishi maisha utakayoyajutia leo.Lipa gharama.

Pili ni lazima uwe mtu ambaye haupendi kulala hovyohovyo;kuna watu wanachelewa kuamka,wakipanda daladala wanalala,wakifika ofisi/kwenye shughuli zao bado wanasinzia na wako hivyo miaka yote.Kuna watu kila siku wanaweka alamu ya kuwaamsha asubuhi lakini ikianza kulia wanaizima.Kama wewe ni mtu ambaye unapenda kulala sana basi ujue umaskini utakuwa ni rafiki yako.Hata kama haujaajiriwa,hakikisha siku yako umeipangia ratiba na una shughuli maalumu sio unajifungia tu ndani unalala ama unaamka saa 3 asubuhi.Hata kama umejiajiri sio tiketi ya kuwa mvivu unalala hovyohovyo na unachelewa kuamka.

Watu wengi wanaoacha ajira na kuanza kujiajiri wanafeli kwa sababu nidhamu ambayo walikuwa nayo wakiwa wameajiriwa huwa wanaiacha.Kama unataka kufanikiwa lazima uwe mtu mwenye bidii ya kufanya kazi zako na uzifanye bila kuchoka.

Juu kumewekwa kwa ajili ya watu walio tayari kulipa gharama za ziada(The Top has been reserved for those who are ready to pay the Price).
USIKUBALI UVIVU UKWAMISHE MAFANIKIO YAKO.
Kumbuka kuwa ndoto yako inawezekana,

Endelea kutembelea www.JoelNanauka.com na www.Mentorship.co.z kujifunza zaidi.
See You At The Top.
©JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website