Navigate / search

Njia 3 Za Kukufanya Uibuke Mshindi Kwenye Kila Changamoto

MANCHESTER, UNITED KINGDOM - MARCH 14: Bradley Pryce lies on the canvas after being defeated by Matthew Hall during the Commonwealth Light Middleweight Championship fight between Bradley Pryce of Wales and Matthew Hall of England at the MEN Arena on March 14, 2009 in Manchester, England. (Photo by Alex Livesey/Getty Images)

Watu wengi sana wamefanya utafiti namna hamasa(motivation) zinavyoweza kumsaidia mtu kufikia malengo yake Kwenye maisha.Ila hakuna ambaye aliyewahi kufanya utafiti kuhusianisha kushindwa kwa mtu na mafanikio yake. Hii ndio maana Dr.Abraham zaleznik wa chuo kikuu cha Harvard aliamua kufanya utafiti huo ili kugundua kama kuna uhusiano wowote katika ya kushindwa Kwenye maisha na mafanikio ya mtu.

Utafiti wa Dr.Abraham uligundua kuna mambo makubwa matatu yanayochangia kuleta tofauti kupitia kushindwa kati ya watu wanaofanikiwa na wale waliofanikiwa. kwa maana nyingine ni kuwa kile wanachofanya watu kipindi wanapokutana na wakati mgumu au kufeli kwao ndicho huwatofautisha kati ya wanaofanikiwa na waliofanikiwa:

1)Wanaofanikiwa wameshaamua kila wakifeli wataanza upya.

Kila aliyefanikiwa alishawahi kufanya uamuzi kuwa hakuna Kitu kinachoweza kumzuia kuifikia ndoto yake.Wasio fanikiwa hawajawahi kufanya uamuzi huu.Ndio maana watu wawili wanaweza kufeli katika jambo moja lakini mwingine akaamka na kuanza tena haraka, mwingine anashindwa kuendelea ama inamchukua muda sana sana.

2)Wanaofanikiwa hutafuta walichojifunza,wanaofeli hutafuta nani wa kumlaumu.

Watu wanaofanikiwa ni Wale ambao kila wakifeli katika jambo hukaa chini na kujiuliza, hivi hapa najifunza jambo gani?wakishapata somo Lao hulitumia ili wasifeli tena.Ila watu ambao huwa wanaofeli maishani ni wale ambao kila wakishindwa jambo kazi yao kubwa ni kumtafuta mtu wa kumlaumu kwa kufeli kwao.

3)Wanaofaulu hupata muda wa kutafakari kutumia akili,wanaofeli hutumia hisia kukabiliana na mambo.

Watu wanaofikia katika vilele vya ndoto zao ni wale ambao hupata muda wa kuchambua chanzo cha tatizo na kutafuta njia za kutatua,lakini wale wanaoshindwa kufikia Hatima zao ni wale ambao kila kitu kibaya kinapotokea hutumia hisia kukabiliana nacho(Hasira,kulia,kutukana, kupiga kelele etc)

Ili ufanikiwe kufikia ndoto yako hakikisha leo unakabiliana na changamoto zako kwa kufuata watu waliofanikiwa.

Endelea Kutembelea ukurasa wa facebook ili kujifunza Zaidi.

Ndoto Yako Inawezekana,

See You At The Top.

Comments

Gerald
Reply

Ni kweli bro.. Napenda mafunzo yako.. Naiman nitatimiz ndoto zang

Prince
Reply

Be blessed pastor

Leave a comment

name*

email* (not published)

website