Navigate / search

Mambo Mawili Yatakayokufanya Ufanikiwe Wengine Wanaposhindwa

Bannister.Mile. Times negs 146590 -146596 Sir Roger Gilbert Bannister, CBE (born 23 March 1929) is an English former athlete, doctor and academic, who ran the first sub-four-minute mile. This was finally achieved on 6 May 1954 at Iffley Road Track in Oxford, with Chris Chataway and Chris Brasher providing the pacing. When the announcer declared "The time was three...", the cheers of the crowd drowned-out the details of the result, which was 3 min 59.4 sec. RogerBannisterWorldRecord - Original image used in 1954 as a tight crop on page 8 of The Times on 07/05/54

Miaka mingi huko nyuma wataalamu wa mbio walihitimisha kuwa haiwezekani kwa mwanadamu wa kawaida kuweza kukimbia chini ya dakika 4 kwa maili moja.Kitaalamu iliionyesha kuwa sio tu HAIWEZEKANI bali pia ni jambo la HATARI kulijariibu kulifanya kwa mwanadamu yeyote yule.Wakimbiaji wengi sana walijaribu kuivunja rekodi hii bila mafanikio kwa maelfu ya miaka hadi wengine walitumia mbinu ya kuwachokoza n’gombe dume wenye hasira(bulls) ili waweze kuwakimbiza kwa haraka kuvunja rekodi hii ila walishindwa kabisa.

Lakini ilipofika May 6, 1954, Roger Bannister aliweka rekodi mpya kwa kukimbia kwa muda wa dakika 3 sekunde 59 an nukta 4.Alipoulizwa amewezaje kufanikiwa kwa kiwango hicho alisema kuwa alikuwa anafanya mazoezi kwa bidii lakini pia kila siku alikuwa anawaza kwa picha ya moyoni (visualize) kama vile tayari amekwisha kufanikiwa.Baada ya Roger kufanikiwa kuweka rekodi hii ,kila mwaka kumekuwa na watu wengi waliendelea kuiweka rekodi hii.

Kwenye maisha ndivyo inavyokuwa,mara nyingi kuna mambo mengi sana ambayo huwa yanaonekana hayawezekani na ni kama kila mtu amehitimisha kuwa haiwezekani kabisa kabisa,lakini ukweli ni kuwa tumezungukwa na fursa za kuweka rekodi mpya kwenye maisha yetu kila siku.Kuna mambo mawili ya muhimu ya kujifunza toka kwa Roger Bannister;

Moja ni kuwa hakukubali maoni ya kitaalamu na viwango vilivyoweka na waliotangulia vimkatishe tamaa.Katika maisha ya kila siku utakutana na maoni ya kitaalamu na maoni ya watu kwa namna mbalimbali.kuna ambao watakuambia kulingana na historia ya familia yenu hakuna mtu anayefanikiwa kielimu,kuna wengine watakuambia kwa mujibu wa historia ya ukoo na kabila lenu watu huwa hawafanikiwi kifedha,kuna wengine watasema Tanzania hatujawahi kuwa na mabilionea wa umri mdoog,wengine watasema haiwezekani kusoma huku unafanya kazi,wengine watasema uchumi ni mgumu hivyo haiwezekani kufanikiwa kibiashara mwaka huu;ili mradi kuna mambo mengi yatatajwa yasiyowezekana.Je kuna jambo linatajwa haliwezekani mahali ulipo?

Unachotakiwa kufanya ni kupuuza kila kinachosemwa hakiwezekani na amua kuwa wewe ndio utakuwa wa kwanza kuweka rekodi mpya.Hii ndio maana Nelson mandela alisema-“Kila wakati itaonekana haiwezekani hadi unapoamua kufanya”-(It will always seem impossible until it is done).Wakisema haiwezekani wewe waaambie-“Mimi nitakuwa wa kwanza kuweza”

Jambo la pili ni kuwa ukiamini kuwa inawezekana basi itawezekana.Najaribu kufikiria jinsi ambavyo ilikuwa ni ngumu kwa watu kubishana na ripoti za wataalamu waliobobea katika riadha kuwa jambo hilo lilikuwa la hatari na lisilowezekana.Najaribu kufikiria juu ya watu wengi ambao walimcheka na kumkatisha tamaa alipowaaambia kuwa anataka kuwa mtu wa kwanza kuweka rekodi hiyo,najaribu kufikiri kila alipojaribu na kushindwa watu walikuwa walikuwa wanamwambia maneno gani-Katika kuelekea mafanikio makubwa ni lazima utambue kuwa hata kama kila mtu haamini kuwa unaweza kufikia lengo lako,jambo la muhimu ni wewe kuamini kwanza kuwa unaweza na kujiona tayari umeshafanikiwa katika hilo na kuchukua hatua.

Kuna wakati katika kutekeleza ndoto yako,utajikuta kuwa hakuna mwingine anayeamini unachofanya isipokuwa mwenyewe;huo ndio wakati mzuri wa kukazana na kufanya bidii kuitimiza.Kumbuka kuna watu wengi hawataamini katika uwezekano wa wewe kufikia malengo yako hadi waone umeanza kufanikiwa kidogo,hivyo usisubiri kuona kila mtu anakuunga mkono,wengine watakukuta njiani umeshaanza safari.

Dunia ya leo inwahitaji akina Roger Bannister wengi katika kila field;hapo ulipo kwenye field yako kuna rekodi unaweza kuiweka bila kujali imechukua miaka mingapi ama watu wamesema haiwezekani kwa kiwango gani.Amini na chukua Hatua.

Je,wewe ni Roger Bannister Ajaye?

Endelea Kutembelea www.JoelNanauka.Com kujifunza Zaidi.

Kumbuka kuwa ndoto yako inawezekana.

See you At The Top.

Comments

Geophrey
Reply

Great word, nimejifunza jambo katika kutekeleza mpango nliojiwekea

nanauka
Reply

SAFI,SONGA MBELE

GERVAS
Reply

unaweza kunitumia hicho kitabu cha milionea next door na ni bei gani?

jacqueline mwasha
Reply

mimi ni zaidi ya roger,lazima ni nitimize ndoto na maono yangu katk maisha yangu,nimethibutu na ninaweza.kwa kweli narekebisha sehemu ndogo ndogo.asante pastor kwa kweli mafundisho yako yanazidi kunijenga na kunipa moyo.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website