Navigate / search

Mambo Mawili Ya kufanya Ndoto Yako Inapoonekana Haiwezekani Kufanikiwa

Kwenye maisha yangu nimeshawahi kupitia wakati ambapo niliona kama vile ndoto yangu na malengo ambayo ninayo kwenye maisha ni kama vile hayataweza kufanikiwa tena.Hali hii sio tu mimi ambaye imewahi kunitokea,niliposoma habari za watu wengine nilikuja kugundua kuwa na wao pia wamepitia sana hali kama hizi na wengine ni mbaya zaidi kuliko ambazo sisi tumewahi kuzipitia,ila kilichowasaidia ni uamuzi wao wa kukataa kukata tamaa.


Ukweli ni kuwa ukipita katika hali kama hii basi utakutana na hali ya kuishiwa nguvu ndani yako na itakuwa ni kama vile hauwezi kuendelea mbele zaidi wkani utakuwa unaona giza limetanda kila upande wa maisha yako.Kuna mambo machache ambayo yalinisaidia ambayo naamini pia yatakusaidia na wewe:
Jambo la kwanza ni kutopoteza imani juu ya kesho yako kwa 100%.Ukweli ni kuwa ukipitia katika hali kama hii ni lazima unapoteza imani yako kwa asilimia kidogo ila usikubali kubakia na asilimia 0 ya imani juu ya kesho yako.Hii ni muhimu sana kwani hata kama utapoteza kila kitu kwenye maisha yako lakini ukabakia na imani yako basi utaweza kuinuka tena ila ukikubali kupoteza imani yako basi unakuwa umepoteza kesho yako yote.

 

 

Njia nzuri ya kujihakikishia kuwa unabakia na imani yako juu ya kesho yako ni kwanza kuhakikisha unakaa na watu ambao bado wanamini katika uwezo wako na wanakutia moyo kuhusu mafanikio yako.Kuna watu ukikaa nao huwa wana maneno ambayo utadhani ndio wanamalizi msumari wa mwisho kwenye jeneza la ndoto yako,watu wa namna hii ni lazima uwaepuke.Tafuta watu ambao bado wanaamini katika ndoto yako,wanaamini katika kesho yako;hawa ndio watu unaotakiwa kutumia nao muda mwingi kukaa nao.

 

 
Njia nyingine ya kutunza imani yako ni kusikiliza mafundisho ambayo yanakupa hamasa zaidi.Katika kipindi hiki unaweza usiwe na nguvu za kusoma ila unaweza kusikiliza.Tumia muda wako kusikiliza mambo ambayo yatakuwa yanakupa hamasa kila siku na kukutia nguvu,kumbuka kuwa imani huja kwa kusikia.Hivyo kadiri ambavyo unasikia zaidi ndivyo ambavyo utakuwa pia unaongeza imani juu ya kile ambacho unakitamanoi kitokee kwenye maisha yako.

 
Jambo la pili pata muda wa kutafakari kuhusu ndoto zako kubwa.Katika kipindi hiki nilichukua mahali nilipoandika ndoto zangu kubwa na nikawa najisomea na kujikumbusha.Kadiri ambavyo nilikuwa naendelea kusoma ndivyo uhalisia ulivyokuwa nazidi kujengeka ndani yangu na nikawa nazidi kupata nguvu.Kumbuka kuwa kadiri ambavyo ndoto yako inakuwa halisi kwako ndivyo inavyokupa hamasa zaidi kuifuatlia.
Kitu muhimu cha kujua kuhusu kufanikiwa kwa ndoto na malengo yako ni hata siku moja kutokubali kuamini kwamba umefikia mwisho.Kuna watu waliamini kwamba sitaweza kuinuka tena,lakini kupitia mambo haya mawili yalinisaidia sana kuinuka na kuendelea na safari.

 

 

Kama unapitia hali ya kukatisha tamaa basi unaweza kutumia mbinu hizi mbili kama haupitii kwa sasa nakushauri uzielewe na uzikumbuke siku utakapopitia.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website