Navigate / search

Maswali Mawili:Ukipata Majibu Yako,Utafanikiwa Kwa Haraka

12733997_1210092152353461_2383054601350825892_n

Kuna maswali muhimu mawili ambayo ukiyapatia majibu yake mapema yataongeza sana kasi yako ya kufikia mafanikio yako.

Ningependa kukumbusha watu wanoitwa magenius duniani nguvu mojawapo waliyonayo ni kujiuliza maswali kila wakati na kutafuta majibu yake kwa nguvu zote.

Swali la kwanza;Ni ujuzi(skill) gani ambao ukiuongeza mwaka huu utakuwa na matokeo makubwa katika kuifikia ndoto yako?inawezekana ni ujuzi wa kutunza muda wako au ujuzi wa kuzungumza mbele za watu(public speaking) ama ujuzi wa kutumia fedha au uwekezaji au kusema hapana pale usipopenda au kuwa ujuzi wa kutoghairisha mambo ?kutegemea na malengo uliyonayo jiulize swali hili na ujipe majibu.

Pili,Je ni aina gani ya watu ambao niko nao na natakiwa kupunguza ukaribu nao kwani wananirudisha nyuma?hili ni gumu ila ni la muhimu sana kwani kiwango cha mafanikio Yako kinatokana sana na aina ya watu unaombatana nao.Jikague, kama watu wanaokuzunguka ni chanzo cha wewe kutumia pesa hovyo, kuwa mlevi ama kuingia Kwenye madeni au ndio huwa wanasababisha ushindwe kufikia ndoto yako kila mwaka;ni wakati wa kuanza kuweka umbali nao.Ukikosa ujasiri wa kuweka umbali na watu kama hawa ndivyo unavyozidi kujichelewesha kufikia malengo yako.

Mambo haya ni kawaida sana ila yanaleta tofauti maishani kwa kiwango kikubwa.

Je,unaweza kuniambia hapa chini kwa swali la kwanza ni ujuzi gani mmoja ambao mwaka huu ukiupata utaleta tofauti sana Maishani mwako?

Tembelea www.JoelNanauka.Com kujifunza Zaidi.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website