Navigate / search

Nkrumah aliwahi kuuza samaki ili kujikimu

images

Katika safari ya kuelekea kilele cha ndoto yako kuna wakati unaweza kujikuta unafanya jambo la chini sana ukilinganisha na ndoto uliyonayo.Jambo la muhimu la kutambua ni kuwa hapo si mwisho bali ni njia tu,Kwame Nkrumah anatufundisha hilo kupitia maisha yake.

Akiwa marekani alikopata degree yake ya Uchumi,sosholoji na falsafa Kwame alifanya kazi mbalimbali wakati wa likizo ili kujikimu.

Moja ya kazi hizo ilikuwa Ni pamoja na kufanya kazi kiwanda cha sabuni,ndani ya meli na kuuza samaki.

Baadaye alienda uingereza kusoma ambako hata hivyo hakumaliza kwani alishikwa na wimbi la harakati za ukombozi na kujikuta akitumia muda mwingi migahawani kujadili siasa na harakati za ukombozi.

Baadaye ndipo alipoitwa Ghana na kuajiriwa kwenye chama.

USIHITIMISHE HATIMA YAKO KWA PALE ULIPO LEO,USIDHARAU WALIO CHINI LEO—WENGINE NI,MPITO!!

Leave a comment

name*

email* (not published)

website