Navigate / search

Namna Gesi na Mafuta vinavyoweza Kuisaidia Tanzania.

Mideast-Israel-Natrua_Horo
Ni 15% tu ya pesa ndio ilitumika katika matumizi ya serikali,5% ilipelekwa mafuta yanakozalishwa na 10% ilitunzwa kwa kizazi kijacho

Katika kwendelezo wa kujifunza kuhusu Rasilimali gesi na mafuta ili viweze kutusaidia nchini Tanzania,leo nakushirikisha sehemu ya pili ya yale niliyojifunza katika kitabu cha Africa’s Oil(Power,Pipelines and Future Fortunes).

Mwaka 1990 Benki ya Dunia na serikali ya CHAD ilifikia makubaliano ya kuanzisha mradi wa CCDP(Chad-Cameroon Development Project) mradi wa uchimbaji na usafirishaji wa mafuta kupitia bomba maalumu ambao gharama ya kuanzisha hadi kuukamilisha ilikuwa ni dola bilioni 4.2

Makubaliano yalikuwa ni kwa ExxonMobil ambayo kwa Chad ilikuwa inajulikana kama Esso kwa CHAD na Retronas&Chevron wangelipa gharama yote ya kuendeleza vitalu vya mafuta na pia gharama ya 1/3 ya ujenzi wa bomba.

Kwa upande wa Benki ya Dunia ilikubali kutoa Mkopo wa dola milioni 300 kupitia International Bank for reconstruction and Development na International Finance Corporation(IFC) na pesa iliyobaki makubaliano yalikuwa ikopwe kutoka katika vyanzo vingine vya taasisi za fedha na benki mbalimbali.

Baada ya kukamilika kwa mradi huu CHAD ilikadiriwa kuingiza kiasi cha dola bilioni 2 kuanzia uchimbaji hadi mafuta yatakapoisha mwaka 2030.Mradi wa aina hii ulikuwa haujawahi kufanyika mahali popote duniani hivyo ilibidi kuundwa kwa bodi ya Ushauri ya Kimataifa(International Advisory Board) na hasa kutokana na presha ya nchi za ulaya ambazo ndio wadau wakubwa wa benki ya dunia.Bodi hii ililenga kuhakikisha ripoti ya maendeleo ya mradi inatolewa na sauti za wananchi wa CHAD zinasikilizwa ili waweze kunufaika na rasilimali zao.

Ili kuhakikisha mradi huu unakuwa na faida zitakazobadilisha Maisha ya wananchi wa Chad Makubaliano yafuatayo yalifikiwa:

1)Mambo yahusuyo Mgawanyo wa Mapato na Sheria Za Usimamizi.

a. Iundwe sheria mpya ya kusimamia mapato yatokanayo na mafuta(Revenue Management) na sharia hii iliyokuwa kwa jina maarufu la Law 001 ilipitishwa mwaka 1998 kwa kura zote za wabunge baad aya masaa 3 ya majadiliano makali.Hapa tuna jambo la kujifunza kama Tanzania,je tunayo sheria maalumu inayotarajia kusimamia mapato yetu yatakayotokana na mafuta na Gesi?Hapa kwetu malalamiko yalitolewa kuwa mikataba ilitolewa hata kabla sera ya gesi na mafuta haijapitishwa

b. Ilikubaliwa kuwa pesa zote zitakazokusanywa ziwekwe kwenye akaunti maalumu nchini UIngereza(account ya Escrow) na ili kutoa ni lazima ikubaliwe kwa kupitishw ana kamati maalumu iliyokuwa imeundwa kwa kujumlisha viongozi wa serikali na mashirika binafsi(NGO’s).

c. Katika pesa itakyotumika 10% ilitakiwa iwekwe kwenye mfuko maalumu wa kizazi kijacho(Future Generation Fund) na haikutakiwa kuguswa na mtu yeyote yule.

d. Kwa 905 iliyobakia,matumizi yake yalikuwa yanatakiwa kufanyika kama ifuatavyo:

 80% iwekezwe kwenye sekta maalumu amabazo zilichaguliwa ikiwemo(Elimu,Afya,Maendeleo vijijini,Mazingira na miundombinu)
 5% iende kwenye mji ambao ndiko uzalishaji uanfanyika(Kama kwa gesi hapa ingekuwa ni Mtwara).Hii ni kutokana na ukweli kuwa athari nyingi za kimazingira na kadhalikazinawakumba wao na sio watu wengine wa maeneo mengine.

 15% iliyobakia ilitakiwa ndio itumike serikalini kwa ajili ya matumizi mengine ya kuendesha serikali.
Ili kuhakikisha kuwa makubaliano haya yanasimamiwa na kutekelezwa chombo maalumu kikaundwa(College de contiole et de surveillance des resources petrolieres-CCSRP-Petroleum Revenue Oversight and Control Committee).Chombo hiki kiliundwa kwa pamoja na serikali na mashirika ya jamii.

Mambo makubwa mawili tunayojifunza hapa ni (1)kuwa lazima kuwa na mpango maalumu wa namna ya kutumia pesa zitazotokana na mafuta na gesi,la sivyo hatutaziona(2)Ni muhimu kuwa na chombo maalumu cha kusimamia makubaliano hayo na kiwe kimehusisha na watu wengine,kuiachia serikali peke yake kutekeleza.
Ukiacha makubaliano haya yalikuwepo mengine kwenye mazingira ili kuzuia athari ambazo ziliwahi kutokea nchini Nigeria eneo la Niger Delta ambapo ardhi ilishindwa kutumika tena kwa kilimo na uvuvi.Tukutane wakati ujao ili kuangalia vipengele muhimu vya makubaliano na changamoto ambazo walikabiliana nazo katika utekelezaji.

Joel Nanauka
jnanauka@gmail.com

Leave a comment

name*

email* (not published)

website