Navigate / search

Njia 2 Za Kutumia Kupanda Cheo kwa Haraka

Mafanikio yako katika kazi unayofanya sio jambo linalotokea kwa bahati tu.Kupanda kwako cheo ama kuongezwa mshahara ni matokeo ya kufanya mambo fulani katika maisha yako ambayo watu wengine wa kawaida huwa hawayafanyi kabisa.Kitu ambachi unatakiwa kujua ni kuwa siku hizi muda wa kukaa kazini sio kigezo cha kukusaidia kufanikiwa kupanda cheo ama kuongezwa mshahara wako kazini.Badala yako kuna mambo ambayo ukiyfanya yatakusaidia sana kutokan hapo ulipo na kupanda ngazi katika taaluma yako kwa kasi sana.
Hivi umeshawahi kujiuliza kuwa inakuwaje watu ambao wanaanza kazin siku moja na wako katika mazingira ya kufanana lakini kuna mmoja anapanda juu kwa kasi kuliko mwingine-Tofauti ni nini?Umeshawahi kushangaa kuna watu wana elimu kama wewe lakini wana vyeo na mishahara mikubwa?Au imeshawahi kukutokea kuwa mtu amekuja nyuma yako na ghafla anapanda cheo kwa haraka na anaanza kupata pesa nyingi kuliko wewe?
Leo ningependa nikufundishe mambo mawili muhimu ambazo zitakusaidia kupanda cheo kwa haraka na pia kuongezwa mshahara kwa kasi:
Moja ni kuongeza thamani yako.Siku zote kumbuka kuwa pesa unayolipwa ni sawasawa na thamani ambayo mwajiri wako ameiweka kwako.Hii inamaanisha wewe ni kama bidhaa ambayo mtu anaiwekea thamani fulani ya kuilipa.Maana yake ni kuwa kama ambavyo wewe huwa unaweka thamani fulanin katika kila bidhaa unayonunua ndivyo ambavyo mwajiri wako anaweka thamani kwako na anakulipa kwa njia ya mshahara.Sasa kitu ambacho unatakiwa ujiulize kwa sasa ni kuwa-Tangu ulipoanza kazi na mshahara wa kwanza kulipwa na nafasi uliyopewa kuna uthamani gani umeshauongeza kwenye maisha yako?Ukigundua kuwa hakuna kitu chochote ambacho umewahi kukifanya cha kukuongezea thamani kwenye maisha yako,inamaanisha bado haujajenga uhalali wa kuongezewa mshahara ama kupandishwa cheo.Kabla haujatamani kuongezwa mshahara ama kupandishwa cheo tamani kwan kuongeza thamani yako.
Kuna watu ambao tangu wameajiriwa siku ya kwanza hawajaongeza thamani yoyote katika maisha yao,lakini kila wakati huwa wanalalamika kuhusu kutoongezwa mshahara ama kupandishwa cheo.Hawajawahi kusoma kozi yoyote ya ziada,hawajawahi kujisomea kitu chochote kile kinachohusiana na taaluma yao.
Jambo la pili unalohitaji la muhimu ni kuwa na kitu kinaitwa “High level of dependability” kwenye kile unachokifanya.Hii inamaanisha kuwa unakuwa ni mtu ambaye kila mtu anajua hapo ofisini kwako kuwa akitaka kazi yoyote ilie ifanyike kwa ufanisi tena kwa haraka basi wewe ndiye mtu sahihi wa kufanya.Njia nzuri ya kutengeneza kiwango cha juu cha kuwa mtu ambaye unategemewa ni kila wakati kufanya kazi yako na kumaliza kabla ya muda uliotarajiwa(deadline).
Moja ya kitu ambacho kila bosi anakitamani ni kuwa na mtu ambaye akimwachia kazi,kwanza hatahitaji kumsimamia wala kumfuatilia ili kumfanya akamilishe kazi yake.Lakini pili ni kuwa ni kuhakikisha kuwa kila kazi unayopewa unaifanya kwa ubora kiwango ambacho bosi wako wa juu hatahitaji kuirekebisha kwa mambo mengi.Kadiri unavyokuwa mtu ambaye unafanya kazi yako kwa ubora wa hali ya juu na kwa haraka kama inavyotakiwa,ndivyo ambavyo kila mtu huwa anawaza kukupa nafasi kubwa na ya juu zaidi.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website