Navigate / search

Tyler Perry:Historia Ya Maisha Yangu Itakusaidia Kuwa Bilionea Kama mimi

1000509261001_2101689729001_Tyler-Perry-Transition-into-Film

Mwaka 2011 katika gazeti la Forbes lilimtaja Tyler Perry kama mtu anayelipwa pesa nyingi zaidi katika sekta ya usanii na uigizaji.Mwaka 2013 alitoa kiasi cha shilingi dola milioni 1 ili kusaidia ujenzi wa kituo cha vijana kwa Bishop T.D Jakes,Hii ni kuthibitisha kuwa bila ya shaka yoyote ni mtu ambaye amefanikiwa sana.Wakati kila mtu alimsifia na kutaka kuwa kama yeye,Perry alizungumzia historia yake iliyomtoa kila mtu machozi.

Katika utoto wake Tyler Perry alinyanyaswa sana kijinsia na watu waliomlea,akiwa shule ya sekondari alifukuzwa kwa matatizo ya ada na hii ilimpelekea apoteze mwelekeo wa maisha yake kabisa.Katika historia ya maisha yake Perry ameshawahi kujaribu kujiua mara mbili na mara ya mwisho alifanya hivyo alipokuwa akiwa na miaka 22.Baada ya kunusurika kufa,Perry aliamua kuhamia Atlanta ambako alianza kufanya kazi za hali ya chini na kuanza shughuli za uigizaji.Ilipofika mwaka 1992 aliandika na kuanza kuiishi ndoto yake kwa kutengeneza igizo la kwanza “I know I have been changed”.

Ili kufanikisha uzinduzi wake alikuwa akiweka akiba kwa muda mrefu sana ,cha ajabu siku ya uzinduzi walikua watu 30 tu na aliweza kufanya show weekend moja tu na baada ya hapo show haikupata wateja.Hata hivyo Perry alikuja kufanikiwa tena baada ya miaka 6 kwa kuwa aliendelea kujaribu kila wakati.
Maisha ya Perry yanatuambia kuwa kila mmoja wetu anaweza kuwa anayo historia mbaya na ya kukatisha tamaa katika maisha yake.Historia ambayo tukiitafakari sio tu inatukatisha tamaa bali pia inatufanya tuone uhalali wa kushindwa kwetu na kutokuchukua hatua katika maisha yetu.Hata hivyo pamoja na kunyanyaswa kijinsia na kushindwa kuendelea na shule Perry hakukubali kukata tamaa kuiishi ndoto yake.

Kilichonishangaza zaidi katika maisha ya Perry ni kuwa baada ya kuwa ametunza pesa zake kwa shida sana kwa miaka mingi,alikuja kufeli vibaya sana alipojaribu tena kuiishi ndoto yake.Hebu fikiria,mtu amefanya kazi ngumu za kuosha vyombo,kufagia barabara n.k kisha anatunza pesa kwa miaka kadhaa halafu siku anayowekeza pesa yake ili aiishi ndoto yake ya miaka mingi anajikuta amefeli vibaya sana katika maisha yake.Hapa kuna funzo kubwa sana;katika maisha tunaweza kuwa na fursa ambayo tumejiandaa na tukawa na uhakika sana kwamba kwa wakati huo tukifanya tutafanikiwa bila shaka,lakini mambo yasiende tulivyofikiri.

Hivi haujawahi kuapply kazi na ukafanya interview ukawa na asilimia 100 utapata?Au haujawahi kuahidiwa pesa na mtu unayemwamini lakini ikatokea hajakupatia?Au hujawahi kufauatilia dili fulani la pesa hadi linakukosesha usingizi kwani unakuwa umeshaanza kupanga hadi na matumizi kabla pesa haujapata halafu mwisho wa siku unakuja kuikosa pesa yote?
Fikria,Yaani mtu ambaye leo anapata mabilioni kwa kuigiza,kuna siku aliandaa show wakaja watu 30 tu?Hii ndio kama vile unaamini unaweza kucheza mpira ukienda kwenye majaribio unaambiwa umeshindwa,unaamini wewe ni mwimbaji mzuri ukitoa albam hata kopi mia moja hauuzi,unaamini wewe una ndoto za biashara lakini ulipojaribu ulifeli ukapoteza hadi mtaji,unaamini una ndoto ya kilimo lakini kilimo chako cha kwanza ulipata loss kubwa-Kumbuka Ndoto uliyonayo lazima itajaribiwa.

Katika mazingira kama haya,umkumbuke mtu kama Tyler Perry ambaye baada ya kupoteza kila alichonacho na kuanza kuishi maisha yasiyo na mwelekeo tena hakuiacha ndoto yake ife,aliendelea kuifuatilia na leo hii amefanikiwa sana.
Katika kuianza kuishi ndoto yako kuanza wakati utalazimishwa na mazingira akurudi nyuma kidogo kujipanga upya,kuna wakati utalazimishwa kupanga mikakati mipya baada ya ile ya zamani kufeli kabisa-Kitu kikubwa,usikubali kabisa kukata tamaa kuifuatilia ndoto yako bila kujali ni mara ngapi ndoto hiyo imefeli katika maisha yako.

Ghafla nimemkumbuka rafiki yangu ambaye miaka michache iliyopita aliamua kuchukua mkopo wa milioni 60 akiamini wakati wake wa kufanikiwa katika biashara umefika na dalili zote zilionyesha hivyo.Kufumba na kufumbua alitapeliwa pesa yote na akaanza maisha mapya kwa kuomba kuhifadhiwa katika nyumba ambayo hata madirisha hayajawekwa nje kabisa ya jiji la Dar es Salaam na ofisi yake ilikuwa posta,lakini leo ninavyozungumza amefanikiwa sana baada ya kuamini tena kuwa anaweza kuinuka na kuiishi ndoto yake upya.Nawe pia usikubali kuanguka kwa mara moja kukuzuie kutimiza ndoto yako ya Maisha.
Kumbuka ndoto Yako Inawezekana,

Endelea Kutembelea www.JoelNanauka .Kujifunza zaidi.

See You At The Top.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website