Navigate / search

Part 2:Sababu 7-Kwa nini CCM wengi wamejitokeza nafasi ya Urais?

b3

Katika awamu ya kwanza tuliangalia sababu kubwa 4 za kwanza zilizosababisha ututiri wa wagombea wa nafasi ya urais wanaoomba ridhaa kupitia chama cha mapinduzi.Katika kuendelea kupanua ufahamu wetu,tunaendelea kuangalia sababu 3 zilizobakia zinazoeleza sababu za kuwa na watu wengi kiasi hiki katika kinyan’ganyiro cha Urais kwa wakati huu.

Tunachagua kama Vipofu,kisha tunalalama kama vichaa.Sasa tuamue;ama tuchague viongozi wetu makini au tukae kimya wakati wakitunyanyasa.Wachagua hovyo wasiwe wasema hovyo wakitendewa hovyo-Jenerali Ulimwengu

5)Wanaojiandaa kwa Uchaguzi ujao wa Urais.

Ni kawaida sana katika siasa kujijenga kwa kugombea nafasi za uchaguzi ili kujiwekea akiba ya mbeleni.Hata Rais Kikwete kushindwa kwake ka mara ya kwanza kulimjengea jina na kutengeneza matarajio ya watu kwa uchaguzi uliofuata,na bila shaka aliwazidi wagombea wenzake mbali sana kwa kuwa na mtaji wa uchaguzi wa miaka 10 iliyopita kabla ya uchaguzi.
Si kila anayejaribu mbinu hii inafanya kazi lakini nimefanya kazi kwa walio wengi.Hatari yake ni kuwa kama utashindwa vibaya sana utaonekana haufai kabisa lakini pia unapotangaza kugombea watu wanakuchambua hadi nukta ya mwisho.Kizazi cha baada ya uhuru wengi wanataka kutumia mbinu hii kujijenga kisiasa kwa ajili ya uchaguzi ujao.SI ajabu kati yao wakafika hatua za juu na kujenga matarajio makubwa kwa ajili ya uchaguzi ujao.
6)Kurahisishwa Kwa Taasisi na cheo cha Rais

Kadiri siku zinavyoendelea ndivyo taasisi ya urais inavyozidi kuwa wazi na mambo mengi kufahamika kuhusiaana na Urais.Pia imeendelea kuwa rahisi sana kufahamu mambo ya ikulu kwa karibu hasa kwa watu walioko katika serikali.Ikulu imekuwa si ya mambo ya siri saaaaana kama ilivyozoeleka huko nyuma.

Katika tabia ya kawaida uoga unakuwa mkubwa kadiri unavyokuwa haujazoea kitu,lakini kadri mazoea yanavyokuwa makubwa ndivyo na hofu inavyopungua.Kuendelea kuwa na wepese na urahisi wa kufahamu,kuwepo,kushiriki na kuhusika kwa wwengi kwenye mambo yanayohusu taasisi ya Urais imewafanya wengi waamini kuwa yeyote anaweza kuimudu kazi hii kwa ufanisi.
Wakati mwingine namna mambo yalivyoendeshwa katika nchi na Maamuzi yalivyochukuliwa kiwepesi na kimzaha imeonekana kama vile yeyote yule anaiweza nafasi hii.Ukweli ni kuwa namna serikali na taasisi ya Urais imekuwa ikiendeshwa hivi karibuni imefanya ionekane kuwa ni jambo jepesei sana kwa yeyote kuliweza kulifanya.
7)Kukosekana kwa Exceptional Candidates(wagombea wenye sifa za Kipekee)

Kadiri kunapokosekana mgombea/wagombea wenye uwezo mkubwa wenye tofauti sana na wengine ndivyo mbio za Urais zinavyoendelea kuvutia watu wengi kila mtu akitaka kujaribu bahati yake.Mbio za Urais huwa nyepesi Zaidi kama kuna wagombea wenye sifa za kipekee zinazowatofautisha na wengine wote(The ones who can stand out of the crowd).Bahati mbaya sana tumeingia kipindi ambacho wengi wa wanasiasa wanaotaka kujihusisha na mbio hizi wamekuwa hawaaminiki na wananchi.Hii imepelekea kukosekana kwa wagombea ambao wamewazidi kwa mbali saaana wagombea wengine.Ni kusema kuwa karibu wagombea wote wanatofautiana kidogo sana kwa sifa za uongozi.
Hii inapotokea inasababisha kila mmoja aone ana nafasi ya kuweza kushinda hivyo kujitokeza.

Najua wapo wasomaji wangu ambao walitamani ningetaja majina;bahati mbaya sana hilo halikuwa dhumuni la makala haya.Hata hivyo ni vyema kutambua kuwa uchambuzi hii ni matokeo ya mawazo binafsi na hayajajengwa katika matokeo ya utafiti wowote.Hata hivyo,pasipo na shaka ni wazi kuwa yaliyozungumzwa hapa yanaakisi ukweli usioweza kupingwa kirahisi.

Katika hali ya namna hii kunaweza kutokea ushindani MKUBWA sana ama kukawa HAKUNA ushindani kabisa.

 

Tanzania ni Nchi Yetu,

Watanzania ndio Sisi,

Tuendelee kuipenda na Kuitumikia,

 

Joel Arthur Nanauka

 

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website