Navigate / search

Mbinu 7 Za Namna Ya Kufikiri Ambazo Waliofanikiwa Huzitumia

 

President Barack Obama sits at his desk in the  Oval Office during a phone call with Chinese President Hu Jintao May 6, 2009. Official White House Photo by Pete Souza.  This official White House photograph is being made available for publication by news organizations and/or for personal use printing by the subject(s) of the photograph. The photograph may not be manipulated in any way or used in materials, advertisements, products, or promotions that in any way suggest approval or endorsement of the President, the First Family, or the White House.

Kitabu cha Badilisha unavyofikiria ili ubadilishe unavyoishi(Change your thinking,change your living) ni kitabu kizurI sana kinachobadilisha mtazamo.Karibu kila sura ya Kurasa hii ina vitu vizuri,kwa kuzingatia ukubwa wa kitabu hiki(Kurasa 290) ambacho ni kati ya vitabu vitatu nilivyosoma kwa mwezi wa pili,nimefurahishwa sana na namna saba ambazo watu waliofanikiwa wanavyofikiri katika sura ya mwisho ya kitabu hiki.

Ningependa nikushirikishe kwa kifupi ili ujipe na ujue kama nawe unaelekea katika mwelekea huo ama la:

1)Waliofanikiwa hufikiri juu ya WANAKOKWENDA

Watu waliofanikiwa hutumia muda mwingi kufikiri juu ya wanakokwenda na sio kule walikotoka.Huwa hawapotezi muda wao kufikiri juu ya namna walivyoshindwa ama walivyofeli.Huweka mawazo yao kwenye hatima yao jinsi ilivyo nzuri.

2)Wanafikiri juu ya malengo na MIPANGO YAO
Huwa hawapotezi muda kufikiri ama kuzungumza juu ya watu wengine.Huweka malengo yao tena mahsusi.Kila wakati hufikiri juu ya malengo yao na huyfanyia kazi bila kuchoka hata kama ni kwa hatua kidogo kidogo.

3)Hufikiri mbinu za kufanya mambo KWA UBORA

Kila wanachofanya huwa hawatakai kufanya mambo kwa kiwango cha chini kwani wanajua kila fursa hufungua fursa nyingine.Kwa sababu hiyo katika kila wanachopewa kufanya,hufanya kwa ubora na hutafuta mbinu za uongeza uwezo wao wa kuboresha Matokeo kila wakati.

4)Hufikiri juu ya kupata SULUHISHO

Kwenye Kila tatizo watu waliofanikiwa hujikita katika kutafuta suluhisho la matatizo yao na sio kutafuta mtu wa kumlaumu ama kutafuta visingizio.Bila kujali chanzo cha tatizo hujiuliza-Hivi suluhisho la changamoto hii inaweza kuna ni ipi?

Watu wanaofanikiwa huamini kuwa kila tatizo lina suluhisho lake.

5)Kila wakati wanafikiri namna ya kupata MATOKEO MAKUBWA

Kwenye kila wanachofanya hutafuta njia za kupata matokeo makubwa.Huweka vipaumbele vya kila siku,na hujiuliza ni mambo gani nikifanya leo yatanipa matokeo makubwa Zaidi na huanza nayo hayo.
Watu waliofanikiwa hawajikiti katika kufanya mambo mengimengi yasiyochangia malengo yao bali huchagua mambo machache yanayochangia kwa kiwango kikubwa kufikia malengo yao.

6)Huwa WANAJIKUZA katika KILA ENEO

Watu wanaofanikiwa hufikiria kila wakati ni njia gani zitawafanya waongeze uwezo katika kila eneo muhimu kwenye maisha yao.Huwa ni watu wa kusoma vitabu,kusikilza mafundisho mbalimbali na kuhudhuria mafunzo yanayowajengea uwezo.

Huwa wanatambua kuwa mafanikio katika ulimwengu na kwenye fani zao hutokana na uwezo wao katika ushindani na sio bahati.

7)Hufikiri namna ya KUCHUKUA HATUA BILA KUCHELEWA.

Watu wanaofanikiwa ni watu ambao huchukua hatua za kutekeleza yale waliyojifunza na wameyaamini.Watu waliofanikiwa si watu wa maneno mengi mengi bali ni watu wa vitendo vingi vingi,huwa na hali ya uharaka kwa kila jambo muhimu(sense of urgency).

Kila siku hujiuliza,leo nifanye nini bila kuchelewa ili kusogea hatua moja Zaidi?Hawapendi kuchelewa kuweka katika vitendo kila jipya wanalojifunza.
Je nawe unafikiri kwa namna hii au kuna maeneo unahitaji kuongeza uwezo wako?

Endelea kutembelea Ukurasa wangu wa facebook Kujifunza Zaidi na ili Kuunganishwa kwenye group la Watsapp kwa ajili ya Mafunzo zaiid bila Malipo,tuma neno-“Ndoto Yangu” na kisha jina lako kenda nambari 0655 720 197

See You At The Top.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website