Navigate / search

Njia nne za kukusaidia kufikia malengo yako kila siku

1573042_full-lnd

Akili zetu zinayumbishwa na kuathiriwa kwa urahisi sana na wakati mwingine inakuwa ni vigumu sana mtu kurudi upya katika malengo yako kwa kazi iliyo mbele yako. Leo tunaonyesha njia kuu nne za kuboresha malengo yako kwa ajili ya kazi iliyo mbele yako na jinsi gani unaweza kujiepusha na mambo yanayoweza kuyumbisha malengo yako. Njia hizi zinategemeana na mtu lakini zina uwezo wa kuleta mabadiliko kwako wewe

Fanya kazi kwa mpangilio

Ni uthibitisho wa kisayansi kwamba akili zetu zinakuwa na umakini sana tunapojielekeza kushughulikia taarifa za kiwango fulani tu na kwa mda fulani uliopangwa. Ugumu unakuja kwenye kuhakikisha kwamba taarifa inayokuja au iliyopo kwenye akili zetu kwa wakati huo inahusiana na kazi iliyo mbele yetu kwa wakati huo. Ili kupunguza mzigo kama huo kwenye akili yako ni vyema kugawa kazi zako katika mpangilio au mgawanyo unaoweza kuusimamia.

Tatizo ni kwamba hatutaki kutumia siku nzima kujielekeza katika jukumu la siku nzima bila kusimama. Kugawanya kazi kutaiwezesha akili yako “kupumua” na baadaye itakupatia kazi nzuri. Fanya kazi kwa mpangilio na katika mpangilio huo unaweza ukapanga muda wa kupata glasi ya maji au kufanya jambo kama sehemu ya mapumziko.

Jipongeze mwenyewe

Sio jambo baya kutembelea mitandao ya kijamii kama vile facebook, whatsapp au twitter kujipatia taarifa za kijamii, lakini ni muhimu sana kutotumia muda mwingi huko hususani pale ambapo kazi yako haijaisha. Ninachoweza kufanya ni kutengeneza mpangilio wa kazi au majukumu ambayo nahitaji kumaliza kabla sijaweza kupitia mtandao wowote wa kijamii na kabla sijatoka kwenye kiti changu cha kazi.

Nitafanya kwa wakati, nitamaliza kazi, kisha nitajipongeza mwenyewe na kupata muda wa kuwasiliana na marafiki. Mbinu hii inaenda na ustahimilivu na nia ya dhati. Kama hautafanikiwa kwenye malengo yako kwa njia hii, jaribu hizi zinazofuata.

Jifanye mjinga

Kama zingine zote zmeshindwa, ukaona haiwezekani kujiepusha na mambo kama facebook na barua pepe zisizoisha za wafanyakazi wenzio, unaweza kujificha. Nenda ujifiche kwenye kwa kutumia mbinu za mitandao ya kijamii, ukionyesha hali (status) yakuwa “una kazi nyingi” au ukaweka “hutaki kusumbuliwa”. Na wale wafanyakazi ambao wenzio ambao wanapenda kuja kwenye kiti chako, weka “simu ya masikioni” wasiweze kuanzisha mjadala na wewe.

Mara nyingi nimekuwa nikijificha ili nisieleweke vibaya na wengine. Inaonekana wakati mtu akianzisha mazungymzo na mimi watu wengine wengi huja. Nimejifunza kuto kujiweka kwenye upande wowote wa majadiliano kwa kujaribu kuwa makini au kuhakikisha kwamba najichunga nunapokuwa kwenye hali kama hizo.

Penda kazi yako

Njia pekee ya kufanya kazi nzuri ni kufurahia kweli na kukipenda kile unachokifanya. Huwa tunaenda umbali mrefu na kufanya kazi bila kuchoka pale tunapopenda kazi tunayoifanya. Lakini tunapoteza malengo na umakini pale ambapo tunapoteza umuhimu na mapenzi ya kile tunachokifanya. Inaweza ikachukua muda kuvutiwa na unachokifanya. Lazima ufikirie kuhusu picha kubwa, na kutilia umakini kufikia matokeo makubwa kama njia pekee ya kubaki katika umuhimu wa unachokifanya.

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website