Navigate / search

Siri Ya Mafanikio Toka Kwa Rubani Mwenye Miaka 20

Kalenga

Kuna watu wengi sana ambao huwa wanafikiri kuwa mafanikio yao yatatokea wakishafikisha umri fulani.Hawa ndio wale aina ya watu ambao kila siku ukikutana nao wanakupa stori za kuwa kuna mipango mikubwa sana ambayo wanaipanga kuifanya kesho wakishakuwa wakubwa zaidi.

Mwaka jana kijana wa Zambia Kalenga Kamwendo alifanikiwa kuwa rubani(first officer) mwenye umri mdogo kabisa nchini humo akiwa na umri wa miaka 20.Hata hivyo mwaka huu amefikia mafanikio mengine ya kuwa ameshaweza kuruka kwa masaa 1000 aliporuka kutoka Lusaka kwenda Mfuwe.Hii inamaanisha amebakiza masaa 500 tu kumwezesha kufanikiwa kufanya mitihani ya kuwa rubani wa cheo cha juu zaidi cha “senior officer”.
Kamwendo ametoa changamoto kwa vijana wa afrika wenye malengo mbalimbali kuhusiana na ndoto zao za mafanikio.Kawaida ni kuwa kama tunataka kufanikiwa ni lazima tujifunze kwa watu kama akina kamwendo ili na sisi tuweze kufika juu pia.

Alipoulizwa kuhusu siri ya mafanikio yake alijibu kwa kifupi-“Hardword and determination”-Ni kujitoa na kufanya kwa bidii zote.Huo ndio ukweli kama tunataka kufikia malengo yetu kwa kasi na kwa kiwango cha juu sana ni vizuri kutambua kuwa tunahitaji kuweka nguvu kubwa katika ndoto tulizonazo.
Kamwendo anatufundisha kuwa muda ni jambo muhimu sana inapofikia suala la mafanikio,hii ndio maana masaa yanaleta tofauti katika mafanikio yake.Hapa najiuliza hivi umeshatumia masaa yako 1000 kufanya nini?Kuna wengine ukijumlisha masaa unayotumia kuangalia movies,kupita kwenye facebook,kuchart kwenye watsapp na kuvizia ofa za simu ili uwapigie watu bila mpangilio maalumu utakuta una masaa zaidi ya 1000 na hakuna mabadiliko katika maisha yako.Kama kweli unataka kufanikiwa kwa kiwango cha juu ni lazima uwe ni mtu ambaye unajali muda wako.Kila wakati Jiulize-Hivi huwa natumia muda wangu vizuri?

Jambo lingine kubwa kutoka kwa kamwendo ni kuwa,unayo nafasi ya kufanikiwa kwa spidi unayoitaka.Siku hizi katika jiji la Dar es salaam kuna mabasi ya mwendokasi na yale ya kawaida,uchaguzi ni wako.Ndivyo ilivyo kwenye maisha unaweza kuamua kufanya mambo ya kuharakisha mafanikio yako ambayo ni sawa na kupanda mabasi ya mwendokasi ama ukaamua kufanya mambo kwa kawaida ambayo ni sawa na kupanda daladala za kawaida.Kamwendo anatufundisha kuwa njia ya kuongeza kasi ya mafanikio yetu ni kujitoa kwa asilimia mia kwa nguvu na muda wetu kufanya yale mambo ambayo yanachangia ndoto zetu,kamwendo anashinda hewani akirusha ndege wakati vijana wengine wako disco,wanaangalia mpira,wanachat n.k.Kama unataka kufanikiwa kwa kasi ya kamwendo basi jitahidi kufanya mambo ya mwendo kasi.

Mwisho kabisa kamwendo anatuonyesha kuwa lolote ambalo linaloonekana haliwezekani kwa sasa linawezekana kama tutaamua kulifanya kwa dhati.Katika umri mdogo aliokuwa nao hakuna mtu alitegemea kama anaweza kufikia mafanikio aliyonayo kwa sasa.Ndivyo ilivyo kwako inawezekana ukiangalia umri wako,pengine ni mdogo sana ama umeshaenda sana kiwango ambacho huwa unadhani kuna mambo huwezi kufanikiwa maishani mwako.Si kweli-Kila mtu ana fursa ya kufanikiwa katika maisha yake katika umri wowote aliopo.

Usikubali kujidharau kutokana na umri wako,usikubali kudharauliwa kwa sababu ya umri wako,usikubali kuwa na ndoto ndogo kwa sababu ya umri wako-Unao uwezo wa kufanikiwa kwa kiwango cha juu katika umri wowote ule ulio nao.Ndoto uliyonayo usiiogope hata kama ni kubwa kwa kiasi gani-Anza kuiishi na utashangaa jinsi unavyoifanikisha bila kuchelewa kabisa.
Natamani siku moja nikutanae na wewe ukiwa umeshafikia katika kilele cha ndoto yako.

Kumbuka kuwa Ndoto Yako Inawezekana.
Endelea Kutembelea www.JoelNanauka.Com Kujifunza zaidi.

See You At The Top.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website