Navigate / search

Sifa 3:Jitahidi Uwe nazo Ili Kuharakisha Mafanikio Yako

index 2

Kuna sifa ambazo ukiwa nazo katika maisha yako huwa ni chanzo cha fursa nyingi kuja kwako tofauti kama sifa hizo hauna kabisa.Kama ambavyo kila wakati huwa napenda kuwakumbusha,jinsi ulivyo ni muhimu kuliko unachofanya katika kuelekea mafanikio yako(In the Journey to your success ,what you become is very important than what you do).Kwa maneno mengine kinachotofautisha wengi sio kile wanachofanya,bali vile walivyo.Hii ndio maana wengi wanafanya vitu vinavyofanana ila wanapata matokeo tofauti.

Katika kulitambua hilo,watu wanaofanikiwa huwa na sifa zinazofanana ambazo ndizo huwa msingi wa mafanikio yao ya kila siku.Leo kuna sifa tatu kuu nataka tujifunze:

1)Wanafanya mambo kwa Haraka.

Watu waliofanikiwa huwa si watu wa kuchelewachelewa au kughairisha kufanya mambo,wakishaamua kufanya kitu ama wakipewa jukumu ni watu ambao huwa hawachelewi kutekeleza.Kwa sababu hiyo hujikuta hawana viporo vya majukumu yao na pia huwa ni watu wanaoaminiwa sana.

Kama umeshaamua kufanya biashara,kutafuta kazi ya kuajiriwa ama kusoma,epuka kughairisha kila wakati mipango yako.Kuna watu kila mwaka ukikutana nao wanakuleza wazo lilelile la tangu miaka mitatu iliyopita ambalo bado hawajaweza kulitekeleza hadi leo.

Je,kuna jambo umeamua kulifanya?Anza Mara moja kutekeleza leo bila kuchelewa.

2)Wanafanya mambo kwa Vipaumbele

Kuna watu wengi wako bize sana kila siku lakini huwa wako bize na mambo ambayo hayana mchango mkubwa katika maisha yao.Watu wanaofanikiwa ni wale ambao hutambua tofauti ya mambo ya muhimu na yasiyo ya muhimu.Kabla hawajajiingiza katika jukumu lolote,huwa wanajiuliza umuhimu wake kwanza.
Usikubali kutumia muda wako kwa mambo ambayo hayachangii kabisa ama yanachangia kidogo katika ndoto yako kubwa.

3)Huwa wanadhibiti wezi wa Muda wao

Kila siku tunakabiliana na wezi wa muda wetu.Wengine wanaibiwa muda na magazeti ya udaku,wengine wanaibiwa muda na mitandao ya jamii,wengine wanaibiwa muda na stori za wasanii n.k,ili mradi tu muda wako unapotea.Kumbuka kuwa muda wa kujifurahisha ni ule ambao umeshachoka baada ya kufanya kazi zenye manufaa.

Ili kufanikiwa ni lazima ujiulize swali hili?Hivi wezi wa muda wangu ni vitu/watu gani?Ukishagundua hilo chukua hatua kukabili na usikubali kupoteza muda wako tena.Kama mwizi wako ni group flani la watsaap,pima uzito wake-unaweza kulimute hadi unapotaka kusoma ama kama halina umuhimu kabisa unaweza kujitoa pia.Kumbuka kuwa kila muda unaopoteza hautarudi tena katika maisha yako.

Endelea Kutembelea Ukurasa wangu wa Facebook iil Kujifunza Zaidi,na kama ujumbe huu umekuwa na manufaa zaidi,unaweza kushare na rafiki zako.Pia unayo fursa ya kujiunga na mtandao wa washindi ili kujifunza zaidi kupitia watsapp group bila gharama yoyote;Tuma neon “NDOTO YANGU”,Ikifuatiwa na jina lako kwenda namba 0655 720 197.

Ili kupata Makala za kila wiki za kujifunza jinsi ya kuifikia ndoto Yako,tafadhali nenda kwenye website yangu na chini upande wa kulia kwenye “weekly newsletter” andika email yako pale kisha itume.

Ndoto Yako Inawezekana,

See You At The Top.

Comments

Milton ngungulu
Reply

Kila nikisoma makala zako ndg natiwa nguvu sana na kijikuta nazidi kustawi kifikra na mtazamo. Hongera sana , Mungu azidi kukfanya bora zaid

nanauka
Reply

Sana Milton,Hilo ndilo lengo kuu.Kuhakikisha kuwa tunapata mitazamo mipya itakayotuwezesha Kufanikiwa Zaidi.

PETER ADAM
Reply

brother i am so inspired with your message for real they bring me up and accelerate my archivement ….be blessed brother

nanauka
Reply

Nafurahi sana kusikia hivyo Peter.

william B.Manyilizu
Reply

nafurahi sana kujifunza kupitia articles zako.mara ya kwanza nilikusikia Temino ya clouds fm nilipenda sana mafundisho yako.jina ckulishka cku ile nilitafta mbino sana niijue blog yako mwisho niliipata na hutumia muda wangu sana kusoma hii kitu na kubadilisha mitazamo yangu…
ubarikiwe sana na uongeze zaidi ya hapo

nanauka
Reply

Ahsante sana William,tuendelee Kujifunza.Naamini utatimiza ndoto Yako.

daud costantine
Reply

asante sana kwa mafundisho mazuri

egla
Reply

Kila siku nimekuwa nikijifunza katika makala zako. Na nimeshaanza kuona mabadiliko maishani mwangu. Mungu akubariki sana kaka Joel.

nanauka
Reply

Amina Rgla,ahsante sana kwa mrejesho.Nafurahi kusikia nimekusaidia kwa sehemu.

Abel Luhamba
Reply

Safiii ubarikiwe sana nimefunguka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website