Navigate / search

Sam Adeyemi:Jinsi Kukosa Fursa Kulivyomfanya Kuwa Bilionea

maxresdefault

Kama walivyo vijana wengi wa kiafrika,na yeye baada ya kumaliza masomo yake ya chuo kikuu miaka ya 90 aliamua kuanza kutafuta nafasi za kwenda kusoma nje ya nchi akiamini kuwa huko kuna maisha mazuri sana.Kama bahati nzuri alipata kufahamiana na tajiri mmoja ambaye alikuwa anamiliki shirika la usafirishaji la ndege na tajiri huyo alikuwa na uhusiano wa karibu sana na ubalozi wa uingereza,hivyo ilikuwa ni jambo rahisi kwake kumtafutia kijana huyu viza bila matatizo yoyote.

Hata hivyo wiki chache kabla ya safari huku kila kitu kikiwa kimekaa vizuri na uhakika wa kwenda kusoma uingereza umepatikana,tajiri huyu alijikuta matatani kwenye uhusiano wake na ubalozi na hivyo kuaminika kwake kote kukapotea,na hii ilipelekea uwezekano wa kupata viza kupitia yeye kupotea kabisa.Ingawa kijana huyu alijitahidi kufanya kila alichoweza ili kufanikisha alijikuta ameshindwa kutimiza ndoto yake ya kwenda kusoma chuo kikuu nchini UIngereza.

Baada ya hapo aliona kama vile maisha yamefikia mwisho na hana tena tumaini maishnai,alihesabu kama vile ni mtu mwenye bahati mbaya kabisa maishani na hawezi tena kufanikiwa,maisha yake baada ya tukio hili yalikuwa yamejaa machozi,vilio na manu’guniko kila siku.Lakini miaka kadhaa baada ya tukio hili yuko wapi?

Hapa namzungumzia mtu anayeitwa Sam Adeyemi,abaye kwa sasa ni kati ya wazungumzaji maarufu duniani,akiwa anamiliki kampuni yake ya Success Power International,ni mashauri wa makmapuni mengi ya kimataifa na anaongoza kituo kikubwa cha mafunzo nchini Nigeria cha Daystar Christian Centre,ana vipindi mbalimbali katika televisheni,redio na amechapisha vitabu vingi sana vya kuwasaidia watu waweze kufanikiwa.Kiufupi amefanikiwa sana kifedha kwa sasa na ni mtu mwenye furaha na familia yake.

Alipokuwa anaeleza historia yake hii anasema baada ya kuwa katika hali ya kukata tamaa alipoona ndoto yake ni kama vile imekufa,alifanikiwa kupata kitabu cha Robert Schuler cha “Tough Times Never Last,but Tough people do” yaani nyakati ngumu huwa hazidumu milele ila watu ng’ang’ari huwa wanadumu.Ni kweli,maisha yake yamethibitisha hilo.

Kuna wengi huwa wanapitia mazingira kama haya,kama haujawahi kupitia katika kuelekea kilele cha ndoto yako pengine kuna siku utapitia pia.Unafika wakati ambao ni kama vile ndoto yako haitaweza tena kufanikiwa,ni kama vile kuna fursa ambayo uliitamani,ulifanya bidii,uliisubiri sana na kuifuatilia sana lakini na ulikuwa na uhakika kuwa utaipata-Ghafla kutoka kusikojulikana inapotea na ni kama vile tumaini lako linakufa kabisa.

Jambo la kwanza unalotakiwa kujua ni kuwa kila wakati katika maisha kuna “second chance”,unayo fursa ya pili kutimiza ndoto yako.Haijalishi muda uliopoteza ni mwingi kiasi gani,haijalishi hasara uliyopata katika biashara uliyokuwa unafanya ni kubwa kiasi gani,haijalishi ulifeli kwa kiwango gani,haijalishi uliumizwa kwa kiwango gani huko nyuma-Bado unayo “second chance”.Napenda maneno ya George Bush siku moja akiwa katika mahafali moja ya chuo kiku kama mgeni rasmi aliwaambiwa wanafunzi”Wale mliopata A na kuwa wanafunzi bora,hongereni sana,ila wale mliopata C kumbukeni;kama ilivyokuwa kuwa kwangu nanyi mnaweza kuja kuwa maraisi”
Usikubali jambo lolote baya lililotokea maishani mwako likufanye ufikiri hauna namna ya kuinuka ama kufanikiwa tena.

Jambo la pili ni kuwa kuna mambo mengi ambayo yakitokea yanakuwa kama ni mabaya lakini ukweli ndani yake kunakuwa kuna mambo mazuri yamejificha,yaani “Blessings in disguise”.Hivi hakuna kitu maishani mwako kilitokea ukakikosa na mwanzoni uliona kama umepoteza lakini mwisho wa siku ukashukuru kwamba ulikosa baada ya kuona madhara ambayo ungepata?Binafsi nilishawahi kukosa nafasi ya kazi niliyoitamani sana lakini baada ya kuwekewa mizengwe alipewa mwingine lakini unajua nini kilitokea? baada ya mwezi mmoja nilikuja kupata kazi nzuri sana mara mbili kwa ubora na maslahi ya ile ya kwanza.

Bila kujali umepitia katika magumu ya kiwango gani,kuna jambo moja unatakiwa kila siku kuliamini kuwa;Kuna jmabo jema liko njiani linakuja kwako,Usikate tamaa.Kanuni ya maisha ni kuwa-Ukiona umepoteza kitu bora ujue kilicho bora zaidi kinakuja.Siku zote kumbuka-“When you loose your Silver ,it’s time to go for the gold”-Ukipoteza medali ya fedha,ni wakati wa kufukuzia medali ya dhahabu.Nasubiri Siku Utakapoitazama jana yako na Kufurahi kwa Fursa Ulizokosa kwani ziliiboresha leo yako.

See You At The Top

Leave a comment

name*

email* (not published)

website