Navigate / search

Mbinu 3 za Kutumia MUDA wako Ili Kuongeza Kasi ya Mafanikio

time-management

Tangu nianze kufuatilia kuhusiana na sayansi ya mafanikio na historia za watu waliofanikiwa katika maisha yao,hakuna mtu ambaye nimeshawahi kukuta amefanikiwa na asiwe mtu ambaye anajali sana muda.Sifa moja ambayo inawaunganisha watu wote ambao wamefanikiwa katika maisha yao ni uwezo wao wa kuthamini muda na kuamua kuwekeza katika kila dakika waliyonayo.Watu wengi sana wameshindwa kufikia hatima za maisha yao kwa sababu ya kudhindwa kujua namna bora ya kutumia muda wao.

Hivi ni mara ngapi katika maisha yako umejikuta umetumia muda mwingi katika kufanya jambo fulani ambalo hukutarajia kutumua muda mwingi ama halichangii katika kukupeleka katika mafanikio yako makubwa.Mafanikio ni matokeo ya kutumia muda wako vizuri katika kufanya mambo ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kukusogeza hatua moja zaidi kuelekea katika ndoto yako na kufeli ni matokeo ya kutumia muda wako katika mambo ambayo hayachangii katika ndoto yako kubwa.

Ili kujua hilo unaweza kuanza kujiuliza kwa siku ya leo ratiba yako ikoje?Umepanga kufanya mambo gani?Hebu jaribu kuangalia katika mambo uliyopanga kuyafanya leo ni mangapi ambayo yanachangia katika malengo yako makubwa ya mwaka huu?Ukigundua kuwa katika mambo uliyopanga kuyafanya ni machache sana/Hakuna ambalo linachangia katika mafanikio yako basi ujue uko katika njia ya wanaofeli.Kama wewe ni mtu ambaye unatumia muda mwingi katika vitu vinavyofurahisha zaidi kuliko ambavyo vinakujenga na kukupa maarifa mapya basi ujue mafanikio yako yatachelewa sana.

Hata hviyo ningependa leo tujifunze namna 3 za kukusaidia kutumia muda wako kwa mafanikio kila wakati ili uweze kutimiza malengo yako bila kushindwa kabisa:

Jambo la kwanza ni kuhakikisha kuwa kila wakati unaanza kufanya jambo la muhimu zaidi bila kujali lina ugumu wa kiasi gani.Watu wanaofanikiwa siku zote ni wale ambao wanajikita katika kufanya mambo ya muhimu zaidi na yenye mchango mkubwa zaidi katika malengo yao badala ya kufanya mambo yasiyochangia katika malengo yao.Watu hawa ni wale ambao wakiamka asubuhi hawaanzi kusoma magazeti kwanza ama kurudia meseji za kwenye magrupu ya watsapp ambazo zilitumwa wakiwa wamelaa ama kuanza kusikiliza nyimbo mpya za wasanii zilizotoka-HAPANA,Huwa jambo la kwanza ambalo wanafanya ni kujiuliza-Hivi katika mambo ninayotakiwa kuyafanya leo ni jambo lipi ambalo ndilo la muhimu zaidi,wakishalijua huanza na jambo hilo mara moja bila kuchelewa.

Kila siku tafuta mambo mawili au matatu ambayo ndio yana mchnago mkubwa katika maisha yako na uanze na hayo.Hata siku ya leo,hebu jiulize ni mambo gani unatakiwa kuyafanya ambayo yana mchango mkubwa katika malengo yako na anza na hayo bila kuchelewa hata kidogo.Na ukianza kufanya,usikubali kuishia njiani hadi umekamilisha.

Jambo la pili ni lazima ujifunze kusema hapana.Kila siku utakuwa na muda mchache sana wa kufanya mambo na hauwezi kufanya kila kitu.Watu wanaofeli katika maisha yao ni wale ambao huwa wanajaribu kufanya kila kitu ndani ya masaa waliyonayo kwa siku hiyo na matokeo yake huwa wanajikuta hakuana cha maana ambacho wamefanikiwa kukifanya hadi siku inaisha.

Steve Jobs aliwahi kuulizwa maana ya kuwa na mtazamo usioyumbishwa(focus) akasema ni uwezo wa mtu wa kusema hapana.Usiogope kumwambia mtu kuwa hautakuwa na muda wa kuhudhuria tukio fulani,usiogope kumwambia mtu kuwa hautakuwa na muda wa kumsindikiza mahali,usiogope kusema kuwa muda wako hautoshi kuhudhuria tukio fulani.Ni lazima uwe mkatili kwa muda wako,kumbuka kuwa pesa unaweza kupoteza na ukapata nyingine ila muda ukienda huwa haurudi tena.Kiufupi ni kuwa kila ambaye umekubali kutumia muda wako kwake basi unatumia sehemu ya maisha yako.Kila wakati unapotumia muda wako kwa jambo fulani hebu jiulize,haya ni matumizi bora ya muda wangu?Kama jibu lako ni hapana basi badilisha unachofanya na ufanye jambo lingine.

Jambo la tatu ni kuhakikisha kuwa kila wakati unapokuwa unafanya jambo fulani hakikisha akili yako yote ipo hapo.Achana na ile tabia ya kufanya kitu sekunde mbili kisha unachart mara umeangalia facebook n.k. Kama umeamua kufanya jambo fulani basi akili yako yote iweke hapo na ufanye bila kuachaacha.Kila mara unapofanya jambo halafu unakatisha na kuanza upya,unaufanya ubongo wako utumie nguvu nyingi katika kufanya jambo moja na itakuchukua muda mrefu kukamilisha kitu kimoja.Leo,utakapoanza kufanya jambo fulani usiruhusu kuachaacha kwa kufanya vitu vingine vya pembeni ambavyo havina umuhimu.

Ili kufanikiwa katika jambo hili unaweza kuamua kuwa kila wakati unapokuwa unafanya jambo fulani la umuhimu basi simu yako utaiweka isitoe sauti ama hata wakati mwingine kuizima(inategemea hilo jambo lina umuhimu kiasi gani) ama kuondoa matumizi ya internet kwa wakati huo(flight mode/data off).Kama umeanza kufanya jambo fulani na mtu anakuja na anaanza kukuongolesha,uwe na ujasiri wa kumwambia kuwa “tafadhali nipe muda nimalizie hili ninalofanya kisha tutaongea”.Kumbuka kuwa watu wengi walioko duniani hawajui kwa nini walizaliwa na hawajui wanaelekea wapi hivyo kwao muda hauna thamanin kabisa,sasa kama unataka kufanikiwa ni lazima ujue namna ya kukabiliana nao.

Kumbuka Kuwa ndoto Yako inawezekana.

Unaweza kuendelea kutembelea www.JoelNanauka.Com na www.Mentorship.co.tz ili kujifunza zaidi.

See You At The Top

© JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website