Navigate / search

TULIPOTEZA BILIONI 340/- KWENYE URANIUM;HIZI ZA GESI TUSIPOTEZE TENA.

images

Mwaka 2011 baada ya ripoti ya kwanza ya TEITI(Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative) ya mlinganisho wa fedha zilizopokelewa na Serikali kutoka katika sekta za madini,mafuta na gesi na zile ambazo zimeonekana kwenye mahesabu ya serikali iligundulika kuwa kuna kiasi cha shilingi bilioni 24 ambazo serikali ilishindwa kutoa maelezo yenye uthibitisho zimeenda wapi.
Hata hivyo kilichoshangaza Zaidi ni kuona kuwa katika mapato yanayopatikana kutoka katika sekta hizi ni kuwa 60% inatokana na michango ya wafanyakazi wa sekta ya madini.Hii ilishtua na kushangaza kwani inamaanisha kuwa wafanyakazi katika makampuni ya madini ndio wanachangia kiwango kikubwa cha pesa kuliko migodi yenyewe.

Katika kukabiliana na matatizo ya upotevu wa mapato katika sekta ya madini,gesi na mabadiliko mbalimbali hasa yanayohusu kodi yamefanyika ili kuepusha hasara iliyokadiriwa kufikia trillioni 1 ya misamaha ya kodi isiyo na manufaa inayotolewa.

Baada ya bunge kupitisha ongezeko la asilimia moja ya kodi ya Mrahaba kutoka 3%-4% majadiliano yaliyotokana na hoja binafsi ya aliyekuwa Mbunge wa Kaskazini,Zitto Kabwe macho ya wengi yalifunguka kuifuatilia kinachoendelea katika sekta hii.

Sheria mpya ya Kodi ya mwaka 2012 ilitoa pia nguvu ya serikali kupata kipato pale makampuni yanapouza hisa zake(Capital gain Tax). Wakati mauziano ya Zain kwa Airtell,Taifa lilikosa kiasi cha US$ 312 millions kwa kukosa kuwa na sheria thabiti.

Kilichoshtua Zaidi ni pale serikali ilipokosa kupata bilioni 340 kutokana na mauziano ya kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa Uranium ya Mantra Resources ya Australia na ile ya Urusi Atomredmetzoloto ARMZ.Ukweli ni kwamba sheria ziko wazi kabisa kuwa kabla mauziano yoyote hayajafanyika basi ni lazima kodi ilipwe kwanza;wote waliohusika na kuruhusu mauziano haya bila kufuata utaratibu wanatakiwa wachukuliwe hatua.Cha kushangaza kesi hii ilivyoenda mahakamani TRA ilishindwa na imekata rufaa isiyo na matumaini ya ushindi wowote.

Dhamira ya Kampuni ya Shell iliyotangazwa hivi karibuni kuinunua Kampuni ya BG yenye vitalu vya gesi hapa Tanzania kwa thamani ya kwa dola za kimarekani bilioni 70 inamaanisha mauzo yakikamilika,Tanzania itatakiwa kupata kodi takribani dola milioni 600 kutokana na sheria ya Kodi ya mwaka 2012.Kifungu cha 90 (1) cha sheria ya kodi ya kipato kinachotokana na wanaouza hisa{wasio wakazi(non-resident) watozwe 20% ya pato walilopata na wale ambao ni wakazi(resident) watozwe 10% ya kipato walichoingiza}
Utaratibu ni kwamba mahitimisho ya mauzo hayatakiwi kufanya kabla ya kodi hii haijalipwa.

Kwa uzembe tulishindwa kukusanya bilioni 340 toka kwenye mauzo ya mgodi wa Uranium ulionunuliwa na Mantra Resources toka kwa Atomredmetzoloto (ARMZ) ya Russia.Wakati huu tusilale.
Jambo linatakiwa liwe wazi,vyombo vya habari na wanaharakati waendelee kupaza sauti ili kutoruhusu mwanya wa kupata hasara yoyote kwa mara nyingine.

TUZILINDE RASILIMALI ZETU,
TUHIMIZE UWAJIBIKAJI

Joel Arthur Nanauka

Comments

Dr. Frateline Kashaga
Reply

Hongera sana Joel , nimependa web site yako, nitaipitia weekend.

Kuhusu Gesi nakubaliana na wewe hivyo tupo pamoja.

Regards
Dr. Kashaga

nanauka
Reply

Ahsante Dr;UFAHAMU ndio nguvu kubwa inayohitajika ili kuleta mabadiliko.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website