Navigate / search

Mambo Muhimu ya Kuyajua Kuhusu Uchaguzi wa Uingereza

ELECTION PHOTOS

Katika kuelekea matokeo ya Uchaguzi wa Uingereza,Kuna hofu kubwa kuwa hakuna chama ambacho kitapata ushindi wa jumla wa kuweza kuunda serikali ya pamoja ambapo wasiwasi ni kuwa huenda kutakuwa na serikali nyingine ya muungano wa vyama viwili kwa lugha nyepesi ya waingereza wanasema kutakuwa na Hung parliament(Bunge ambalo wabunge wa chama kimoja au mrengo mmoja hawawezi kuunda serikali).

Katika kura za maoni, bado kuna ushindani mkubwa baina ya Labour na Conservatives. Mpaka hii leo, Labour wako shingo kwa shingo na Torries kwa wastani wa asilimia 35% kwa 35%.

Conservatives imekuwa katika wakati mgumu kuweza kufanikiwa kushawishi watu kuwapa nafasi nyingine kuweza kuunda serikali. Wameshindwa katika baadhi ya Nyanja ikiwemo sera ya afya na elimu ambako vijana wengi walichukizwa na suala la kuongezwa kwa ada ya masomo ya juu kutoka £3000 mpaka £9000 kwa mwaka.

Lakini pia suala la Afya na sera za upatikanaji wa huduma za Afya limekuwa mwiba kwa serikali hii kuweza kuaminiwa tena na wananchi.Lakini yote kwa yote bado siasa za Uingereza zimetawaliwa na upepo na ngome za Utaifa(England/English) na wasio Waingereza.Mfano mzuri ni hali ambayo inaonekana hivi sasa nchini Scotland.Labour imekuwa ikifurahia ushawishi na ushindi mzuri nchini Scotland lakini sasa wameonja shubiri.

Wascotish wameonyesha hali ya kuikataa Labour kwa sababu tu iliwaunga mkono Conservatives kwenye kura za maoni za kusalia kwenye muungano wa falme za Uingereza mwaka jana.Suala hili limewafanya waone Labour si watetezi wao na badala yake wanaona ni bora kuwapa kura SNP ili waunde serikali kuliko kuipa kura Labour.Kura ile ya maoni ilikuwa na athari kwa upande wa labour huku tories wakiwa hawana cha kupoteza nchini Scotland kwa sababu hawana ushawishi mkubwa.

Hali hii ilifanya kwenye kampeni za mwaka huu David Cameron kuwashutumu Labour kuwa huenda wakaunda serikali na SNP, suala ambalo waingereza wa England hawalitaki kwa sababu wanaona SNP kama ni tatizo kuhusu muungano huu. Labour wamekataa na kuwa wako na nia ya kuunda serikali na SNP.Bado kura za maoni zinaonyesha kuwa lolote linaweza kutokea lakini Labour wako katika hali nzuri japo pia itategemea na namna hali ya hewa ya siku ya kupiga kura hii leo itakavyokuwa.Waingereza ni watu wa ajabu sana, kwanza wana uvivu wa kutopenda kuamka asubuhi sana ndo maana hata kazini wamejiwekea muda wa saa tatu kuanza kazi rasmi za kiserikali huku ofisi nyingine zikifunguliwa hata saa nne asubuhi.

Ikiwa hali ya hewa itakuwa ni ya mvua na baridi kuna uwezekano mkubwa working class people wasiende kupiga kura. Jamii hii ya wafanyakazi ndo wapiga kura na wanachama wakubwa wa Labour.Hivyo Labour pamoja na kuwa na faida ya kuwa swan a Conservatives lakini bado wanakabiliwa na changamoto hii na wanaomba mungu hali ya hewa iwe nzuri ili watu wao wajitokeze kupiga kura.

Kwa upande wa Conservatives wao kwenye maeneo yao ni wazi watu watajitokeza kupiga kura bila shida kwa sababu wanaungwa mkono na jamii ya watu matajiri na koo zenye uwezo kifedha.Ukitazama kwenye chambuzi za ramani ya Uingereza, maeneo ambayo Tories wana nguvu ni maeneo yenye utajiri au jamii za watu wenye uwezo kifedha, hawa wengi watawasha moto magari yao na kwenda vituo vya kupigia kura na kutekeleza jambo lao. Hawa huwa hawasumbuliwi na suala la mvua au baridi japo pia idadi ya watakaojitokeza inaweza kupungua.Ila kwa Labour na jamii ya wafanyakazi suala la hali ya hewa ni muhimu mno.

ED MILBAND Vs DAVID CAMERON.

ED VS CAMEROON

Hawa wote wana historia inayofanana, wakisoma Chuo kimoja na hata masomo yao wakisomea masomo yanayofanana.David na Ed wamesoma Oxford University, na wote wakisoma PPE(Philosophy, Politics and Economics) .

Cameroon amefanya siasa na kampeni kwa usadizi mkubwa wa wakongwe wa chama cha Conservatives wakati Ed akiachiwa jukumu peke yake la kuongoza kampeni peke yake, si kaka yake David Milband wala aliyekuwa waziri mkuu Tonny Blair ambao wamejitokeza kumpa ushirikiano wa moja kwa moja. Sababu kuu ni vidonda vya uchaguzi wa ndani ya Labour ambao ulishuhudia David Milband akikosa nafasi ya kuwa kiongozi mkuu wa chama.

Lakini Zaidi anaonekana ni mtu mwenye sera za mrengo wa kushoto Zaidi na ujamaa kuliko msimamo wa wengi ndani ya chama ambao walirejesha Labour madarakani kupitia New Labour madarakani.Jambo jingine ambalo linazungumzwa chini chini ni kuwa David Cameroon ni mwingereza halisi(Babu wa babu yake akiwa mmoja wa Wafalme wa Uingereza zamani hizo, King William IV) lakini Ed Milbannd anasemwa kuwa Mwingereza wa kuzaliwa lakini asili yake si Uingereza kwa kuwa wazazi wake walikuwa wahamiaji kutoka Ubelgji.

Ni Labour au Conservatives? Hili ndilo swali kuu ambalo majibu yake yatajulikana Saa chache zijazo.

Mwandishi:Van(Mtanzania aishie nchini Uingereza)

Leave a comment

name*

email* (not published)

website