Navigate / search

Mashahidi muhimu TZ:Wanakufa,Wanajiua ama wanauwawa?

tanzania-court-of-appeal

Ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania kama nchi tunakabiliwa na tatizo kubwa sana la Rushwa  (Grand Corruptions) ambazo kwa muda mrefu zimeathiri shughuli za kimaendeleo na kuleta hasara kwenye pesa za umma.Wakati Kamati ya PAC ikiandaa ripoti yake ya mwisho kuhusu ESCROW ili kuisoma bungeni mwenyekiti wa kamati na makamu wake(Zitto Kabwe na Deo Filikunjombe) walieleza kuwa walipata vitsho vya kuuwawa.Hata hivyo kinara muibua hoja David Kafulila alieleza kuwa usalama wake ulikuwa hatarini kiasi cha kutafuta mtu maalumu wa kuja kumpikia chakula kwani alikuwa haamini mtu mwingine kabisa.

Leo kwa masikitiko makubwa nimesikia kifo chandugu Erasto Kihwele aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa reli Tanzania.Hii ni baada ya hivi karibuni waziri sitta kusimamisha viongozi watano wa ngazi ya juu katika shirika hilo.Ni jambo lisilo na ubishi kuwa katika kufichua ubadhirifu na ukiukwaji wa kanuni katika ununuzi wa mabehewa 25 yenye thamani ya bilioni 230 ilikuwa ni kazi kubwa ya Bwana Kihwele.Kifo chake kilichoelezwa kutokana na kisukari na BP kimekuja masaa 17 tu baada ya waziri Sitta kuwasimamisha viongozi waandamizi.

Kifo cha Bwana kihwele kimwnikumbusha kifo cha Bwana Sylvester Rwegasira aliyeafariki mwaka 2011 aliyekuwa ni katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa Reli pia.Wote waili wamesifika kwa umahiri wao wa kusimamia maslahi ya wafanyakazi na kuibua uozo uliokuwa unaendelea katika shirika hilo.Ingawa vifo vyote vinaelezwa kuwa i vya kawaida,jicho la upande mwingine linapata shaka hasa kutokana na muda wanaofariki ukizingatia kuwa wao ni watu muhimu katika ushahidi wa kina.

Mwaka 2014 May aliyekuwa mkurugenzi wa petrol wa EWURA mr.Julius Gashaza alikutwa amekufa katika chumba chake cha hotel.Hii ilikuwa ni baada ya kuibuka kwa wizi wa bilioni 83 zilizokuwa hazijulikani ziko wapi.Taarifa ya awali ilionyehs kuwa anaweza kkuwa amejinyonga lakini polisi walitamka rasmi kuwa hwanaendelea kuchunguza kifo chake na watatoa taariffa sahihi(sina uhakika kama ripoti ilishatoka).

Mwaka 2009 katika kesi iliyomkabili Abdalh Zombe ilipata pigo baada ya shahidi muhimu namba 11 Ramadhani Lema kufariki ghafla kwa kile kilicosemwa kuwa ni saratani.Kwa mujibu wa upande wa mashtaka huyu ndiye alikuwa shahidi muhimu kuliko wote katika kesi hiyo.

Hata hivyo baada ya muda mchache ndugu yake wa Karibu Raphael mchaki naye aliuwawa kwa kupigwa Risasi akiwa anelekea nyumbani kwake akiwa na mkewe.Taarifa zinaonyehs akuwa aliuwawa yeye na hao wauaji hawakuchukua kitu chochote ikiashiria kuwa kusudi lao lilikuwa ni kumuua yeye tu.Mchaki alikuwa ni mtu muhimu baada ya kifo cha kaka yake kwani inasemakana mambo mengi alishasimuliwa na Lema na alianza kuyasimulia.

Pia utakumbuka kuwa mtu aliyeonakana ni muhimu katika sakata la Mh.Mwakyembe kuwekewa sumu iliyoharibu ngozi yake na kuhatarisha maisha yake alisemekana kuwa alifariki katika mazingira ya kutatanisha pia.

Nchini kenya iliripotiwa kuwa Maafisa wa polisi waliupata mwili wa shahidi muhimu wa mahakama ya ICC siku chache tu kabla ya kutoa ushahidi wake katika kesi ya Makamu  wa rais(Wiliamu Rutto) katika mahakama hiyo.Ripoti za vyombo vya habari nchini Kenya zilisema kuwa mwili wa Meshash Yebei ulipatikana karibu na mto zaidi ya wiki moja baada ya kuonekana akibebwa na kuingizwa katika gari moja lisilo na nambari za usajili katika mji wa Eldoret, umbali wa kilomita 200.

Bwana Yebei alitarajiwa kusafiri kuelekea mjini Hague kwa kesi dhidi ya bwana Ruto-makamu wa rais ambaye anakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na mashambulizi dhidi ya watu wa jamii ya kikuyu katika makaazi ya wakalenjin huko Rift valley wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi miaka saba iliopita.

Ukweli ni kuwa mashahidi mahsusi(Key Witnesses) ni muhimu katika kesi yoyote ili.Jambo la msigi ni kufanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa vifo vyao ni vya kawaida(natural death) na sio mipango ya kuwaua.Hili ni muhimu hasa katika nchi yetu ya Tanzania ili kujenga utawala wa sheriaa.

Jambo la kuzingatia ni kuwa haya mambo hata yakifunikwa kwa muda gani,yatakuja kuibuka tena kama ambavyo kifo cha Sankara kinataka kuanzwa kuchunguzwa baada ya miaka zaidi ya 25.

Naipenda Tanzania.

Joel Nanauka.

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website