Navigate / search

Siri Ya Kutimiza Ndoto Yako Toka Kwa Arnold Swarzenegger

arnie-edit-xlarge

Mwaka 1976 Arnold Schwarzenegger hakuwa mtu Maarufu kama alivyo sasa.Siku moja mwandishi wa habari wa gazeti la Tucson Citizen anayeandika habari za michezo,Steve Chandler alipata nafasi ya kukutana na kufanya mahojiano na Arnold katika hotel ya Double Tree Inn Tucson iliyoko Arizona.Steve anasema siku hiyo hakuna mtu alikuwa anamtambua Arnold pale kwenye mgahawa walipokutana kwani hakuwa maarufu kabisa.
Arnold alikuwa katika mji wa Arizona akiitangaza movie mpya ya Stay Hungry,hii ni baada ya kufanya vibaya sana katika movie zilizotangulia za Jeff Bridges na Sally Field.

Kati ya Maswali ambayo Steve alimuuliza Arnold ni”Sasa kwa kuwa umestaafu kuwa mtunisha misuli,unapanga kufanya nini tena?”Akiwa mtulivu Arnold alijibu-“Nitakuja kuwa mwigizaji maarufu nambari moja wa Hollywood”

Kwa kuzingatia jinsi movie zake zilizopita ambavyo hazikufanya vizuri kabisa,Steve alishikwa na kicheko kwa maneno ya Arnold yaliyoonekana hayawezi kutimia kabisa na kama alikuwa anajifariji.Alipomsikiliza lafudhi yake ya kiaustralia na umbo lake lisilovutia,ilikuwa ni wazi kabisa kuwa hawezi kufanikiwa Hollywood.Lakini akijaribu tu kumtia moyo akamuuliza.atafanyaje kutimiza ndoto hiyo?Arnold Akamjibu-“Mchakato ni uleule,unatengeneza maono unayotaka,na unaishi na picha ya kule unakotaka kufika kama vile umeshafika” {“What you do is create a vision of who you want to be, and then live into that picture as if it were already true.”}

Hivi ndivyo maisha yalivyo.Mara nyingi tunapoeleza ndoto zetu kwa watu wanaotuzunguka wanaweza kuona kama vile ni jambo lisilowezekana.Wanaangalia uwezo wetu wa elimu,wanaangalia historia zetu kisha wanasema,hakuna namna utafanikiwa.

Miaka michache baada ya mahojiano ya Arnold na Steve,maisha ya Arnold yalibadilika na alifanikiwa kufikia lengo lake la kuwa mcheza sinema maarufu wa Hollywood kama alivyomwambia Steve hapo awali.

Mbinu moja kubwa unayohitaji kuitumia kila siku maishani mwako ili uweze kutimiza ndoto yako ni kuhakikisha kuwa picha ya kule unakokwenda au vile unavyotaka kuwa iko ndani yako kila wakati.Ukweli ni kuwa yale yanayotokea nje yetu ni matokeo ya yale yaliyo ndani ya mioyo na akili zetu.James Allen katika Kitabu chake cha “As the Man Thinketh” anasema wewe ni matokeo ya mawazo yanayozunguka akilini mwako kila wakati(You are the product of your dominant thoughts).Usiruhusu Mawazo ya kushindwa ama kutofanikiwa yawe sehemu ya maisha yako.Jaza akili yako na mawazo ya maisha mazuri unayotaka kuishi,mafanikio unayotaka kuwa nayo n.k.

Usiruhusu kutumia muda wako kuwaza kushindwa,kutofanikiwa ama kuona haiwezekani.
Usiogope kusema kwa ujasiri unataka kuwa nani ama unataka kufanikiwa kwa kiwango gani.Siku moja nawe utatimiza lengo lako kama Arnold Schwarzenegger kama hautakata tamaa maishani mwako.

Kumbuka,Ndoto Yako Inawezekana.Endelea kutembelea

www.JoelNanauka.Com ili kujifunza Zaidi.

See You At The Top.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website