Navigate / search

Njia 2 Za Kuhakikisha Hakuna Anayekuzuia Kutimiza Ndoto Zako

1

Jeff Nelson katika kitabu chake cha “The Slight edge” anasema kuwa maisha yetu(kifedha,kiwango cha furaha,idadi ya furs tunzopata etc) ni wastani wa maisha ya watu 6 wanaotuzunguka kila wakati,watu wa karibu yetu.Hii inamaanisha hatima yetu inategemea sana tunaambatana na watu wa namna gani(Our destination is determined by our association).Maana yake ni kuwa mafanikio yetu katika maeneo mbalimbali yanachangiwa na watu tulioamua kuwaweka karibu katika maisha yetu ya kila siku.

Ili kuweza kufanikiwa ni lazima kujua njia mojawapo ya kubadilisha hali yako ya sasa ni lazima pia ubadilishe vipaumbele vyako vya unaoambatana nao(physically,vitabu vyao au unaowaangalia kwa TV,Movie au kwenye mitandao ya jamii).(Before you change your position,you will first need to change your association).Kumbuka wanaokuzunguka ndio wanaojulisha wewe utakuwa unapata taarifa gani,aidha za kukusaidia au kutwa kuchwa mnaongelea watu wengine na mambo yasiyochangia katika kuelekea ndoto yako.

Maisha ya watu waliofanikiwa huwa yanaongozwa na vipaumbele vifuatavyo inapofika suala la watu wa kuambatana nao:

1)Wanakaa mbali na watu ambao wako Negative kila wakati.

Kuna watu ambao huwa hawawezi kuona kitu chema katika maisha ya mtu mwingine,kila wakati wanaona mabaya.Ni watu ambao hawawezi kukutia moyo katika uwezo ulio nao, ila wako pale kukukatisha tama.Kila unapokuja na wazo jipya Watakuambia hilo haliwezekani, ama siku ukishindwa ni kama vile walikuwa wanasubiri,watakuwa wa kwanza kukukambia”Nilijua tu utafeli,utashidnwa”.

Watu wa namna hii ni hatari sana kwani huvunja ile hali ya kujiamini kwako na hukufanya uone kuwa hautaweza tena kufanikiwa katika maisha yako.
Hebu kagua maisha yako leo?Je kuna watu ambao uko nao karibu ni ni watu wenye sifa hizo?Kama wapo,waambie wabadilike lakini ikishindikana punguza ukaribu nao kwani maneno yao yanaweza kukufanya ushindwe kabisa kufikia ndoto yako.

2)Waliofanikiawa Wanachagua kimkakati watu wa kuwa na urafiki nao mitandaoni

Miaka miwili iliyopita nilifanya utafiti mdogo kuona watanzania wengi wamelike page gani katika mtandao wa facebook.Nilishangazwa sana kuona kuwa watanzania wengi walikuwa wamelike Zaidi page za udaku,pombe na vichekesho.Wachache sana walikuwa wamelike page zenye kutoa mafunzo ya kuwasaidia kujenga uwezo wao ama kupata ushauri wa kimaisha.

Ni hatari kukuta mtu anaamka asubuhi na kitu cha kwanza kufanya ni kuanza kuangalia skendo mpya zasiku hiyo,burudani na hata mitandao ya utupu.Katika dunia ya leo,mitandao huwa ni sehemu ya association yetu.
Kuanzia leo kagua magroup ya watasaap uliyojiunga,Jiulize-Hivi kila group nililopo lina msaada kwangu au linanipotezea muda?Hivi ninapoamka asubuhi natakiwa kuangalia page gani za facebook au kusoma vitu vya aina gani kujijenga kwa ajili ya mafanikio ya siku hiyo?

Kama utagundua kuna pages,watsaap groups au kuna watu una urafiki nao katika mitandao wasio na faida,usione Haya.JIONDOE MARA MOJA.
Je,Unataka kuifikia ndoto yako?:ZINGATIA UNAAMBATANA NA WATU WA NAMNA GANI PHISICALLY NA MITANDAONI PIA.

Endelea kutembelea tovuti hii na Ukurasa wawngu wa Facebook ujifunze Zaidi.

SEE YOU AT THE TOP.

Comments

JAPHETH LUTTASHOBYA
Reply

i like it pastor joel,,,,,,,,,,,,,,,,

Leave a comment

name*

email* (not published)

website