Navigate / search

SIMU MOJA YA RAIS GOODLUCK JONATHAN ILIVYOIEPUSHA NIGERIA ISIMWAGE DAMU BAADA YA UCHAGUZI…..!!!

Buhari receives call

Tangu uchaguzi wa Nigeria ulipoanza ilionekana wazi kuwa mpambano mkali utakuwa kati ya Muungano wa vyama wa APC(All Progressive Congress) ulioundwa na February 2013 ukiunganisha vyama vikubwa vitatu vya upinzani vya Action Congress of Nigeria(CAN) the Congress for Progressive Change (CPC) na All Nigeria Peoples Party (ANPP) uliokuwa unaongozwa na Mgombea wake Mahammudu Buhari na chama tawala cha PDP kilichokuwa kinaongozwa na mgombea wake Goodluck Jonathan.

Katika historia ya chaguzi zilizopita nchini Nigeria wapinzani waliokuwa wakishindwa kila wakati walikataa kuyatambua matokeo kwa tuhuma za wizi na hivyo kusababisha vurugu na vifo kwa wafuasi wao.Swali kubwa lilikuwa je,Rais Goodluck Jonathan atasema nini baada ya kushindwa?Ni ukweli kuwa matamko yake baada ya matokeo ya uchaguzi yalikuwa ni jambo kubwa linaloweaz kuleta amani ama kuitumbukiza Nigeria katika vita kubwa.

Wakati matokeo yanaendelea kutangazwa katika kituo maalumu kilichowekwa na tume huru ya uchaguzi ya Nigeria(INEC) mwaklishi wa chama tawala cha PDP cha Rais Goodluck Jonatha,Bwana Godsday Orubebe alichukua kipaza sauti na kutangaza kuwa haridhiki na mwenendo wa matokeo na kutoa ishara kuwa chama cha PDP kinaweza kuyakataa matokeo hayo.

Hata hivyo bila kutaraiwa na wengi habari zilielezwa kuwa Rais Goodluck Jonathan baada ya kuona mwelekeo wa matokeo na kujua kuwa hamna namna yay eye kuibuka na ushindi wowote aliamua kufanya juhudi ya kumpigia simu Mpinzani wake Bwana Buhari ili kumpongeza na kukubali kushindwa.

Juhudi ya kufanya hivyo ilithibitishwa na watu wa karibu wa Bwana Buhari waliompa taarifa mwandishi wa BBC bwana Mansur Liman kuwa Rais Jonathani alifanya juhudi ya kumpigia Bwana Buhari na wasaidizi wake mara kadhaa bila maafanikio,kwani simu zao zilikuwa bize sana.

Baada ya kuona kuwa simu yake haipokelewi Rais Jonathan aliamua kumtuma mjumbe kwenda kumwambia Bwana Buhari apokee simu yake;hapo ndipo Bwana Buhari alipoweza kupokea simu ya Bwana Jonathan mnamo majira ya saa kumi na moja ana robo siku ya tarehe 31 mwezi wa tatu.

Wakati Rais Jonathan anapiga simu hiyo wajumbe wa Kamati ya amani ya Taifa inayoongozwa na Rais wa zamani Abdulsalami Abubakar walikuwa wamemtembelea.Jambo la muhimu katika uamuzi wake ni kuwa Rais Jonathan hakuwasiliana kabisa na washauri wake ama wasaidizi wake kabla ya kufanya uamuzi wa kupiga simu hiyo.Inasemekana kuwa kama angeamua kuomba ushauri kwa wasaidizi wake hakuna ambaye angekubali kumwacha apige simu hiyo na hapo ndio ingekuwa chanzo cha machafuko Nigeria.

Mwaka 2011,April baada ya Mahammudu Buhari kutamka kuwa hakuridhishwa na matokeo ya uhaguzi baada ya Goodluck Jonathan Kushinda;machafuko yalitokea nchini Nigeria na taasisi ya Civil Rights Congress iliripoti zaidi ya watu 500 waliuawa kaskazini mwa Nigeria.

Kwa kiongozi yeyote ni lazima atambue kuwa demokrasia haiwi imara pale unaposhinda tu bali pia pale unaposhindwa.Kwa uamuzi huu mdogo,ameiacha Nigeria salama na kuiepusha kutoka katika umwagaji damu.

Mara baada ya kushindwa alitoa tamko lake lililowagusa wanaigeria na pia dunia nzima kwa ujumla alisema “As I have always affirmed, nobody’s ambition is worth the blood of any Nigerian. The unity, stability and progress of our dear country is more important than anything else”.akimaaanisha kama alivyosisitiza wakati wote hakuna matamanio ya cheo ya mtu yeyote yanatakiwa yawekwe juu kuliko uthamani wa damu ya wanaigeria na amani,umoja na utulivu wa Nigeria ni muhimu zaidi ya kitu chochote kile.

Tanzania inapoelekea katika uchaguzi mkuu hili ni funzo muhimu sana kwa watakaoshindwa.

Joel Arthur Nanauka
me@joelnanauka.com

Leave a comment

name*

email* (not published)

website