Navigate / search

Mambo Mawili Ya Kukutofautisha

Kwenye kila field(profession fulani au aina fulani ya biashara)  kuna waliofanikiwa sana na Kwenye eneo hilohilo kuna ambao wamefeli sana. Hii maana yake ni kuwa si sawa kusema ukiwa na taaluma fulani lazima utafanikiwa ama ukifanya biashara fulani lazima itakutoa.

Kinacholeta tofauti maishani sio kile unachofanya bali:

1)NAMNA unavyofanya :Ukifanya bila ubora (lack of excellence),ukifanya bila kuwa na maarifa ya kutosha,ukifanya kwa ulegevu(slothful hand),ukifanya namna hii hata tukikupa mgodi wa dhahabu baada ya miaka michache utakuwa maskini tena.

2)Tabia(CHARACTER ):Tabia ni Msingi wa uwezo. ukiwa mtu sio mwaminifu, Muongo, haupendi kujifunza,mgomvi .. Popote tutakapokupeleka utafeli.Kuna wengi wenye UWEZO na VIPAJI vya KIPEKEE lakini TABIA zao zimewaangusha.

Mafanikio ni zaidi ya nini cha kufanya(WHAT TO DO),ni muhimu zaidi kuzingatia HOW YOU DO(unafanya namna gani) na WHAT TO BE(Uwe mtu wa namna gani

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website