Navigate / search

Mbinu 3 Alizozitumia JUSTINA Kujenga Kiwanda Chake Akiwa Bado Ameajiriwa

Justina31

Justina Kavale ni binti wa miaka 33 ambaye akiwa bado ameajiriwa alikuwa na  ndoto ya kuja kujiajiri siku moja katika maisha yake.Wazo lake la kwanza kuhusu biashara alilipata wakati anasoma shahada yake ya uzamili katika utawala wa biashara(Masters in Bussiness Admininstration).Anasema wakati anaendelea kusoma awamu mbalimbali(modules) aligundua kuwa nafasi anayofanyia kazi katika shirika kwa sasa haimruhusu kutumia maarifa yote ambayo anayapata.Hivyo akafikiria kuwa akiwa na kampuni yake mwenyewe basi ataweza kutumia kanuni ambazo amejifunza katika masomo yake.

Ilipofika mwaka 2012 alifanya maamuzi ya kusajili kampuni yake mwenyewe lakini wazo hili alikaa miaka miwili bila kulifanyia kazi hadi mwaka 2014 alipochukua hatua ya kwanza kuanza utaratibu wa kusaijli.Kwa kuanzia alianza kutumia jina la bidhaa zake(brand name) la “ELI” ambapo alianza kuuza sabuni za kuogea,za kuoshea vyombo,na kusafisha sakafu.Anasema lengo lake ilikuwa ni kuongeza bidhaa mpya mbili kila baada ya mwezi mmoja.

Alipoulizwa kwa nini aliamua kuingia katika uzalishaji wa bidhaa hizo,alisema kuwa aligundua kuwa biashara ya namna hiyo ina wateja wengi nchini Namibia ila kuna viwanda 4 tu vinavyotengeneza bidhaa hizo.Anasema aligundua kuwa ili mtu afanikiwe kibiashara ni lazima auze bidhaa ama atoe huduma ambayo inahitajika na watu wengi na inahitaji kwa kila siku pia.

Kati ya changamoto kubwa ambayo alikutana nayo kwenye kuanza kutimiza wazo lake ilikuwa ni kupata mtaji.Anasema kila wakati alipopeleka mchanganuo wake (proposal) benki maafisa wa benki walisema wazo lake haliwezi kuleta faida ya kumwezesha kulipa mkopo.Hivyo aliamua kuanza kutunza sehemu ya mshahara wake kila mwezi hadi alipopata kiasi cha kutosha cha kuweza kununua mashine za kwanza kabisa.Alipoulizwa aseme siri moja ya mafanikio katika maisha ya kuanzisha biashara anasema,ni uwezo wa kuamini katika mawazo yako bila kukata tamaa kwa namna yoyote ile.

Ukichunguza hatua za Justina utagundua kuwa kuna mambo mengi ambayo yanafanana na watu wengi sana kwa leo.Kama ambavyo Justina alikuwa mwajiriwa huku akiwa anatamani sana kuwa na chanzo cha kipato nje ya ajira yake na siku moja afanikiwe kujiajiri,ndivyo ilivyo kwa watu wengi sana duniani leo.Hata hivyo,mafanikio yake yalijengwa katika misingi mitatu ifuatayo:

Kwanza ni uamuzi wa kufanya na kuchukua hatua kuanza kufanya.Kama ilivyo wengi,Justina naye alikiri kuwa ilichukua muda kabla hajaanza kufanya kwa vitendo kitu alichoamua kukifanya.Kwake yeye ilimchukua miaka 2 kabla hajaanza kuchukua hatua.Najua hata wewe una mawazo fulani umekuwa ukiyawaza kila wakati na kila siku unasema utafanya,lakini bado haujafanya hadi leo.

Unachotakiwa kujua ni kuwa kama Justina asingechukua hatua yoyote ile ili kuanza kufanya ambacho ameshaamua basi hadi leo angekuwa wa kawaida.Kuamua kufanya jambo ni hatua ya kwanza bali kuanza kufanya ni hatua muhimu zaidi unayohiitaji.Kwa chochote ambacho umeamua kukifanya katika maisha yako,Chukua hatua leo.Usiseme utasubiri kesho,Anza leo.

Jambo la pili la kujifunza kutoka kwa Justina ni uwezo wa kuliamini wazo lake katikati ya watu wanaokatisha tamaa.Hebu fikiria unaenda benki kwa wataalamu halafu wanakumabia wazo lako haliwezi kufanikiwa hata kidogo.Ndivyo ilivyo,mara nyingi utakapoanza kuwaeleza watu mawazo yako utakutana na watu wa namna hii ambao kila wakati watakuambia kuwa “Hilo haliwezekani”,”Kitaalamu hili ni gumu”.Kama Justina angekubali kuwasikiliza watu waliomkatisha tamaa basi leo hii asingekuwa amefanikiwa ama kuchukua hatua.Haijalishi watu wangapi wanasema unachofanya/Unachotaka kufanya ni kitu hakitaweza kufanikiwa,unatakiwa kuamini zaidi ya wale wasioamini;Kama kuna kitu chochote utakosa katika kufanikisha ndoto yako basi usikose kuamini kuwa wazo lako litafanikiwa.

Jambo kubwa la tatu ambalo limemsaidia sana Justina ni kuamua kutafuta njia mbadala ya kupata mtaji aliokuwa anauhitaji.Baada ya kuona kuwa imeshindikana kabisa kwa mabenki kuweza kumpatia pesa aliyokuwa anahitaji,Justina aliamua kuanza kuweka akiba kidogokidogo ya pesa aliyokuwa anaipata kila mwezi.Kwa namna yoyote ile,bila kujali wazo ambalo unalo katika maisha yako leo,lazima kuna njia mbadala.Kama kuna watu ulitarajia wakusaidie kwa namna fulani lakini imeshindikana,unachotakiwa kufanya sio kuishi katika kuwalaumu waliokunyima bali ni kuanza kujiuliza kila wakati-“Hivi njia mbadala ya kulitimiza ili ni ipi?”.Ukiilekeza akili yako kuanza kutafuta jibu la swali hili leo,utashangaa jinsi utakavyopata njia mbalimbali.Siku zote usikubali kuamini kuwa hakuna njia ya kupata suluhisho la changamoto uliyonayo.Kwa kila changamoto sikuzote kumbuka kuwa kuna suluhisho yake mahali fulani.

Naamini leo utakuwa mwanzo mpya wa kile ambacho umekuwa ukikiwaza kila siku na hakuna kitu kitakachokusababisha ughairishe ama ukate tamaa.Kumbuka kuwa ndoto Yako Inawezekana,

Endelea kutembelea www.JoelNanauka.Com ili Kujifunza zaidi.
 See You At The Top
©JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website