Navigate / search

Ripoti ya CAG Yafichua Ufisadi kila Kona

D92A2489

Ripoti mpya iliyotolewa ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa serikali imebaini ufisadi wa kila kona na kuendelea kuonyesha jinsi pesa za watanzania zinavyotumika vibaya.
Dhambi ya kuendelea kulipa mishahara hewa kwa watumishi wa umma imesababisha serikali kupoteza Sh. bilioni 1.01 zilizokuwa zitumiwe nahalmashauri na serikali za mitaa kwa mwaka wafedha unaoishia Juni 30, 2014.Hasara hiyo imetokana na halmashauri 36 kulipazaidi ya Sh. bilioni 1.0 kwa wafanyakazi,marehemu, wastaafu, watoro na waliofukuzwa.Taarifa hizo ni kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzina Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyotangazwa jana mjini Dodoma . Mkaguzi MkuuProfesa Musa Asad, alisema na kuongeza kuwahali kama hiyo ilijitokeza kwenye watumishi wa umma na serikali ambako zaidi ya Shilingi milioni141. 4 zililipwa kwa mwaka huo.Mkaguzi Mkuu alieleza kuwa marehemu
walioacha kazi wastaafu mbali na kulipwa mishahara walilipiwa bima za matibabu, kodi ya mshahara (Paye) na michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii.“Hili linatokana na kuchelewa kuwaondoa watumishi hao kwenye mtandao ya orodha ya mishahara ya watumishi wote.”Aliongeza: “Hali hii bado inaendelea licha yakuwa serikali imewekeza kwenye mfumo wa kompyuta wa LAWSON kama njia mojawapo yakudhibiti upotevu huu,” alisema Mkaguzi Mkuu.Aliongeza kuwa milioni 845 zinazohusiana na halmashauri 32 zililipwa kama makato ya pensheni, bima ya afya, TRA kwa watumishi hewa.

HUJUMA MADINI
Makampuni ya madini ya Geita Gold Mine na Resolute Tz Ltd, yameisababishia serikali hasaraya Sh. bilioni 22.33 kwa kuhujumu misamaha ya kodi waliyopewa. Wawekezaji hao walipewa msamaha wa kodi ya mafuta yanayotumika kwenye migodi yake ambayo yana thamani ya Sh. bilioni 22.33, kwa mujibu wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Musa Asad.
Alikuwa akizungumzia ripoti ukaguzi ya hesabu za serikali kwa mwaka unaoishia Juni 30,2014.

Alisema ufisadi huo uliotokea kwa vile kampuni hizo, hazikutumia mafuta hayo badala yake iliyatoa kwa wakandarasi wasiostahili msamaha huo hivyo kutumiwa bila kulipiwa ushuru nakuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 22.33. Alitaja ufisadi mwingine uliosababisha hasara ya Sh. milioni 392.7 ulifanywa na kampuni ya Kiliiwarrior Expeditions ya Arusha iliyokuwaimesamehewa kodi ya Sh. milioni 465.2 ili kuingiza magari 28. Alifafanua kuwa kampuni hiyo ilitumia misamaha hiyo kinyume cha malengo na Mamlaka ya Mapato (TRA) ilipata kiasi cha Sh. milioni 72. CCM, CHADEMA CUF HATI MBOVU VYAMA vya siasa vya CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi vimepata hati zenye shaka zilizotolewa na Ofisi ya CAG, kutokana na taarifaza fedha zisizoridhisha. Alisema vingine vilivyopata hati hiyo ni TLP na Chaumma, huku vyama vya NLD, UMD, ADC, NRD, APPT na SAU vilipata hati mbaya ya ukaguzi.Akizungumzia vilivyopata hati zenye shaka,alisema katika ukaguzi wa vyama 12 ilibainika kuwa taarifa zao za fedha zilifanywa tofauti na misingi ya uhasibu na mfumo wa uandaaji wa taarifa za fedha. Alieleza kuwa hadi Juni mwaka 2013 hesabu za vyama vya siasa 21 zilikaguliwa kati ya hivyo ni vyama 12 vilivyowasilisha taarifa zake wakati vyama tisa havikuwasilisha taarifa. “Vyama hivi ni UPDP, TADEA, UDP, Demokrasia Makini, CHAUSTA, DP, Jahazi Asilia, AFP na CCK.”Alisema Profesa Asad.

Alisema katika ukaguzi wa taarifa za fedha tatizo la kuchelewesha uwasilishaji ripoti za fedha zavyama kwa CAG limejiri na kupendekeza kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kushirikiana na Bodi ya Taifa ya Wahasibu waandae muongozo wa aina ya muundo wa taarifa za fedha utakaotumiwa na vyama vyote vya siasa.

MASHIRIKA YANAYOCHAKACHUA
Pia GAC ameitaja Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro kuwa imefanya ufisadi wa zaidi yaSh. bilioni 2.3 (Dola milioni 5.54) kwa kununua bidhaa zisizokuwa na sababu ya msingi.Pia Kampuni ya Simu ya TTCL nayo ilinunua manunuzi yasiyokuwa na lazima yenye thamani
ya Sh. milioni 381.97 (Dola 986, 938) kama ilivyofanya Ngorongoro.Kadhalika imelitaja Shirika la Nyumba la Taifa,(NHC) kuwa limefanya manunuzi bila kushindanisha wazabuni yenye thamani ya Sh.bilioni 1.75.Kwa upande wa deni la serikali katika mifuko yahifadhi ya jamii limefikia Sh. bilioni 1.6 Juni mwaka jana, kwa mujibu wa Mkaguzi Mkuu Profesa Mussa Asad.
Akizungumzia suala la kukataa kutumia mashine za stakabadhi za kielektroniki (EFDs) , ameshauri serikali isifanye biashara na kampuni kama haitumii EFDs.Alisema ofisi yake ilibaini kuwa yamefanyika malipo ya Sh. bilioni 4.4 yasiyo ya risiti hizo kwenye serikali kuu, wakati malipo mengine ya Sh. bilioni 4.6 yalifanywa kwa halmashauri mbalimbali. Alisema ili kuondoa kiburi cha kukataa EFDs serikali kuu na zile za mitaa zisifanye biashara nawasiotumia risiti hizo.
SOURCE: NIPASHE

Leave a comment

name*

email* (not published)

website