Navigate / search

Sababu 3 Zinazosababisha Watu Washindwe Kutatua Changamoto Zinazowakabili

maxresdefault

Siku moja nilikuwa namsikiliza Jim Rohn akifundisha kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika kujiendeleza uwezo wako katika katika maeneo mbalimbali.Alisema kuwa mentor wake alimwambia siku moja jambo la muhimu sana katika maisha yake-“Don’t wish things were easy,wish you were better”-Usitamani mambo yangekuwa marahisi bali tamani wewe ungekuwa bora ili uweze kuyakabili.

Huu ndio mtazamo unaoweza kukusaidia kila siku katika maisha yako,kufanya bidii na kujitahidi kuwa na uwezo wa juu Zaidi na maarifa ya juu Zaidi kuliko yale uliyonayo kwa sasa.Ukweli ni kwamba,kama utaamua kujiongeza katika uwezo ulionao wa sasa utajikuta unaweza kutatua changamoto nyingi zinazokukabili.

Kuna sababu 3 kwa nini watu wengi wanashindwa kutatua changamoto wanazokabiliana nazo:

1)Hawaamini kama wanaweza kuzitatua

Watu wengi leo wamenasa katika mtego wa kuamini kuwa hawana uwezo wa kupata suluhisho la tatizo walilonalo,kwa sababu ya Imani hii;watu wengi wamejikuta wanaamua kukubaliana na kuvumilia hali walizonazo.Nimeshakutana na watu wengi sana ambao husema,”nimeamua kuvumiila nitafanyaje sasa,sina uwezo”.Haujaumbwa ili kuvumilila matatizo yanayokukabili,umeumbwa ili uyatatue na upige hatua.Chunguza matatizo yanayokuzunguka leo na ujiambie nafsi yako-“Hata tatizo hili lina suluhisho,sitakubali kushindwa kulitatua”

2)Kusubiri watu wengine wawasaidie

Kama kuna kitu hatari ni kuwa na mtazamo wa kusubiri mtu mwingine akusaidie,ukiwa wa namna hii utachelewa sana kufanikiwa.Kuna watu wanaamini ni haki yao kusaidiwa,kulipiwa ada,kupewa mtaji n.k.Ukweli ni kuwa hauna haki hiyo,mtu akiamua kukusaidia ni kwa kupenda kwake mwenyewe na sio jukumu lake.Watu wengi leo ukiwauliza mbona umekwama-wanaanza kuorodhesha watu wanaosubiri wawasaidie..HAPANA-Chukua hatua mara moja,anza kutumia kile ulichonacho na kile unachoweza kwa sasa na msaada utakukuta njiani.Tafiti zinaonyehs kuwa watu wengi hupenda kuwasaidia watu ambao tayari wameshapiga hatua.

3)Hawaongezi uwezo wao wa maarifa.

Albert Einstein alishawahi kusema-“We can’t solve our problems at the same level of thinking we used when we created them” akimaanisha,huwezi kuktatua tatizo kwa kutumia kiwango kilekile cha uwezo wako wa kufikiri ulichokuwa nacho wakati unapata hilo tatizo.Kila chanagamoto inayokukabili leo inahitaji uwezo mkubwa Zaidi wa kufikiri au maarifa ili uweze kuitattua.Kinachofanya changamoto iwe ngumu,sio kwa sababu ya jinsi ilivyo bali kwa sababu ya uwezo mdogo wa maarifa uliyonayo.
Chunguza changamoto zinazokukabili leo na jiulize,je?Kuna maarifa gani natakiwa kuongeza katika eneo hili ili niweze kukabiliana na changamoto hizi na kuzishinda?
Leo utakapokutana na kila changamoto maishani mwako;usitamani chnagamoto hiyo ingekuwa nyepesi Zaidi bali tamani kuwa na uwezo mkubwa kuliko changamoto inayokukabili.Nakutakia mafanikio katika kutimiza malengo yako ya siku ya leo.

Kumbuka ndoto Yako Inawezekana.Endelea kutembelea www.JoelNanauka.Com kujifunza Zaidi.

See You At The Top.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website