Navigate / search

Njia 5 za Kutumia ili Kupata Wazo La Biashara Litakalokufanikisha

a businessman relaxing in the chair of his office with his hands behind his head

Habari za wakati huu,ningependa kuanza na msemo toka wa swami vibekananda aliyenena “Take up one idea. Make that one idea your life. Think of it, dream of it, live on that idea. Let the brain, muscles, nerves, every part of your body, be full of that idea, and just leave every other idea alone. This is the way to success. That is way great spiritual giants are produced.”Akimaanisha kama utaamua kuchukua idea/wazo moja na kuliwaza,kulitafakari na kuwa ndio kitu cha muhimu kwako,basi mwisho wa siku utafanikiwa.Kwa ufupi ni kuwa kila mtu mkubwa duniani alianza na wazo fulani lililomfanikisha.

Kiufupi ni kuwa yeyote ambaye huwa ana Mawazo ya tofauti na yaliyotangulia kuliko wengine huwa anakuwa wa tofauti na atajikuta anapiga hatua kuliko wengine katika field yake.Aidha uwe umeajiriwa,umejiajiri,mfanyabiashara, mwanasiasa ama mwanafunzi ;uwezo wako wa kuja na mawazo ya tofauti ndio kiini na chanzo cha mafanikio yako.

Njia hizo ni:

1)Tafuta Uhitaji/Tatizo(Identify a need)

Kila mafanikio ni matokeo ya Uhitaji wa watu.Kila unacholipia pesa,kwako ni UHITAJI na kwa unayempa pesa ni kuwa AMETATUA TATIZO lako.
Kwa maneno mengine Kadiri unavyoweza kutatua matatizo MAKUBWA na MENGI ndivyo unavyopata vyanzo vya pesa zaidi. Kwa ufupi umaskini ni matokeo ya Kukimbia kutatua matatizo na utajiri ni matokeo ya kukimbilia Kutatua matatizo.

Leo ningependa tuangalie njia kadhaa za namna ya kupata mawazo Yanayoweza kuwa chanzo cha kubadilisha maisha yako unapoamua kuyafanyia kazi.

Na hapa ningependa kuwakumbusha maneno ya William J. Cameron aliyesema “Money never starts an idea; it is the idea that starts the money”
Fedha haileti mawazo ila mawazo ndio huleta pesa, ndio maana kuna watu walishawahi kupata pesa nyingi ila kwa Kukosa mawazo wamerudi katika kufeli na umaskini.

Hebu chukua dakika Moja jiulize:Katika mazingira niliyopo je,kuna Uhitaji gani ninaoweza kuutatua? chukua notebook yako na aandika kabla hatujaendelea.
Hivyo basi angalia mazingira yanayokuzunguka,je kuna Uhitaji gani?Kama maji yanatoka mara moja kwa wiki mtaani Kwenu ukifanikiwa kununua simtank kadhaa na kuuza maji siku ambazo hayatoki hapo unakuwa umetatua tatizo na umepata pesa.Kama umegundua watu karibu na maeneo ya Kwenu wanatumia gesi na hakuna duka la karibu tafuta namna ya kuwa wakala wa kuuza,kadhalika na mahitaji mengine eneo ulilopo.

Naamini umepata mawazo kadhaa.Tutaendelea kujifunza kisha utabaki na wazo moja.Njia ya pili ni ipi????

2)Boresha wazo la mwingine(Adapt and Improve somebody’s else idea)

Kuna wakati mwingine hautahitaji kuanza na Wazo jipya kabisa,badala yake utahitaji kuchukua wazo la mwingine kuliboresha.Kwa mfano badala ya mtu kuuza matunda na kutamenya mtu anaponunua mwingine akaboresha akaamua kuyamenya kabisa kisha anayapark vizuri tayari kwa kuyauza.
Chunguza kile ambacho kinafanywa na wengine kisha jiulize,hivi nawezaje kuliboresha wazo hili?

3)Hamisha wazo la wengine na lipe uhalisia wa mazingira yako(import and contextualise)

Kuna mawazo mengi yaliyofanikiwa leo ni matokeo ya mawazo yaliyohamishwa toka mahali pengine na yakapewa uhalisia wa mahali husika. XFactor ya UK imezaa Bongo Star Search,DECA na SONY records label ndio leo tunaona WCB labels,fast jet ni matokeo ya easy jet ya Marekani n.k
Jaribu kuangalia Kuna wazo gani ambalo unaweza kuliimport na ukaliwekea mazingira ya kwako na ukalifanyia kazi.Unaweza kulitoa nje ya Tanzania na ukalileta Tanzania ama ukalitoa dar na ukalipeleka katika mko unaoishi.

4)Rahisisha mchakato wa kitu ama bidhaa fulani.

Sasa hivi kila Mtu anajitahidi kutumia teknolojia Kuuza bidhaa ama kutoa huduma?kwa nini?kwa sababu ya kurahisisha mchakato kwa wateja.Tunaishi katika ulimwengu ambao watu hupenda kutumia muda mfupi kupata huduma ama bidhaa, hivyo unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa hata kama unatoa bidhaa/huduma ileile kama wengine jaribu kurahisisha.
Ndio maana ving’amuzi wanaweka huduma zao Kwenye MPESA,tigopesa, airtel n.k wanachojaribu kufanya ni kurahisisha.

Nguvu ya biashara ya maxmalipo sio kutoa huduma mpya bali KURAHISIHA Utoaji wa huduma.

Ni rahisi kwa mama ntilie anayepeleka chakula maofisini na akaongeza gharama ya usafiri juu ya 500 kwa kila sahani kuliko auze bei ya chini huku akisubiri watu wamfuate kilometa moja kule anakouza.
Inawezekana unataka kufanya kitu ambacho kila mtu anafanya, swali ni je unaweza kutoa Urahisi gani utakaovutia wanunuaji wa huduma/bidhaa yako?

5)Tengeneza Uhitaji(Create a Need)

Hii si njia Rahisi sana ila inawezekana. Inaamisha kuna vitu vingi watu wanahitaji ila hawawezi kuvitumia hadi viwepo.

Kabla soda hazijaja watu walikuwa wanakunywa maji,kabla TV hazipo watu walikuwa ni radio tu na hakuna mtu alikuwa anadai TV kwa kuwa haikuwepo. Lakini leo ni kama vile haiwezekani kuishi bila TV.Kuna mtu siku moja akauliza “Hivi wazee wa zamani waliishije bila simu?appointments walifanyaje wakifika kariakoo na kila mtu yuko kona yake”

Hii ina maana kuna mahitaji mengi bado yako ila watu hawawezi kuyadai au Kuulizia hadi yatakapokuwepo.Zamani scrub hazikuwepo ukienda saloon,lakini siku hizi ni kama vile ni Ulazima kila ukinyoa utajikuta unataka kufanya na scrub tena ina bei kubwa kuliko hata kunyoa kwenyewe?
Hiyo inamaanisha kuna wazo unaweza ukaja nalo watu wakaanza kuhitaji hata kama hawajawahi kujua kama wanahitaji.

HITIMISHO:

Mawazo yako kila mahali, kiwango chako cha kujitoa kuyatafuta na kuyafanyia kazi ndio kitu muhimu zaidi.

Kumbuka;kiwango Chako cha kutengeneza mawazo mengi na Kuyafanyia Kazi ndio kitategemea utafanikiwa kwa kiwango gani katika maisha yako.
Ningeshauri:Anza kuwa na IDEA PAD-Notebook ambayo utakuwa unaandika mawazo yako ama fungua faili maalumu Kwenye computer yako.Isipite wiki bila kuwa na muda wa wewe kutulia na kupitia mawazo yako.Kadiri unavyoyapitia utagundua yapi yanafaa na yapi hayafai.
Naomba Kuwasilisha.

Endelea Kutembelea www.JoelNanauka.com Kujifunza Zaidi.

See You At The Top.

Comments

David
Reply

thanks much for your starting businesses ideae

Emmanuel Timothy
Reply

Am so blessed, nainuliwa kifikra najengeka mnoo! barikiwa sana kaka

Stella Komu
Reply

Mungu akubariki kaka…yani nimepata kitu…nitafanyia kazi nije nikupe feedback

Leave a comment

name*

email* (not published)

website