Navigate / search

Mbinu Wanayotumia Wanasayansi Wakubwa Kuongeza Uwezo Wao Wa Kufikiri

Kwa mujibu wa mtaalamu wa sayansi ya ubongo,Tony Buzan anasema kuwa kila kmwanadamu ana jumla ya seli bilioni mia moja katika ubongo wake ambazo pia zimeunganishwa na seli zingine elfu ishirini kwa kila mojawapo.Hii maana yake ni kuwa,uwezo wa mtu mmoja kupata mawazo na kuja na mambo ya ubunifu wa aina mbalimbali hayawezi kuzuiwa na kitu chochote kile katika maisha yake.
Inasemwa kuwa kwa mwanadamu wa kawaida huwa anatumia chini ya 2% ya uwezo wake wa ubunifu katika kutatua matatizo yanayomkabili.Kwa mfano mwanasayansi maarufu sana Albert Einstein ambaye alionekana kufanya mambo makubwa sana duniani ni kwamba aliweza kutumia kati ya 10%-15% ya uwezo wake wote ambao alikuwa nao.Hii ni kusema kama na wewe utaamua kuanza kuushughulisha ubongo wako na kujua mbinu za kuutumia basi utaanza kupata matokeo makubwa sana katika maisha yako.
Hata hivyo,kitu kimojawapo ambacho unatakiwa kujua ni kwamba unahitaji mbinu ambazo wengine wamekuwa wanazitumia ili na wewe pia upate matokeo kama ambayo wao pia wamekuwa wanayapata.Kama utaaishi bila kujua kabisa mbinu ambazo wenzako huwa wanazitumia ili kujenga uwezo wao wa kufikiri na kuwa wabunifu katika yale wanayoyafanya basi utajikuta unafanya kazi kwa bidii lakini unapata matokeo hafifu.Leo ningependa kukusaidia kujua mbinu moja ambayo itakusaidia kuongeza ufanisi katika kazi unayofanya,biashara yako,masomoni ama chochote kile.
Mbinu hii ya inaitwa “Brain Storming” ambayo maana yake ni kuulazimisha ubongo kufikiri kwa kiwango cha juu kuliko ulivyozoea.Jambo moja ningependa ulifahamu kabla hatujaendelea ni kuwa ukuaji wa uwezo wa ubongo wako unafanana kabisa na ukuaji wa misuli ya mwili.Kadiri mtu anavyofanya mazoezi ya mwili ili kukuza misuli yake ndivyo ambavyo atazidi kuwa mkakamavu,na vivyo hivyo kadiri mtu ambavyo anafanyisha mazoezi ubongo wake kupitia mbinu hii basi ndivyo ambavyo atazidi kuujenga uwezo wake katika kufikiri.
Unapotaka kutumia mbinu hii hatua yab kwanza ni kuwa na “Focused thinking” kufikiri katika jambo moja bila kuyumbishwa.Hii inamanisha unaamua kufikiri juu ya jambo fulani bila kuondoa mawazo katika hilo ama kuanza kuwaza jambo lingine.Hii itakuhitaji uwe na sehemu ya utulivu unapotaka kufanya zoezi hili,ndio maana wanasayansi wengi ambao waliwahi kutumia mbinu hii walikuwa wanatafuta mahali penye utulivu kama vile kwenye maabara ambako ndiko waligundua mambo mengi sana ya kisayansi.
Hatua ya pili ni kuhakikisha kuwa una mahali pa kuandika.Kama kuna changamoto inakusumbua ama kama kuna lengo unataka kulikamilisha na unataka kutumkia mbinu hii;basi hakikisha unakuwa na karatasi ya kutumia.Unachotakiwa kufanya ni kuandika kile ambacho unakitafutia majibu pale juu kabisa kisha unaanza kujiuliza-Natakiwa kufanya nini ili niweze kukamilisha lengo hili nililonalo/niweze kuishinda changamoto hii niliyonayo?Unapojiuliza swali hili ni rahisi sana kuona kuwa hauna majibu ya haraka au mepesi kama unavyofikiria.Ila watu ambao wanafaidika ni wale ambao huwa wanajilazimisha kuwa na majibu yasiyopungua angalau 20 kwa kila changamoto.Hii inamaana unajilazimisha kufikiria hata wakati pale unaona hauna majibu ya haraka.Ukweli ni kuwa mwanzoni itakuwa rahisi lakini kadiri unavyokuwa unaendelea mbele ndivyo utaona ugumu,lakini unatakiwa kujilazimisha.Hii ni sawa na mtu ambaye anafanya mazoezi ya mwili na anasikia maumivu lakini inabidi ajilazimishe kuendelea.
Unachotakiwa kufanya ni kwa kila changamoto ama lengo ulilonalo kufanya zoezi hili ili uweze kujipatia majibu mengi na unatakiwa kuanza kuyafanyia kazi mara moja.Leo unaweza kuanza kutumia mbinu hii na itakushangaza kuona kuwa mambo mengi ambayo ulikuwa unafikiria kuwa hayana majibu ama hauna mbinu ya kuyatatua ni kwa sababu ulikuwa hautumii mbinu hii ya “Brain Storming”.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website