Navigate / search

Matokeo Ya Utafiti:Tabia Hii Moja Ndio Huwafanya Watu Wafeli Maishani.

 

child-walk-support

Professor Simon Sherry ni mwalimu wa saikolojia wa chuo kikuu cha Dalhousie University aliyewahi kufanya utafiti juu ya uhusiano kati ya mafanikio ya mtu na tabia ya kupenda kusubiri mazingira timilifu kabla ya kufanya(perfectionism).Baada ya kufanya utafiti alichapisha utafiti huo katika jarida la “University Affairs Magazine” na akaeleza kuwa kuna uhusiano mkubwa na wa moja kwa moja kati ya tabia ya kusubiri mazingira timilifu(perfect conditions) na kupungua kwa kiwango cha mafanikio ya mtu.

Utafiti ulionyesha kuwa watu ambao huwa wanasubiri mazingira kukamilka na kuwa timilifu kabla hawajachukua hatua kuanza kutekeleza malengo yao huwa wanachelewa sana kufanikiwa kwa sababu zifuatazo.

Moja,huwa wanatumia muda mwingi sana kukamilisha lengo moja.Watu wanaopenda ukamilifu wa kila kitu kabla hawajuchukua hatua huwa wana tabia ya kusubiria mazingira yawe kama wanavyotaka-Ukiwauliza kwa nini haujaanza ile biashara ,watakujibu bado mazingira hayajakamilika?Ukiwauliza kwa nini haujaanza ile kampuni watakuambia bado nasubiri mambo yakamilike.Watu wa namna hii huwa ni watu wenye mawazo lakini hawana vitendo.Kazi yao kubwa ni kuongea na sio kutenda,ni watu wanaoamini ili waanze kufanyia kazi mawazo yao ni lazima kila kitu kiwe sawa na ni lazima kila mtu wanayehitaji awasapoti awe tayari kufanya hivyo.Kama kweli unataka kufanikiwa achana na tabia ya kusubiri kila kitu kiwe sawa,anza kutumia ulichonacho na kwa kiwango unachoweza pale ulipo sasa.Je,katika mawazo uliyonayo,leo unaweza kuanza hatua gani?Kumbuka huwezi kupata unachotafuta hadi umeweza kutumia ulichonacho.

Mbili,huwa ni watu wa kughairisha ghairisha mambo.Watu wa namna hii utafiti uligundua kuwa ni watu ambao klia wakati wanaghairisha mambo.Ni wale watu huitwa mr/Mrs Tommorow.Wao kila kitu utasikia nitafanya kesho.Walipoanza mwaka walikuwa na mipango mingi na walikuwa hawachoki kuisimulia lakini hadi robo ya mwaka inaisha utasikia nitafanya kesho,kitabu nitaanza kusoma kesho,nitaanza kuweka akiba kesho n.k,huwa hawachukui hatua kwa haraka.Kama unataka kufanikiwa ni lazima uwe na “sense of urgency”(uharaka wa kufanya mambo).Usiwe mtu wa kughairisha mambo kila wakati.Leo,hebu kagua mipango yako ya mwaka huu na jiulize,kuna mambo mangapi nimekuwa naghairisha tangu mwaka huu umeanza?Yaandike chini na jipange namna ya kuanza kuyatekeleza.Mafanikio sio matokeo ya kuwa na mipango mizuri tu bali ni matokeo ya kuwa na utekelezaji mzuri.

Tatu ni kuwa huwa wanakatishwa tamaa na mambo madogomadogo na kusahau ndoto kubwa ya maisha yao iliyo mbele yao.Watu wa namna hii wameonekana kuwa huwa wanakata tamaa sana mambo madogomadogo yanaposhindwa kufanikiwa katika maisha yao.Kama wewe ni mtu ambaye jambo dogo tu likienda mrama unakata tamaa,au mtu mmoja tu akiongea neno la kukuudhi ama kukukatisha tamaa basi ameharibu siku yako nzima,ujue kuwa unajitengenezea mazingira magumu ya kufanikiwa.Ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe mtu ambaye haukatishwi tamaa kirahisi na magumu yanayokupata kila siku.

Wiki hii,usikubali jambo lolote litokee na likukatishe tamaa katika maisha yako,kila wakati angalia ndoto yako kubwa na uamini kwamba utavuka kila kikwazo na utafikia lengo lako.
Mafanikio yamejengwa katika misingi ya kisayansi,zingatia mambo haya matatu na ujiepushe kuwa kati ya wale ambao hawatafikia malengo katika wiki hii.Chukua hatua muhimu kuelekea katika kuitimiza ndoto yako.

Endelea kutembelea www.JoelNanauka.com ili kujifunza Zaidi.

Kumbuka kuwa Ndoto Yako Inawezekana.

See You At The Top.

Comments

jacqueline mwasha
Reply

shaloom pastor asante sanaaaa mnooo kwa mafundisho haya,ni kweli kbsaaa watu wa aina hii ni wengi sana,i use to be one of them lakini namshukuru YESU i am not anymore.ubarikiwe sana.ur blessed.

saul samwel
Reply

Hallo , nafurahi kwa mtazamo ulionao ktk kufuatilia mambo ya maana sana kwenye website hii.Hata Mimi , Mentor was website hii ananibariki sana japo ninashauku sana ya kuongea nae via his hotline no. If you have it, kindly naomba unisaidie.

chisanyo Charles
Reply

Fundisho lina mashiko,kimsingi watu wengi tuna tatizo la kuthubutu na tumekuwa tukiangalia mara nyingi hasara gani utapata pasi kujikita katika malengo na furusa zilizopo.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website