Navigate / search

Njia 3 za kubadili kushindwa kwako kuwe Ushindi

images

Umewahi kujiuliza kwa nini watu wanaweza kupitia changamoto zinazofanana katika maisha mmoja akazitatua na mwingine akashindwa. Tafsiri au maana ya kufeli ndiyo inayoamua nini utafanya baadaye. Watu waliofanikiwa hukabiliana na kushindwa ama kufeli kwa mtazamo ufuatao;

1) Fursa ya kujifunza njia ambazo haziwezi kukuletea matokeo unayotaka.

Wakati mwingine kama vitu havifanikiwi tambua hujafeli, bali ni njia uliyotumia ndio iliyofeli. Kwa hiyo ukibadilisha njia, uko tayari kwa ushindi.

2)Hawatafuti mtu wa kumlaumu

Wakati mwingi unapolaumu watu, unakuwa umepoteza uwezo wa kutatua matatizo. watu waliofanikiwa wanachukua jukumu la kujifunza katika kushindwa kwao na kuanza kupambana tena na changamoto.

3)Wanatazama kipi kinaweza kufanyika na sio kilichofanyika na kushindwa.

Mungu kakuwekea macho mbele kama alama ili kama utatazama mbele na utazame. Jifunze kutokana na yaliyopita kwa kutazamia yajayo. Achana na maumivu na kushindwa kulikopita bali tazama mbele. Habari njema ni kwamba kuna nyakati nzuri mbele yako kama utachagua kuendelea.

Kumbuka;

Ninaamini katika ndoto yako,
Ninaamini katika uwezo wako,
Ninaamini katika kesho yako,

Mafanikio Yanakuita

Joel Arthur Nanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website