Navigate / search

Njia Moja Ya Kuongeza Thamani Katika Siku Yako

Siku moja muhudumu wa mgahawa wa AppleBees ulioko Texax Kasseys Simons,alikuwa amepitia kwenye Supermarlek kufanya manunuzi kaba hajaingia katika zamu yake kazini.Wakati akiwa kwenye mstari akashangaa kumuona mwanamama mbele ya mstari akiwa analia.Akiwa ananona ndio njia nzuri ya kuweza kumfariji,aliamua kumlipia kaisi cha dola 17 za bidhaa ambazo alikuwa amenunua lakini pia alimpa mawasiliano yake na kisha alimkaribisha katika mgahawa aliokuwa anafanyia kazi kama angependa kupata kahawa pamoja naye.
Siku ya pili akiwa kazini,mtu mmoja alikuja na kuagiza maji ya dola 37,baada ya kunywa akamwachia tip ya sola 500.Akiwa bado anaendelea kushangaa akagundua kuwa kweye “tissue”(napkin) iliyokuwa pale mezani ilikuwa imeandikwa maneno fulani.Alipoichukua alikutwa imeandikwa “Kwa niaba ya familia ya sulivvan,ningependa kukushukuru sana kwa kwa jinsi ulivyo mwema.Moja kati ya siku ambayo ilikuwa mbaya sana kwa mama yangu,alipokuwa anakumbuka miaka 3 ya kifoc cha baba yangu ulifanya kitendo kilichomfariji sana.Tangu wakati huo alikuwa mtu mwenye furaha sana.Ahsante sana.”

 

Kila siku kwenye maisha huwa tunakutana na watu mbalimbali na wengine huwa ni watu ambao wanaonekana wenye huzuni sana na ni kama vile wamekosa matumaini.Wengine ambao tunakutana nao watakuwa ni watu ambao wanaonekana hawana msaada kwetu na kila wakati tutajaribiwa sana kuwadharau na kuwaona hawana maana kabisa.Hata hivyo,kila siku kumbuka kuwa,kila mtu ana umuhimu wake.
Kati ya mambo muhimu sana ya kujifunza katika maisha yako ni kuhakikisha kuwa haumdharau mtu kwa sababu ya vile anavyoonekana leo,muheshimu kwa vile ambavyo anaweza kuwa kesho.Kila mtu ana kitu kikubwa ndani yake,usipumbazwe nay ale unayoyaona nje kwa sasa.
Kila mtu unayekutana naye amebeba fursa yako ya kesho.Kuna watu leo unaweza ukawaona hawana maana kabisa kwenye maisha yako,ila kesho Mungu atawatumia kukuvusha hatua inayofuata katika maisha yako.Leo nataka ujifunze kuthamini kila ambaye unakutana naye kwenye maisha.
Kwa upande mwingine,kuna watu ambao neno lako moja ama kitendo chako kimoja cha upendo na kutia moyo kinaweza kuokoa maisha yao.Kuna watu ambao wlo wanasubiri uwaambie tu unaweza na watachukua hatua muhimu kwenye maisha yao,kuna watu ambao wanasubiri tu leo uwaambie kuwa wao ni wathammani na wataanza kujiamini kufanya ndoto kubwa,kuna watu wanasubiri uwaambie watainuka tena na wataghairisha wazo la kujinyonga n.k
Maneno yako ya kutia moyo na vitendo vyako vya kuonyesha kuwa unamthamini mtu ni vya maana sana kwa leo.Kwanza vitatumika kama njia ya kuweza kukusaidia kufungua fursa nyingine na pia uanweza kutuimika kuwasaidia watu wengine.
See You At The Top
@JoenNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website