Navigate / search

Muhtasari wa Kitabu : CASHFLOW QUADRANT cha Robert Kiyosaki

rich-dad-cashflow-quadrant

Katika kitabu cha Robert Kiyosaki, anapozungumzia kipengele cha fedha, mtunzi anaelezea kwamba kuna aina nne za wafanyakazi, ambao ni WAAJIRIWA! WALIOJIAJIRI! WAMILIKI WA BIASHARA! na WAWEKEZAJI. Kiyosaki anatutaarifu pia, kuna ngazi saba za wawekezaji na kumalizia kutuelezea hatua saba za mafanikio ya kifedha.

Kuna aina nne za wafanyakazi, WAAJIRIWA! WALIOJIAJIRI! WAMILIKI WA BIASHARA na WAWEKEZAJI! Waajiriwa wanaamini kwamba “hawaridhiki na hali ya sintofahamu kuhusu maisha yao ya baadaye” ( Nukuu, ukurasa wa 21, Kiyosaki, Kipengele cha fedha). Matokeo yake waajiriwa wanaona ni bora zaidi kwao kuwa na kazi salama kuliko kupoteza nafasi ya kutajirika kwa haraka.

WAAJIRIWA wanalipwa kidogo sana huku wakitozwa kodi kubwa. Mtu mmoja anafanya kazi kama mtunza fedha, katika kampuni ya Vons, ni muajiriwa. Huwa anaamka asubuhi na kwenda kazini na kufanya kazi kutwa nzima kila siku. Ni mtu anayefanya kazi kwa bidii japokuwa anamtajirisha bosi wake tu.

WALIOJIAJIRI ni watu ambao wanamiliki biashara zao.“Waliojiajiri mara zote ni watu waliojitoa kikamilifu” ( Nukuu, ukurasa wa 22, Roboduara nne za Mzungunguko wa Fedha) Ni watu ambao wanamiliki biashara ndogo kama saluni au maduka ya wastani. Ni kweli kwamba watu waliojiajiri ni mabosi, lakini ni mabosi hata kwao wenyewe. Tatizo ni kwamba wanasimamia wenyewe biashara zao,kodi na hata mambo mengine yanayohusu biashara. Matokeo yake watu wengi waliojiajiri wanaelemewa na kuacha biashara ndani ya miaka mitano.

WAMILIKI WA BIASHARA! Hawa ni tofauti na waliojiajiri. Wakati aliyejiajiri lazima awepo kazini kundi hili la wamiliki wa biashara“wanapenda kugawa madaraka” (Nukuu, ukurasa wa 23, kipengele cha fedha, Kiyosaki) Kwa maneno mengine huwa hawapo kazini. Badala yake, anawaajiri watu wengine kusimamia biashara yake. Tunapoenda kwa Mac Donalds ni vigumu kumuona mmiliki. Tunapokuwa na tatizo, tunaweza tu kulisuluhuisha na msimamizi sio mmiliki.

“WAWEKEZAJI! wanatengeneza pesa kwa kutumia pesa” (Nukuu, Kiyosaki, ukurasa wa 29, Roboduara nne za Mzungunguko wa Fedha). Ninaye rafiki yangu ambaye alichukua kiasi cha fedha, dola za kimarekani elfu ishirini ($20,000) kama mkopo, badala ya kununua gari jipya, aliwekeza tena fedha ile kwenye amana yenye kurudisha maslahi makubwa. Ndani ya mwaka mmoja, alilipa madeni yake yote na sasa anaingiza kipato cha dola za kimarekani elfu sita ($6,000) kila mwezi kutoka kwenye zile dola za kimarekani elfu ishirini ($20,000). Kwa maneno mengine hajawahi kufanya kazi apate pesa, lakini hela yake rafiki yangu, inafanya kazi kuleta pesa. Hata kama yeye anaamua kucheza mpira wa gofu au pool table siku nzima. Mwandishi anasema kwamba kila mtu ameridhika na kipengele chake. Kiyosaki anashauri WAMILIKI WA BIASHARA na WAWEKEZAJI ndio ambao wana uhuru wa muda wao na fedha.

KUNA AINA SABA ZA WAWEKEZAJI.
Aina ya kwanza: Wale wasio na kitu cha kuwekeza. Ni watu ambao wanapata fedha na kuzitumia zote kwa kununua magari na vitu vingine vya kifahari.

Aina ya pili: Wakopaji. Ni watu ambao kila siku wanasema “niazime”. Wanapenda kupokea. Las Vegas, Marekani, ni mahali ambapo kuna wakopaji, watu wenye mali bila pesa. Mwisho wa siku mikopo inakuwa mingi wanajikuta wakosa hata mahali pa kuishi.

Aina ya tatu: Wawekezaji. Wakati wawekezaji ni zaidi ya wakopaji. Na wao pia hawajui kama hela yao inashuka thamani kutokana na mfumuko wa bei. Mfumuko wa bei mara nyingi unafikia asilimia nne (4%) kila mwaka. Kwa bahati mbaya akaunti nyingi za watu waliohifadhi fedha benki, zinalipa asilimia mbili (2%) kwa mwaka. Tufanyeje? Suluhisho! Wekeza kwenye biashara ya hisa, dhamana au mifuko ya fedha ya pamoja(Mutual Funds).

Aina ya nne: Wawekezaji bora. Ni watu wa tabaka la kati, ambao wana mipango ya baadaye kama vile bima, pensheni na mafao ya uzeeni. Wanapostaafu “wawekezaji bora” wanaamini serikali itawalipa mafao yao. Leo kitu hiki hakiwezekani. Kadiri gharama za wazee zinavyoshuka, bima za afya za wazee zinapanda kwa kasi sana. Ni vizuri kuwa na hisa na dhamana nyingi za kuwasaidia.

Aina ya tano: Uwekezaji wa muda mrefu. Watu hawa wana mipango mikubwa wanayoifuata. Wameweka fedha zao kwa ajili ya hisa, dhamana na uwekezaji unaodumu. Ngazi hii ya tano ni ngazi ya mabadiliko kwa watu wengi. Katika ngazi hii watu wanaanza kugundua tofauti iliyopo kati ya kufanya kazi upate pesa na kuwa na pesa inayoleta pesa. Kusoma vitabu na kusikiliza audio zinazohusu uwekezaji ni njia muhimu kama unataka kuingia uwekezaji wa muda mrefu.

Aina ya sita: Wawekezaji wa kisasa. Wawekezaji hawa wanaenda kwa kasi sana. Wana ujasiri wa kuthubutu kufanya mambo makubwa (ya kuhatarisha). Wawekezaji wa kisasa wanamiliki heka nyingi za ardhi, wananua nyumba na majengo makubwa ya kukodisha tena kwa bei ya jumla. Wanatunza mali hizi vizuri na kuziuza tena kwa bei ya faida ya rejareja. Wawekezaji wengi wa biashara ya kukodi majengo makubwa ya biashara wanaingia hapa.

Aina ya saba: Mabepari. Watu hawa wamekubuhu katika eneo la uwekezaji na umiliki wa biashara. Huwa ni watu watu wawekezaji wakubwa kama Fords, Rockfellers, Paul Gettys, Ross Perots na Kennedys ( Nukuu, Kiyosaki, ukurasa wa 93, Roboduara nne za Mzungunguko wa Fedha). Wamejaliwa kipaji cha kufanya kazi kwa bidii kuibadili dunia kwa kutengeneza ajira na kutoa misaada mikubwa ya kifedha kwa hiari. Mtazamo huu umetolewa katika kitabu cha Kiyosaki, ukurasa wa 93, kipengele cha fedha.
Kama unataka kuwa tajiri jiulize , kwanini ni maskini? Ukweli ni kwamba lazima uhojiane na mawazo yako ili uishi maisha ya watu wa hali ya juu, na kujielimisha wewe mwenyewe kwa kusoma vitabu vingi juu ya fedha na uwekezaji. Kwa mwanzo mdogo, amua kuwa ni salama kuwekeza baadaye kwenye hisa na dhamana. Kumbuka elimu inaanza kabla haujawekeza.

HATUA SABA KUELEKEA MAFANIKIO YAKO YA KIFEDHA.
1. Jali mambo yako
Achana na watu ambao wanasema “ hauwezi kufanya hiki ” “ Haiwezekani” “ utashindwa ”. Njia pekee ya kushindwa ni wewe kukubali na kuruhusu kuwa umeshindwa. Wewe pekee ndiye unayejijua zaidi kuliko mtu yoyote duniani. Dunia imejaa vikwazo. “Kiuhalisia vikwazo na kushindwa sio kitu bali ni vile anavyojiwazia mtu binafsi.”

2. Chunga mtiririko wako wa kifedha
Pata muda wa kukaa chini na kupanga ni kiasi gani unalipa kama ni nyumba au gari au gharama zingine. Kazi yako ni kuona wapi ulipo leo. Ujue unaanzia kituo A kuelekea kituo B.

3. Tambua kipi ni salama na kipi ni hatari
Nilidhani kuwa uwekezaji katika hisa ni hatari. Japokuwa nilipojifunza kwa Kiyosaki, hususani kitu anachokiita game (Mchezo) 101, nikagundua kuwa hisa zina faida. Pale unapoona hatari unazo njia mbili za kuchagua, kuondoa mtazamo wa hatari kwa kujielimisha kuhusu hiyo hatari au kuacha.

4. Tambua wapi unataka kuwekeza
je! unataka kuwekeza kwenye hisa au nyumba? Chagua uwekezaji vizuri. Kama hujui chochote kuhusu vifaa vya umeme, usinunue hisa za vifaa vya umeme. Ni hivyo tu.

5. Tafuta ushauri
Kwenye maisha utakuwa kama watu unaombatana nao. Marafiki wana nguvu ya kukufanya ujisikie vizuri au vibaya. Chagua washauri wazuri. kama ilivyo mwanasheria siyo daktari. Chagua mshauri mwenye taaluma ya uwekezaji huo.

6. Badili changamoto kuwa nguvu yako
Kila siku tafuta kitu kizuri katika kila kibaya. Badili changamoto kuwa mafanikio. Unapokuwa na tatizo usiseme “ siwezi ” fikiri “ ni jinsi gani naweza kutatua hili tatizo ”. Katika kila tatizo kuna jibu usikate tamaa.

7. Nguvu ya Imani
Kama unadhani unaweza basi unaweza. Kama tatizo ni kubwa tafuta kila linalowezekana kulitatua.. Kwa upande wangu najisikia amani kuwa na Mungu kama rafiki yangu wa karibu. Ninapoona mambo kama hayaendi huwa nayakabidhi mikononi mwake. Nina imani kwa Mungu kunipa mimi nguvu, wakati wajibu wangu ni kufanya kazi.
Kipengele hiki kimetolewa kwenye ukurasa wa 199, Roboduara Nne za Mzungunguko wa Fedha. Jua uko wapi leo, vuta picha wapi unataka kwenda. Onyesha wengine kwamba una nguvu ya kutimiza ndoto zako, zikawa halisi. Usikate tamaa na umwamini Mungu. Endelea kujielimisha kwenye eneo la fedha. Kuwa na mshauri mzuri wa kukutia moyo hata kushinda vikwazo.

Roboduara nne za Mzungunguko wa Fedha, katika kitabu cha Kiyosaki kinaelezea kwa undani zaidi kuliko hata kitabu chake cha kwanza “ Rich dad, Poor dad ”. WALIOAJIRIWA na WALIOJIAJIRI wanatozwa kodi kubwa wakati wanapata kipato kidogo. WAWEKEZAJI na WAMILIKI WA BIASHARA wanatozwa kodi ndogo wakati wanaingiza kipato kikubwa. Jifunze kuwekeza kabla hujaanza kuwekeza. Fuata ndoto zako na matendo yako yazidi maneno yako.

Comments

Dr Ipyana
Reply

Asante sana mkuu usiache kuamdika

nanauka
Reply

Nashukuru Kwa Feedback Dr.Ipyana.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website