Navigate / search

Sifa 5 za Malengo Yanayofanikiwa

 

Screen-shot-2012-07-07-at-12.17.51-PM

Kama ukijaribu kuuliza ni yapi malengo ya watu wengi katika maisha, hakika watakupa majibu yasiyo sahihi ama yasiyo kamilika, kama vile; nataka kufanikiwa, kuwa na furaha, kuwa na maisha bora na hayo ndiyo. Yote yanakuwa matamanio hakuna malengo sahihi.Zifuatazo ni sifa 5 za malengo ambayo yatafanikiwa sikuzote.

Malengo lazima yawe;

1)Yawe Mahususi:Kwa mfano nataka kupunguza uzito. Haya ni mawazo ya kufikirika. Yatakuwa malengo ikiwa nitajiumanisha ” nitapoteza kiasi cha Kilo 10 katika siku 90.”.Hii ni tofauti na mtu nayesema nataka kupunguza uzito mwaka huu.Ama anayesema mwaka huu nataka kuanza kujifunza kuendesha gari mwezi wa sita tarehe kumi na tano kwenye chuo cha Veta;yuko kwenye nafasi nzuri ya kufanikiwa kuliko anayesema,mwaka huu hauishi kabla sijaweza nkuendesha gari.

 

2)Yawe Yanapimika:Kama yatakuwa hayapimiki, hatuwezi kuyafanikisha. Kipimo ndiyo njia ya kusimamia mafanikio yetu.Kama malengo yako hamna namna unaweza kuyapima basi ni sawa na kusema kuwa ni ngumu kujua kama unapiga hatua kwenda mbele ama la.

 

3)Yanawezekana kufikiwa:Kuwezekana maana yake ni kufikiwa na kuwa licha ya changamoto lakini yasiwe mbali na malengo, lasivyo itakuwa kupoteza matumaini.

 

4)Yawe Halisi na uhakika:Mtu anayetaka kupoteza kilo 50 kwa siku thelathini si mkweli,ni sawa na anayeweka malemgo ya  kuwa mkurugezi wa benki ya kimataifa  baada ya mwaka mmoja kumaliza shahada yajke ya kwanza.

 

5)Yawe na Muda maalumu:Lazima yawe na tarehe ya kuanzia na kumalizia.Malengo yasiyo na atrehe ni upotezaji wa muda na nguvu.Umuhimu wa tarehe ni kuhakikisha kuwa unazingatia kupiga hatua kila siku kuelekea katika lengo kubwa la Maisha yako.Kila lengo ligawe katika malengo madogomadogo utakayoyawekwa muda

Angalia malengo yako na kama yana hizi sifa zote,kama hayana.Ni wakati wa kushughulikia,.

Kumbuka

 

Ninaamini katika NDOTO yako,

Ninaamini katika UWEZO wako,

Ninaamini katika KESHO yako.

Joel Arthur Nanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website