Navigate / search

TUZO KUTOKA TAASISI YA WOF (WOMEN OF FAITH) YA KUTAMBUA MCHANGO WA JOEL NANAUKA KATIKA KUBADILISHA JAMII

j3

Tarehe 2 mwezi wa 9, Taasisi ya WOF(Women of Faith) ilimtunikiwa tuzo maalumu Joel Nanauka ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi na kujitoa kwake katika kuleta mabadiliko katika jamii na njia ya kumtia moyo ili aweze kuendeleza mikakati ya kuleta matokeo chanya. 

Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Havanah Hotel Mikocheni,ilihudhuriwa na wanachama wa WOF wakiambatana na wenzi wao ambako pia walijumuika kwa pamoja kwenye chakula cha pamoja.Pamoja na mambo mengine uongozi wa WOF ulitoa pole kwa changamoto mbalimbali ambazo Joel amezipitia katika harakati za kuleta mabadiliko na pia kumtia moyo kuendelea na juhudi zake.

Tumetiwa Moyo sana na jinsi ambavyo haujawahi kurudi nyuma katika kujitolea kuleta mabadiliko kwa jamii ya kitanzania,na sisi tunalo tumaini kuwa ndoto kubwa uliyonayo kuna siku itafanikiwa.Tunakupa tuzo hii ikiwa ni ishara ya kusema hongera kwa juhudi zako na usonge mbele bila kukata tamaa-See You At The Top” Ilikuwa ni sehemu ya hotuba ambayo ilisomwa na mwenyekiti wa WOF kwa niaba ya taasisi.

Joel aliwashukuru kwa kupata tuzo hiyo na pia alielezea kuwa anaitoa kwa mke wake kwa jinsi ambavyo amekuwa mtu wa kipekee katika kumsaidia kutimiza ndoto na kupiga hatua kila wakati.

Ninamshukuru Mungu sana kwa taasisi ya WOF(Women Of Faith) kunipatia tuzo ya kunitia moyo na kutambua mchango wangu katika kuitumikia jamii.Nimeidedicate tuzo hii kwa mke wangu kipenzi Rachel,kwa kujitoa kwake kunisaidia kuyatimiza yote yanayoonekana kwa nje.Mara nyingi ni rahisi kuonekana ni hodari kwa nje bila kujua kuna nguvu iliyojificha.Kila wakati nilipotaka kuishia njiani aliniambia-“Unaweza,endelea niko nawe“. 

Since I met her,she has brought balance and stability in my life.She knows her role and she has brought the best out of me.You better Miss Everything but never miss a support and Love From your Wife.I Love You Rachel Wangu-You are the Invisible Lady Behind All of My ExploitsSehemu ya maneno ya shukrani ya Joel. Joel ameichukulia tuzo hii kama sehemu ya chachu ya kuendelea kutumikia watu kwa namna mbalimbali katika jamii ya kitanzania. Zifuatazo ni baadhi ya Picha Katika tukio hilo

Leave a comment

name*

email* (not published)

website