Navigate / search

Njia Rahisi Ya Kujenga Tabia Unayoitaka Kwenye Maisha Yako

Siku moja mwandishi wa kitabu cha namna 100 za kujihamasisha wewe mwenyewe(100 ways to Motivate yourself),steve Chandler alikuwa anafundisha semina kwa wafanyakazi.ILipofika wakati wa mapumziko mzee mmoja mwenye umri wa miaka 60 akamfuata na kuanza kumueleza changamoto zake.

Mzee Yule akamwambia Steve Chandler-“Mimi nina tatizo kubwa sana la kutokumaliza kila ninachoanza katika maisha yangu.Kuna vitu vingi sana nimekuwa navifanya na naishia njiani na siwezi kumaliza.Naomba unisaidie nifanyaje?”.Steve Chandler aliamua kumuuliza anaamini kama yeye ni mtu anayeweza kumaliza mambo akiamua?Mzee Yule alijibu kuwa,haamini kwa sababu hajawahi kumaliza jambo lolote katika maisha yake na hivyo huwa anajiona yeye ni mtu wa kushidnwa kila wakati na hakuna kitu ambacho anaweza kufanya na kumaliza.

Ushauri ambao alimpa ndio kitu kikubwa ambacho nataka nikufundishe pia leo.Ukweli ni kuwa katika maisha yetu huwa huwa kuna mambo mengi ambayo tumeyachukulia kama udhaifu na yametufanya tusiamini kuwa tunaweza kuishi vinginevyo.Tunaamini hivyo ndivyo tulivyo.Mzee Yule aliamini pengine kuna jambo fulani ambalo akiambiwa mara moja tu litaweza kubadilisha fikira yake na ataanza kuwa mtu ambaye anamaliza mambo kwa haraka bila kuishia njiani tena.

Chandler alimpa zoezi moja-Alimwambia kuwa kila siku awe anajitahidi kumaliza jambo fulani katika maisha yake hata kama ni dogo kiasi gani ila awe analimaliza na kuliandika.Mzee yule aliamua kufanya zoezi lile kwa muda fulani.Kila akifanya kitu na akakimaliza anaandika hata kama ni kidogo kiasi gani.Ikawa kadiri ambavyo anaandika ndivyo kadiri ambavyo alikuwa anatamani kumaliza mambo mengi zaidi.Matokeo yake ilikuwa mzee Yule alikuwa anaanza kujiona ni mtu wa kumaliza.Kadiri alivyokuwa anazidi kufanya zoezi hili ndivyo alivyokuwa anazidi kuwa mtu amabye anamaliza hadi ilipojengeka kuwa ni tabia yake.

Kwa namna rahisi ni kusema kuwa,namna bora ya kujenga tabia yoyote ambayo unaitaka kwenye maisha yako ni kuanza kuifanya na kuiishi tabia hiyo.Hakuna njia rahisi ya kujenga tabia fulani katika maisha yako kama kuanza kuishi kwa tabia hiyo.Umuhimu wa zoezi hili ni kuwa linakusaidia kubadilisha namna unavyojiona na itabadilisha tabia unazokuwa nazo pia.

Kama kuna kitu ambacho unataka kukijenga kwenye maisha yako,njia nzuri ni kuanza kukifanya ili uanze kujiona kuwa ni mtu wa namna hiyo.Usisubiri tabia yoyote ijengeke kwako kwa bahati mbaya,amua kufanya juhudi za makusudi kujenga tabia unayotaka kwa kuanza kufanya kisha baada ya muda utaanza kujiona namna hiyo na itakuwa sehemu ya tabia yako.

See You At The Top

@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website