Navigate / search

Thom Packets:Hii Ndio Sauti Ya Mafanikio Unayotakiwa Kuisikiliza

homeless-in-car-634x330

Thom Packets alifanikiwa kuwa tajiri sana akiwa bado hajafikisha miaka 50,alikuwa na mali nyingi na alijulikana sehemu mbalimbali kama mfanyabishara mkubwa sana wa kizazi chake.Bahati mbaya sana alipofika takribani miaka 55 ilitokea bahati mbaya mtu mmoja alikutwa amekufa ofisini kwake na akafunguliwa kesi.Kesi ile ilikuwa mbaya sana na Thom alkitakiwa kulipa pesa nyingi sana zaidi ya dola laki saba na hamsini na gharama kadhaa.

Na katika kipindi hichohicho ndoa yake iliingia matatani na akajikuta imevunjijka na biashara yake kufilisika kabisa.Hapo ndipo ilikuwa kama vile Thom anaanza maisha mapya.Katika maelezo yake Thom anasema alijikuta akianza kuishi kwa kulala ndani ya gari lake katika mitaa ya George Avenue jijini Washington Marekani.Leo hii maisha yake yamebadilika na amefanikiwa kuliko ambavyo alifanikiwa kabla hajapoteza mali zake za kwanza.

Siku moja baada ya kuona maisha yamekuwa magumu kabisa aliamua kuchukua vidonge 35 vya usingizi akivinywa akijua kabisa kwa idadi hiyo basi hataweza kuamka tena na atakufa akiwa usingizini.Cha kushangaza baada ya siku mbili Thom alijikuta ameamka na yuko hospitalini anatibiwa.Wakati alipopona alieleza kuwa akiwa katika hali ya kupoteza fahamu kabisa alisikia sauti ikimwambia mambo kadhaa ndani yake.

Moja ilimwambia kuwa kuna tumaini tena hata kama amepitia magumu kiasi gani.Kwenye maisha kuna nyakati za giza nene sana,nyakati ambazo zile zinazoitwa bonde la uvuli wa wa mauti.Hizi ni nyakati ambazo shauku ya kuondoka duniani huwa ni kubwa kuliko kuendelea kubakia kuishi.Huu ni wakati ambao kila unachojaribu kufanya huwa kinaonekana kinafeli,ni wakati uanpoteza furaha yako ya ndani,kila unayemtarajia akusaidie huwa haonekani kabisa.Huu huwa ni wakati wa upweke na huzuni kwani ni kama vile kila ndoto yako uliyokuwa unaiamini kwa nguvu na kwa bidii sana ni kama vile haifanikiwi tena,ni wakati unaojiuliza “Hivi mimi nitaweza kufanikiwa kweli?”.Lakini ukitulia vizuri sauti iliyosikika ndani ya moyo wa Thom inaweza kusikika kwako pia-Kuna tumaini tena.Hakuna magumu yasiyo na suluhisho,hakuna matatizo yanayoweza kudumu milele,Kwa hali yoyote ile unayopitia leo-Jua kuna tumaini tena.

Mbili ni kuwa sauti ile ilimwambia kama unataka kupata zaidi ni lazima ufanye kitu zaidi ya ulichofanya hapo kabla.Ni hekima ya kawaida kujua kuwa kama unafanya mambo yaleyale kila siku bila kubadilisha,huwezi kupata matokeo tofauti na yale unayopata sasa.Kama mwaka jana ulisoma kitabu kimoja kwa mwaka na mwaka huu ni hivyohivyo ujue matokeo yako ya mwaka jana na mwaka huu yatafanana kabisa.Baada ya kuamka kutoka usingizini Thom aliamua kuanza kufanya shughuli zake kwa bidii kuliko ilivyokuwa hapo awali.Aliamua kuongeza maarifa kwa kujisomea zaidi ya ilivyokuwa hapo awali,kiufupi aliamua kufanya mara mbili ya kila alichokuwa anafanya hapo kabla-Matokeo yake?Alipata mafanikio mara mbili zaidi ya yale ya kwanza.Njia rahisi ya kubadilisha maisha yako ya sasa ni kuanza kufanya vitu ambavyo haujawahi kuvifanya hapo kabla.

Bila kujali uliwahi kupoteza nini huko nyuma,bila kujali hali inayokuzunguka ni ya kukatisha tamaa kiasi gani.Bado unao uwezo wa kufikia mafanikio zaidi yale ambayo ulishawahi kufanikiwa wakati wowote huko nyuma.

Leo amua kuwa unataka kuisikiliza sauti gani katika maisha yako-Je,Unataka kuisikiliza sauti inayokuambia kwamba hauwezi na utashindwa?Je unapenda kuisikiliza sauti ambayo inasema utaweza na utafanikiwa?Chaguo ni lako,hata hivyo nakushauri uwe kama Thom-Chagua kuisikilza sauti inayokuambia bado unayo fursa ya kufanikiwa katika maisha yako.
Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Endelea kutemebelea www.JoelNanauka.Com kujifunza zaidi.

Ndoto Yako Inawezekana.

See You At The Top.

Comments

Anthony Twipa
Reply

Nimejifunza kitu ndania ya simulizi hii kilichobaki ni kuaply natoka maisha yangu

Daniel isaya
Reply

I real like your speech during lastnight at dpc

joram mwangosi
Reply

niceeee…inspiration
sorry huwa unafanyia wapi inspiration speaking ?

Pastor_Joel16
Reply

Kila jumamosi ya mwisho wa mwezi huwa tunakutana pale GEPF Towers Victoria Ghorofa ya 4.Mwezi huu wa saba ni tarehe 30.Karibu sana

Leave a comment

name*

email* (not published)

website