Navigate / search

Nyakati Tatu Kabla Hujafika Kilele Cha Mafanikio

Muda pekee ambao uanweza kuepuka vikwazo katika maisha yako ni pale ambapo uankuwa haufanyi kitu chochote kile cha maana.Ukioan wakati wowote ule unakabiliwa na changamoto na vikwazo,ni ishara tosha kuwa uko katika kupiga hatua kuelekea mbele.Hakuna mtu ambaye amewahi kufanikiwa bila kukabiliana na vikwazo vya aina fulani akiwa njiani kuelekea kuitimiza ndoto yake.Na ili ujihakikishie kuwa utafika katika kilele cha mafanikio ni lazima uhakikishe kuwa kila wakati uko katika mwendo wa kusonga mbele bila kukata tamaa.Hii ndio maana Mwanaharakati wa haki za watu weusi wa marekani,Martin Luther King Jr aliwahi kusema kuwa-Kama huwezi kuruka basi kimbia,kama hauwezi kukimbia basi tembea,kama hauwezi kutembea basi tambaa-Ila kwa namna yoyote ile fanya kila unachoweza kuelekea katika kuitimiza ndoto yako.

Wakati nafanya utafiti wangu binafsi juu ya maisha ya watu waliofanikiwa katika yale ambayo wamekuwa wanayafanya,niligundua kuwa kuna nyakati za aina tatu ambazo kila mmoja wao aliwahi kuzipitia.Na kwa sababu waliweza kuzishinda basi kila mmoja waoaliibuka kuwa mshindi na kufika kileleni.

Moja ni hali ya kusikia maumivu makali ndani yao wakiwa wameanza kufuatilia na kuishi lile jambo ambalo wanalitamani katika maisha yao.Jambo hili lilielezwa vizuri na kwa ufasaha zaidi na mwanaridha maarufu wa nchini Czech,Emil Zatopek(Alishinda medali tatu za dhahabu katika mashindano ya olimpiki yaliyofanyika Helsinki) ambaye alisema kuwa kinachowatofautisha vijana na watu wazima ni namna wanavyoweza kukabiliana na maumivu na mateso wanayoyapata pale wanapokuwa wameanza safari ya kuelekea katika mafanikio yao.

Katika kuifuatilia ndoto yako na kutimiza malengo yako,utakutana na nyakati za maumivu nyingi sana ambazo kwa ukweli zitakuwa zinakufanya ukose nguvu ya kuamka tena na kuchukua hatua nyingine mbele.Nikiwa shule ya msingi niliwahi wakati fulani kushiriki mbio za mita 200.Wakati bado sijashiriki nilikuwa naona kama ni kitu kirahisi sana na naweza kukifanya bila tatizo lolote.Hata hivyo nilipoanza kukimbia,nilianza kwa mbwembwe na nikatoka spidi kali bila kujua kuwa suala la mbio lina “timing” zake.Nikiwa mita kama hamsini kumaliza nilishangaa kuona kila mtu ananipita kama nimesimama vile,na kila nikijaribu kuongeza kasi naona kama niko palepale,huku misuli ikiuma na kinisikia kama harufu ya damu kifuani.

Nyakati kama hizi huwa zinawatokea watu wengi sana.Unaweza kukuta mtu ameanza kufanya jambo kwa kasi kubwa sana,lakini ghafla anakutana na changamoto zinazomfanya apunguze kabisa kasi ya yale aliyokuwa anayafanya.Unashangaa tu,huoni mtu tena akiendeleza kasi ya kufuatilia ndoto yake.Watu waliofanikiwa huwa wanakiona kipindi hiki kama ndicho muhimu cha kuthibitisha kuwa ndoto yao ni ya uhalisia.Usikubali maumivu yakufanye uache kufuatilia ndoto yako.Kuna msemo wa kiingereza maarufu unasema-“Feel the pain,and do it any way”-Hisi maumivu lakini endelea tu kufanya ulichokusudia.Kumbuka siku zote kuwa maumivu ndio gharama unayoilipa ili kufanikiwa katika yale unayoyatafuta kwenye maisha yako.

Wakati wa pili ni ule ambao mtu anaona kama ni bora akate tamaa kuliko kuendelea.Kama umeshawahi kuangalia mchezo wa ngumi,utagundua kuwa kuna wakati bondia anaweza kupigwa ngumi akaanguka chini,na refa akianza kumuhesabia ukimwangalia bondia machoni utaona ni kama vile anajiuliza niendelee ama nisiendelee.Kila aliyefanikiwa,lazima amepitia katika hali hii,ambapo huwa anafika kiwango anajiuliza swali la kuendelea ama asiendelee.

Katika kufuatilia mafanikio yako na kutimiza malengo ya maisha yako,ni lazima siku moja utajikuta umepitia katika hali kama hii ambayo itakufikisha katika tafakari ya kuendelea ama kuishia njiani.Watu waliofanikiwa,huuita wakati huu kama “Destiny Deciding Moment”-Wakati ambao huamua hatima yako.Inawezekana na wewe uko kwenye wakati huu leo,na umefika hatua uanona kama vile hauna nguvu za kuendelea hatua moja mbele.Ningependa nikukumbushe kuwa ukiweza kuvumilia na kushinda wakati kama huu basi ujue una uwezekano mkubwa sana wa kufanikiwa kufikia kilele cha ndoto yako.

Jambo la muhimu la kukumbuka ni kuwa,kushinda ni utamaduni ambao huwa unatengenezwa kama ambavyo kushindwa kulivyo.Ukijizoeza kuwa mtu ambaye kila changamoto kidogo basi unajikuta umeshakata tamaa na unaacha kuendelea basi kila wakati utakuwa mtu wa kuanza upya kwa kukimbia changamoto.Hebu jiwekee malengo leo ya kuwa utaendelea “kukomaa” hadi mwisho ili upate matokeo unayotaka.Kama njia moja haijafanya kazi basi jaribu njia nyingine,hadi umepata unachotaka.Usikubali kuuishia njiani.

Wakati wa pili ni ule ambao utapoteza marafiki kwenye maisha yako,na wengi wao watakuwa ni wale ambao ulikuwa uanwachukulia kama watu muhimu sana kwenye maisha yako.Kwenye safari ya mafanikio ni lazima ujue kuwa kila hatua itakuwa mtandano mpya na itakuondolewa baadhi ya watu klatika mtandao wako.Kuna watu ambao wakiendelea kuwa sehemu ya maisha yako ya kila siku watakufanya uchelewe kufika unakoenda.

Watu wengi wana mawazo madogo sana katika maisha yao na mara utakapoanza kuwaza mawazo makubwa watashindwa kabisa kuendana na wewe(They will fail to contain your big ideas).Hili ni jambo la kawaida na kila ambaye amefanikiwa katika maisha yake amelipitia.Usishangae kuona aina fulani ya watu wameanza kuwa mbali na wewe na kila ukitafuta sababu hauipati-Siku zote kumbukwa kila kiwango kipya cha maisha yako kitatengeneza watu wapya na kitapunguza wale wa zamani.

Kuna baadhi ya marafiki utaumia sana kuwapoteza,lakini kama vile ambavuyo kila mmoja wetu angependa kuendelea kuishi na wazazi wake hata baada ya kuingia kwenye ndoa-Lakini ili uwe mtu mzima mwenye familia lazima uwaache wazazi wako.Kuwaacha wazazi haimaanishi hauwapendi ila ni kuonyesha kuwa uko kwenye hatua nyingine ya maisha yako.Vivyo hivyo kuna watu utawaacha kwenye maisha yako sio kwa sababu hauwapendi,bali kwa sababu kiwango cha juu ulichoenda wao wameshindwa kubadilisha kiwango chao pia.

Katika kitabu cha TIMIZA MALEONGO YAKO nimeeleza mambo 4 ya muhimu ya kuyafanya kuhusu marafiki wote ulionao ili wasiwe kikwazo cha wewe kutimiza malengo ya maisha yako. Siku zote usikubali mambo haya mawili yakukwamishe.

Kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO kimeelezea mbinu 60 ambazo watu waliofanikiwa wanazitumia kufikia kilele cha mafanikio yao.Unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba 0655 720197 na tutakuelekeza kwa wakala wetu katika mkoa uliopo ama kama uko Dar Es Salaam na unahitaji kuletewa hadi pale ulipo uanweza kuwasiliana nasi kupitia 0712 224282

See You At The Top.

@JoelNanauka

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website