Navigate / search

Ufanye Nini Unapojikuta Umefanya Kosa Kubwa Maishani

Moja ya tatizo kubwa sana linawalowakabili watu ni hali ya kushindwa kujisamehe baada ya kuwa wamefanya kosa fulani kubwa kwenye maisha yao.Kuna watu ambao wamekosa kujiamini tena katika maisha yao.Kuna watu wanajutia kuwa walichezea fura yao ya kusoma na leo imewasababishia wasiwe watu ambao wana elimu nzuri,kuna watu ambao waliwahi kupendwa sana ila wakapoteza hiyo fursa na leo wameshindwa kuupata ule upendo tena,kuna watu ambao waliwahi kupata pesa nyingi sana na wakazitumia vibaya na leo wako kwenye madeni ama wanaishi maisha magumu n.k
Kwenye maisha angalau kila mtu kuna siku aliwahi kufanya maamuzi fulani ama akachukua hatua fulani ambayo ilimletea majuto ya muda mrefu.Wakati wengine huwa wanaweza kujisamehe na kusonga mbele kuna wengine hali hii huwatesa maisha yao yote na huwasababisha kutokuishi maisha ya furaha na wanakosa hamasa ya kuendelea mbele kabisa.Ila sawli kubwa ni kwa nini wengine wakifanya makosa wanaweza kusonga mbele na wengine hawawezi kabisa?
Moja ni kwa sababu kuna watu wanaamini kwa sababu walifanya kosa fulani basi hawana fursa nyingine kabisa.Huu ni uongo wa akili ambao umewarudisha sana watu wengi nyuma na kuwafanya washindwe kabisa kusogea hatua moja mbili.Kuna watu wanaamini kwa sababu ya kukosea kwao kulikopita basi hakuna namna wanaweza kufanikiwa tena katika maisha yao,sio kweli.Unaporuhusu hali hii inakuletea kujihukumu kwa ndani “Inner self-condemnation” ambayo inakufanya ukose kujiamini na unajiona kila wakati kuwa wewe ni mtu usiyefaa kabisa
Usiruhusu hata simu moja kosa lako moja la jana iue ndoto yako kubwa ya kesho.Kila unayemuona amefika juu sana Katina maisha yake kuna siku aliwahi kufanya kosa fulani katika maamuzi ama hatua fulani lakini alipoamua kurekebisha basi alifanikiwa kuinuka na kusonga mbele.
Mbili ni kwa sababu kuna watu ambao kila wakati huwa wanawaambia hawataweza kuinuka tena.Kuna watu ambao wamefanikiwa kabisa kujisamehe lakini wamezungukwa na watu ama mtu ambaye kila wakati huwa anawakumbusha makosa yao na mara nyingine anayatumia kuwanyang;anya ujasiri walio nao katika kufanya mambo fulani.
Kuna watu ni mahodari sana katika hili,tena kuna wengine ambao wanaweza kukuambia kuwa wamekusamehe kosa lako fulani lakini kila wakati likitokea jambo huwa wanakukumbusha kosa ambalo wanasema walishakusamehe.Hii imewasabishia watu wengi sana kukosa tena ujasiir kuhusu kusonga kwao mbele.Mara nyingi watu wa namna hii huwa ni watu walio karibu sana na sisi na ni watu ambao tulitegemea watusaidia katika kujenga upya ujasiri wetu baada ya makosa yetu.
Kuna njia mbili unaweza kufanya kuhusiana na watu wa namna hii.Moja ni kujaribu kukaa mbali nao.Watu wa namna hi inabidi ufanye juhudi za makusudi ili kutengeneza umbali nao.Lakini kama ni jambo ambalo haliwezekani kuwa mbali nao uanwchoweza kufanya ni kukabilina nao.Hata siku moja usiruhusu mtu aendelea kutumia kosa lako lililopita kukuvunja kujiamini kwako-Awe rafiki yako,bosi wako n.k ikitokea kila wakati anakukumbusha kosa lako kwa nia ya kukufanya ujisikie hauwezi ama mnyonge,mwambie-“Hilo limeshapita na nakubali nimekosea kwa sasa natazama mbele kufanya mambo vizuri zaidi”
Kiufupi ni kuwa,wakikukumbusha makosa yako ya jana wewe wakumbushe ndoto yako kubwa ya kesho.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website