Navigate / search

Rais Ajaye anatakiwa Kuanza na Vipaumbele Hivi.

index

Katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Tarehe 25 Oktoba,ni wazi kuwa Taifa letu linakabliwa na changamoto ambazo zinahitaji mtu mwenye uwezo wa kipekee aweze kuzitatua ili kuvusha wananchi kutoka hatua ya sasa hadi ile wanayoitamani.

Wakati benki ya dunia inaonyesha kuwa uchumi wa Tanzania unaendelea kuimarika kwa ukuaji wa 7% kwa mwaka,ni dhahiri kuwa maendeleo ya watu(Human Development) imeendelea kuonyesha kuwa hali za wananchi bado ni dhaifu.Najua wako wengi wamejitokeza katika kuonyesha nia yao ya kuwa viongozi wa Taifa letu;bila kujali majina yao leo nitaanza kuelezea majukumu mbalimbali yanayomkabili kiongozi wa nchi yetu ajaye;

1)Kupambana na Adui namba 4 anayeendelea kudhoofisha nchi yetu.
Baba wa Taifa mwalimu Julius K. Nyerere alisema kuwa kama Taifa tunakabiliwa na maadui watatu;Ujinga,Umaskini na Maradhi.Hata hivyo kwa mazingira ya sasa ni wazi kuwa kuna adui ambaye ni jitu kubwa Zaidi la ufisadi.

Ufisadi ndio unaosababisha tushindwe kupeleka pesa za kutosha kwa kulipa madeni ya walimu Zaidi ya bilioni 300 ili kuboresha elimu;na kwa kufanya hivyo ujinga unashamiri.

Ufisadi ndio unaosababisha pesa ambazo zilitengwa kwa ajili ya mendeleo ya wananchi ziliwe na wachache na kuendeleza umaskini Zaidi.

Ufisadi ndio unaosababisha dawa zisipatikane mahospitalini na kuuzwa kupitia maduka binafsi ya viongozi wa afya.Kiufupi ufisadi ndio chanzo cha maadui hao wengine watatu.

Rais ajaye anatakiwa aanze na “Operesheni safisha Nyumba” kama ile aliyoifanya Lt.Jerry Lawrings mikaa takribani 37 iliyopita.Kwa upande wake Lawrings aliagiza kuuwawa kwa viongozi 8 waliohusishwa na ubadhirifu na Rushwa na ufisadi,wakiwemo majenerali wa jeshi na marais wastaafu 3.

Ingawa hii si njia ambayo anatakiwa kuitumia Rais huyu mpya wa Tanzania lakini jambo la msingi ni kuwa anatakiwa kuchukua hatua nzito zisizo na mashaka kuwa amekusudia kuisafisha serikali na nchi kutoka katika wimbi hili la Ufisadi.

2)Kufufua na kuanzisha viwanda vipya.
Katika kukuza uchumi wa Tanzania na kuelekea kuwa Taifa la kati ni wazi kuwa suala la uzalishaji na uuuzaji wa bidhaa za Tanzania nje ya nchi ni lazima ufanyike kwa juhudi za makusudi.Kuendelea kupiga mayowe ya kuwa na uchumi wa gesi ni kujenga matumaini ambayo yanaweza kugeuka kuwa shubiri kwa wananchi hapo baadaye kama matokeo yake hayataonekana.

Ukweli ni kuwa tafiti zinaonyesha kuwa nchi nyingi za Afrika hazijafaidika sana na rasilimali za gesi na mafuta hasa kwa tabaka la chini la watu maskini.
Nchi kama Nigeria inayongoza kwa uzalishaji wa mafuta ghafi Afrika bado ina asilimia 68% ya watu wake wanaishi chini ya Dola moja na 80% ya mapato ya mafuta yanaenda kwa watu 1% ya watu wote.Lakini pia ziko nchi nyingi ambazo uchumi wake umekabiliwa na “dutch disease” ambapo sekta ya mafuta na gesi imeongeza thamani ya pesa za nchi zinazozalisha na hivyo kufanya bidhaa zake kuwa za ghali kusafirisha nchi za nje.

Hivyo suluhisho la kudumu ambalo nchi nyingi zimefanya ni kuwa na mapinduzi ya Kilimo yanayoambatana na viwanda kuongeza thamani ya bidhaa mbalambli.Hii itafanya mambo makubwa mawiil:Moja ni kuongeza nafasi za ajira za watanzania na pili ni kuhakikisha thamani ya mazao tunayouza nchi za nje inapanda na hivyo kuwanaufaisha wakuliama wetu ambao wamekuwa wnanyonywa kwa miaka mingi.Nchini Ivory Coast,Karibu kokoa yote wanayoizalisha inauzwa nchi za nje na kurudishwa nchini kwao kchocolate,na bei wanayouziwa kwa chocolate moja ni gharama kuliko bei inayouzwa ufaransa.

Wakati Mwalimu Nyerere anakabidhi nchi mwaka 1985 aliacha mashirika ya umma takribani 250 na viwanda lukuki; Zana za Kilimo (UFI) ambacho kilikuwa maalum kwa ajili ya kutengeneza zana za kilimo. Vingine ni Tanzania Sewing Thread na Poly Sacks. Viwanda hivyo hivi sasa havifanyi kazi.

Vipo vya nguo vilivyokufa au kusuasua kama vile Sunguratex, Kiltex, Tabora Textile, Mwanzatex, Mbeya Textile na kadhalika.Pia,kiwanda cha kusindika nyama cha Tanganyika Packers ambacho kilikuwa kikizalisha nyama za kopo zilizokuwa zikiitwa Frey & Bentos na zilikuwa zikiuzwa ndani na nje ya nchi.

Kulikuwa na viwanda vya magunia Moshi na Morogoro, Kiwanda cha Ngozi Morogoro,viwanda kumi na mbili vya kubangulia korosho na kadhalika,.

Nchi za mashariki zilizojulikana kama Asia Tigers,ziliweka mkazo sana katika eneo hili na sio ajabu kuona kuwa leo zinasafirisha bidhaa zake nyingi kwenye nchi mbalimbali ikiwemo nchini kwetu.Uchumi wa Tanzania hautajengwa kwa uchuuzi ama kilimo uchwara,bali kwa kuhakikisha viwanda vinafufuka.Rais ajaye lazima aweke kipaumbele katika kuwekeza uzalishaji kupitia viwanda vyetu;Itatengeneza ajira,itaimarisha pesa yetu na itatuepusha na imported inflation.Ni hatari kwa nchi yetu hadi kuagiza toothpick kutoka kenya na China.Hili ni lazima lipewew kipaumbele.

Itaendelea

Joel A. Nanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website