Navigate / search

Mambo Mawili Ya Kuyafanya Ili Utoke Katika Hali Ngumu Inayokukabili.

 

Siku moja Mzee Mel Borchardt kama ilivyokuwa kawaida yake alienda kanisani kupiga kinanda kama sehemu ya vitu anavyovipenda.Cha kushangaza baada ya muda mfupi alipotaka kuinuka akagundua kuwa mguu wake uanshindwa kuinuika na mkono wake wa kushoto unashindwa kufanya kazi pia.Mawazo yakaanza kumuingia kujaribu kufikria afanye nini ili kukabiliana na hali hii.Mara akakumbuka kuwa kuna simu mahali na anaweza kuinuka na kwenda kuipiga ili amuite mke wake.Alipojaribu kuinuka akagundua kuwa hana nguvu za kwenda hata simu ilipo na upande mmoja wa mwili wake umekuwa mzito sana;hapo ndipo alipogundua kuwa amepooza upande mmoja(stroke).

Baada ya kuona kuwa ameshidnwa kabisa kufanya chochote,aliamua kusubirian hadi mke wake atakapokuja.Baada ya muda fulani mke wake Elsie alikuja na kumkuta katika hali ile na moja kwa moja alijua kuwa amepata stroke na hivyo alifanya juhudi ya kupiga simu ili awaite madktari.Wakati madaktari wanasubiriwa mzee Mel aliendelea kupiga kinanda kwa kutumia mkono wake mmoja.Na mara madktari walipofika na kumuona ;mmoja wao akamwambia-“Unapiga kinanda vizuri sana”-Bila kuchelewa Mzee Mel alimjibu na kumwambia.”Ahsante sana,ila ngoja nitakapopona na mkono wa pili utafurahia zaidi”.Kwa mshangao mkubwa kwa kuangalia umri wake na hali yake daktari Yule alijua kuwa haiwezekani kwa mzee Mel kupona haraka na kurudi katika shughuli zake za kawaida.Kwa kuona hali kama hiyo katika sura ya Daktari,Mzee Mel aliamua kusema kwa sauti-“Usiwe na wasiwasi daktari,mimi nitapona na nitarudi katika hali yangu ya kawaida”.

Siku zote akiwa hospitali hata wakati kila mtu alipokuwa anaona hali yake ni mbaya sana,yeye aliendelea kukiri kuwa ataweza kupona na kurudia katika hali yake ya kawaida.Na kwa mshangao wa wengi alikuja kupona na akaweza kutembea na kuendelea na upigaji kinanda aliokuwa anaupenda sana.

Hii inaitwa “Kun’gang’ania uanchokiamini kinyume na mazingira”.Kama unataka kufika mbali katika maishani lazima uwe mtu ambaye haukubali kuaminishwa katika mambo ya kukatisha tama  kama wengine wanavyosema.Kuna wakati unaweza kupitia hali ambazo kwa ukweli kabisa zitakuwa hazileti matumaini katika maisha yako na unaweza kujikuta unakubaliana na hali halisi na unafikia kiwango cha kukata tama katika maisha yako.

Kama mzee Mel angeamua kukubaliana na ukweli wa kidalktari kwamba haitawezekana kabisa yeye kupona pengine angeishi maisha yake yote yaliyobhakia akiwa katika hali hiyo.Lakini kwa sababu aliamini kutokea moyoni kuwa hakuna linaloshindikana,aliweza kusimama na kutembea tena.

Kuna wakati uanweza kujikuta chini kabisa katikia biashara yako,kazi yako ama chochote kile ambacho unafanya.Unaweza kujikuta kuwa kila mtu anakuambia haitawezekana tena,unaweza kuwa katika hali ambayo kila dalili inaonyesha kuwa umefikia mwisho na hakuna namna uanweza kuinukua tena-Unachotakiwa kufanya ni kuamini tokea ndani yako kuwa ianwezekana kuinuka tena na ukafanikiwa tena.

Inawezekana unapitia kipindi ambacho hali yako ya kiuchumi ni ngumu sana na huko nyuma mambo yalikuwa mazuri,inawezekana unapitia wakati mgumu sana katika masomo yako,inawezekana mahusiano yako yanapitia wakati mgumu sana na una jiuliza kama utaweza kuyanusuru ama kuyafurahia tena.Katika hali kama hii unatakiwa kufanya mambo mawili ya umuhimu:

Moja usikubali kufikai kiwango cha kuamini kuwa hautaweza kuinuka tena.Kuamini kuwa hautaweza kuinuka ni hatua ya kwanza ya kujiroga mwenyewe na kujifikisha mwisho kwa haraka.Kadiri uanvyoamini haiwezekani ndivyo kadiri unavyoifanya akili yako isione suluhisho hata kama suluhisho lipo.Kumbuka kuwa kwa mujibu wa kanuni ya uvutano (Law of attraction),mawazo yako yana nguvu ya kuvuta vitu,hali na watu ambavyo vinakuja kutimiza kile uanchowaza.Hivyo kama ukiwa na mawazo ya kukata tama basi unavutia kila kitu cha kukatisha tamaa.Ukianza kuona na kuamini kuwa hauwezi kuinuka tena basi utajikuta kila unachokiona na kinachotokea katika maisha yako kinapelekea kushindwa kwako sawasawa na unavyoamini.Ukitaka kuvutia fursa za kuinuka tena achana na mawazo ya kushindwa.Kuna watu wanawaza kusindwa hadi wanajikuta wanaota.Ukianza mawazo ya namna hii tu,usiyakubali-Jiambie:”Mimi si mtu wa kushindwa ni mtu wa kushinda,naamua kuwaza kushinda”

Jambo la pili ni kuhakikisha kuwa maneno yako yanaendana na kile unachokiamini.Kunan watu wengi sana nhuwa hawajui kuwa maneno yao yana nguvu sana katika kutengeneza hatima yao,hivyo wanajikuta wanasema tu hovyohovyo.Hivi umeshawahi kujiuliza kwa nini watu wakisemasema habari za wao kufa,unashangaa baada ya muda wanakufa?Mara nyingi ikitokea hivi huwa tunasema wamejitabiria lakini ukweli ni kuwa walitengeneza kifo chao.

Siku zote za maisha yako kumbuka kuwa maneno yako yana nguvu ya uumbaji(Creative Power).Kila unachokisema inamaanisha ni mbegu unayoipanda ili na itakuja kuota na siku moja utakuja kiuvuna.Hivyo kama hautaki kuvuna kushindwa basi usikubali kukiri maneno ya kushindwa katika maisha yako.Hata kama uko katika hali ngumu namna gani,usikubali kukiri kuwa haiwezekani ama hautainuka tena.

Kumbuka kuwa maisha yako ni matokeo ya yale ambayo unayakiri kila siku(Your current life reflects your past confessions).Kama unachukia maisha yako ya leo basi badilisha maneno yako.Anza kukiri ushindi hata kama mazingira na watu wanasema haiwezekani kabisa.

Hakuna hali ambayo haiwezi kubadilika,hakuna jambo ambalo halina majibu:Lakini siku zote kumbuka kuwa chanzo cha kwanza cha mafanikio yako ni aina ya mawazo unayowaza na pili ni aina ya maneno unayosema.Je uko katika hali ngumu kwa sasa kama ambayo aliwahi kuipitia mzee Mel?Unaweza kuchukua hatua zile zile ambazo alizichukua yeye,kwanza amini kasha umba unachotaka kwa maneno yako.Siku zote usizungumze mambo ambayo usingependa yakutokee kwenye maisha yako.

Hivyo basi,kwa kuamini kuwa  changamoto yoyote ile ambayo inakukabili kwa sasa ina majibu yake,anza kuwaza tofauti,zungumza tofauti na chukua hatua za kubadilisha maisha yako ukiamini kuwa utainuka tena na utashinda.

Kuna mtu maisha yake yanaweza kubadilika kwa kusoma ujumbe huu na akakushukuru,chukua hatua ya kushare ili wengine wanufaike pia na uchangie maisha yao.Unaweza pia kuagiza kitabu chako cha TIMIZA MALENGO YAKO ili ujifunze zaidi mbinu za watu waliofanikiwa ambazo nao pia walipitia hali kama hii na wakainuka na kufanikiwa tena.

See You At The Top.

 

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website