Navigate / search

Mbinu Itakayokusaidia Kutatua Kila Changamoto Inayokukabili

Umeshawahi kujiuliza uwezo wa kubuni vitu na kupata suluhisho ya mambo mbalimbali huwa unatoka wapi?Ukweli ni kuwa kila mtu ambaye una muona ana uwezo mkubwa sana katika maisha yake kuna mbinu alitumia ambazo zilimsaidia kuongeza uwezo wake wa ubunifu na uwezo wake wa kutatua matatizo katika maisha,na wewe ukizijua mbinu hizi basi utajijengea uwezo mkubwa sana wa kutatua matatizo katika maisha yako.
Leo nataka nikushirikishe mbinu muhimu ambazo na wewe unaweza kuanza kuzitumia kuongeza uwezo wako wa ubunifu na kupata suluhisho kwenye changamoto zinazokukabili:
Njia hi inaitwa “Focused thinking”: Focused thinking ni njia ya kutatua matatizo ambayo yanakukabili kwa njia ya kuamua kufikiria kuhusu jambo moja tu na kuamua kuacha kabisa kufikiria mambo mengine.Hii inawezekana kutokea pale ambapo uanaamua kuchukua peni na karatasi na kukaa peke yako na kujiuliza hivi kuna njia ngapi za kutatua tatizo hili linalonikabili.
Watu wengi sana wanapokuwa kwenye changamoto za maisha huwa wanakosa kabisa muda wa kuwa peke yao na kutafuta majibu ya changamoto zinazowakabili.Unaporuhusu changamoto ikufanye usipate muda wa kufikiri,kitakachotokea ni kuwa utaendelea kujiingiza katika matatizo zaidi kwa kufanya maamuzi ambayo siyo sahihi kila wakati.
Unapopata muda wa pekeyako na kujilazimisha kutofikiria kitu kingine isipokuwa kitu kimoja ambacho unataka kupata suluhisho lake,ubongo wako huwa unaacha kila kitu na kuanza kukusaidia kutafuta majibu.Ukiwa katika hali hii,unazima simu zako zote,hakuna TV wala redio n.k Unatengeneza mazingira ya kubakia wewe tu na kufikiria jambo moja.Hata kama ubongo wako utakuwa unajaribu kukufikirisha kuhusu jambo linguine unatakiwa usikubali,urudishe mawazo yako katika kile uanchotaka.
Njia bora ya kutumia focused thinking ni ile ambayo inaitwa (20 answers)-Majibu 20.Unachofanya unaandika changamoto inayokukabili juu ya karatasi kabisa na unajilazimisha kuwa na mbinu 20 za kuitatua.Utakapoanza kuandika tano za kwanza itakuwa rahisi ila kadiri ambavyo unaendelea itazidi kuwa ngumu lakini inabidi udhamirie kufikisha hadi 20 na usiache,andika kila unachofikiria unaweza kukifanya ili utatue changamoto hiyo.Ukishafanikiwa kumaliza kuandika orodha yote ya mambo ishirini-Jiulize ni mambo gani 3 kati ya haya ambayo nikiamua kuyafanya yatanisaidia katika kutatua changamoto hii.
Ukishaweza kuyapata mambo haya basi hatua inayofuata ni kuhakiksiha kuwa unachukua hatua mara moja bila kuchelewa.Wakurugenzi wa makampuni makubwa sana huwa wanatumia mbinu hii ili kupata majibu na mbinu za kukuza biashara zao.Wako wafanyabiashara wakubwa sana ambao walitumia mbinu hii ili kujitoa katika changamoto za kibiashara na wakaweza kurudi tena kuendelea na biashara zao.
Leo na wewe anza kutumia mbinu hii-Kama kuna lengo ambalo uko serious unataka kulitimiza,kama uko kati kati ya changamoto n.k anza kuutumia ubongo wako kwa njia hii na utashangaa matokeo ambayo utayapata.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website