Navigate / search

Sifa Mbili Muhimu za Kukusaidia Usipoteze watu wa Muhimu Maishani Mwako

shutterstock_7024555

Kuna sifa mbili ambazo ni lazima uwe nazo maishani ili Kujenga uwezo wa kupata fursa zaidi na kudumisha mahusiano yako na watu wanaokuzunguka.
Ni Lazima kutambua kuwa UWEZO au KIPAJI pekee hakitoshi kukufikisha unakotaka kwenda, ni lazima ujenge Tabia rafiki za kuwawewezesha wengine wawe comfortable na wewe.

1)Uwe Tayari Kukosolewa
Umeshawahi kuwa karibu na watu wanaojifanya wanajua kila Kitu? Hawapendi kukosolewa,hawapendi kuambiwa upande wa pili wa jambo pia hawapendi kusikiliza wengine.
Wengine wana Kitu kinaitwa “intellectual arrogance “,wanaona wao wana akili kuliko mtu yeyote.Kumbuka kuwa hakuna bosi atakayemvumilia mtu wa namna hii,hakuna rafiki anayependa kuwa karibu na watu hawa.Kwa sababu ya ujuaji wao wakiwafanya mambo yatakayowaharibikia watu huwa hukaa kimya na hawaambii chochote kwani wanajua ni watu wasiopenda ushauri,na pia huwa hawadumu na marafiki kwani baada ya muda watu huwakimbia.

Plato alisema “I am the wisest man of all the people because I know one thing, and that thing is I know nothing “
Ukitaka kuwa mwenye hekima kubali kukosolewa kwani kuna vitu hauvijui.

2)Uwe tayari kuomba msamaha
Kuomba msamaha si udhaifu bali ni kiwango cha juu cha kukomaa na kujitambua (only the strong and matured can ask for forgiveness). wengi wanaoshindwa kuomba msamaha ni wale wenye inferiority complex.
Unapoomba msamaha unapandisha kiwango Chako cha kuaminiwa zaidi na unatoa fursa ya kudumisha mahusiano na wengine pia.Watu ambao kila wakati hutafuta namna ya kujitetea makosa yao hata pale wanapojua wamekosea huwa hawafiki mbali maishani.Ukichelewa appointment kwa kuchelewa kuamka usisingizie foleni.

LEO:Ukikosolewa kubali, na kama kuna ulipokosea omba Msamaha.

Endelea Kutembelea (www.JoelNanauka.Com) kujifunza Zaidi

Comments

onsphorius Balambirwa
Reply

Safi sana comrade

nanauka
Reply

Karibu sana

Leave a comment

name*

email* (not published)

website